Nini kinasababisha fuel consumption isiyo ya kawaida

Jimmie Gatsby

JF-Expert Member
Mar 7, 2013
3,588
7,254
Wana jukwaa naombeni msaada nina kausafiri kangu bhana ghafla kameanza kunitia hasara kwa ulaji wa mafuta usio wa kawaida...

Ni TOYOTA CAMI with 1.3 ltr petrol engine hapo mwanzo ilikuwa inakunywa mafuta kawaida yaani lita moja nilikuwa naenda kilomita 13 hadi 14 yani nikiweka full tank elfu 92000

Natumia hadi miezi miwili kwa matumiz yangu ya kawaida ambayo ni hayazidi km 10 per day sasa ghafla engine imechanganyikiwa inatumia lita 1 kwa kilomita 6 yani nimekuwa mtu wa kutembea na kidumu maana muda wowote mashine inakata wese ...

Naombeni kujua tatizo linaweza kuwa wapi maana kwa uzoefu wangu nikabadilisha spark plug..nikabadilisha fuel filter nikabadilisha air filter, nikabadilisha ignition coil lakini bado tatizo lipo palepale.

Msaada jamani mwenzenu naumia maana kagari kanakunywa mafuta kuliko range rover sport asee
 
Kwa nini mkuu uliamua ubadili vitu vyote hivyoo??…

Anyway mara nyingi ulaji wa mafuta kwa gari ndogo unaweza kubadilika ghafla iwapo tu air to fuel ratio itakuwa haiko katika usawa unaotakiwa…

Hivyo kwa gari ambayo inafanyiwa service kwa muda muaafaka kulikuwa hakuna haja ya wewe kuingia gharama ya kubadili hizo vitu vyote hapo juu….

Kwa kuanzia mpelekee Fundi umeme wa magari akuchekia Air flow sensor kama iko vizuri kiongozi.
 
The last don Asante sana kiongozi ngoja nifanya hivyo .... kuhusu kubadili hivyo vitu kuna kipindi nilikuwa na mark x ilizidisha ulaji na ikawa ina lose power nilivyobadilisha spark plug na coil ikawa sawa nikafikir na kwenye hiki ki CAMI itakuwa hivyo ila hali ikawa tofauti
 
mkuu the last don nashukuruuuuuu saaaanaaaaa na wadau wote mliosaidia kunipa ushauri.... juzi nilienda kwa fundi tukaipima gari ikagundulika ni sensor ya hewa... (mass air flow sensor) ila pale kwenye gari kimeandikwa pressure sensor tukakabadilisha tena hata siyo gharama kanauzwa laki moja ukijumlisha na hela ya diagnos 50k jumla imenitoka 150000 tuuu... alafu kadude kenyewe sasa hata mkononi hakajaiii ndio kalikuwa kananitesha .... kutoka pale tukaflash tank nikaweka wese la elfu kumi hadi now gari inasoma soma 50km bado haijazimaaa .... asanteni sana wadau

narudia kusema kuwa imeniumaa sana kugundua kakifaa kalichonitesa hakajai hata mkononi yani ndio kalisababisha gari itoke kula 14km per liter mpaka 5km per lita
 
Je engine inaenda kwenye RPM ngapi hadi kubadili gia tofauti na mwanzo?
Je gari ina nguvu?


GARI IMESHAPONA MKUU TATIZO LILIKUWA pressure sensor..(mass air flow sensor)

nijibu swali ulilouliza kuhusu (RPM) gari ilikuwa gia zote inachange RPM ya 3 na sometimes 4 kitu ambacho siyo cha kawaida maana nna gari nyingine ambayo ni 2.5 ltr V6 a very powerful lakin nisipo flow fuel pedal haifiki hizo RPM
 
Hongera mkuu, basi kami iko fuel efficient sana aisee. Huwa naifananisha na terios kid hio gari sijajua tofauti yake ni nini baina ya hizo gari mbili.
 
Aisee

Hongera mkuu, basi kami iko fuel efficient sana aisee. Huwa naifananisha na terios kid hio gari sijajua tofauti yake ni nini baina ya hizo gari mbili.

kiukweli fuel consumption ya CAMI ipo vizur plus ni mini SUV u get that huge ground clearence a four wheel drive basi raha mustarehee

kuhusu uhusiano wa CAMI/ TERIOS na CAMI KID/TERIOS kid

hili ni gari moja sema linatolewa na kampuni mbili likitolewa na toyota linaitwa CAMI kwa long chesis na CAMI KID kwa kile kidogo

hivyo hivyo akilitoa DAIHATSU analiita TERIOS kwa ile kubwa na TERIOS KID kwa vile vidogo.. mimi yangu ni CAMI toleo la toyota ile kubwa sio KID...

kwa sasa wapo generation ya PILI toyota akiitoa inaitwa TOYOTA CAMI / TOYOTA RUSH na DAIHATSU akiitoa anaiita DAIHATSU BEGO ila ni gari moja

ni kama toyota harrier na lexus 220g
au toyota Altezza na lexus is300
 
Petrol filter na plug feki huchangia hii hali

ahsante mkuu mshana jr hivyo vyote ukisoma hapo juu nilichange nikafunga vipya tena OG ila tatizo lilibaki palepale

kwa sasa gari iko fresh kabisa mafuta yangu ya 20k mimi mzungu kabisa hapa mjini

tatizo lilikuwa ni pressure sensor (mass air flow sensor) ilichanganyikiwa ikawa haitoi taarifa vizuri kwa ECU ni kiasi gani cha mafuta kinatakiwa kitemwe kwa kiwango cha oxygen inayoungia kwenye combustion chamber ikawa hewa inaingia kidogo yenyewe inapekeleka readings za uwongo matokeo yake mafuta yakawa yanamwagwa mengi..

na hayachomwi yote kuna kipindi nilikuwa nikiflow pedal hadi ndan ya gari naskia harufu ya petrol na moshi wake ulikuwa mkali sana yan ukiuvuta lazima kichwa kiume au kizunguzungu
 
Back
Top Bottom