Nini kinaikumba mikoa ya Tanga na Pwani kuwa wa mwisho kielimu kila mwaka?

Tunzo

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
4,023
2,298
Yani kila mwaka lazima hii mikoa iburuze mkia, kwenye shule 10 za mwisho mkoa wa Tanga huwezi kosa kuanzia shule 3 kwenda juu, vivyo hivyo unguja na pemba, unakuta wamelundikana kule chini kwenye mikia, nini shida,

Nimeangalia shule kadhaa za Tanga mjini, korogwe na Lushoto, yani ni balaa, matokeo ni mabaya sana, unakuta shule ina zero karibu watahiniwa wote, Div waliofaulu wana 4 tena wachache.

kuna wilaya kadhaa za Tanga kama Handeni, Kilindi, Korogwe, Lushoto, Muheza, Mkinga, Pangani na Tanga mjini.
Wilaya zote hizi zinakadiriwa kua na watu 2M na ushee, na kusema kweli swala la kielimu kwao si kipaumbele kwa jamii!

Inabidi hii mikoa ijitadhmini kielimu, Ndugu zangu Wasambaa, Wazigua Wabondei, Wadigo, Tafadhali muamke sasa, Mambo yakusifiwa katika mapenzi yamepitwa na wakati.

Na Nyie maafisa elimu wa mkoa, wilaya na kata mjitathmini upya.. mnyanyue hiyo mikoa si kila siku kuburuza mikia!

Mwaka huu naona Kilimanjaro nayo imeingiza shule moja, hahaa naona hiyo shule wamepiga zirotu, hiyo shule imeaibisha mkoa.

Pia na kwa Dar kuna shule moja naona imakamatia kule mkiani, hii nayo yakuamgalia, kama vipi ifute na kuhamishiwa shule zingine kama wanavyofanya mabenk ambayo yameshindwa kujiendesha.
 
kwanza tatizo linaanzia kwa jamii husika ukijumlisha na wazazi umoumo, hawana muamko kielimu.pili tatizo ni serikali nasema ivo kwasababu ili nitatizo sugu ilitakiwa serikali ifanye uchunguzi na kujua tatizo ni nini ikiambatana na njia za kutatua ilo tatizo, pia mila za jamii husika waangalie namna nzuri ya kupangalia sijasema zifutwe au zipigwe marufuku ila tu kuwe na mpangilio mzuri wa ratiba, mfano mtoto akitoka shule wenzetu upande wa pili watampeleka madraasa na siku nzima itaishia uko akirudi home amechoka hoi maana kuna mda wanapata na kipigo uko uko wakirud nyumbani wamechoka ata kujisomea masomo ya darasani hawawezi tena, pia kwa hawa wazaramo binti akishavunja ungo tu wanataka kumuweka ndani achezwe sasa iyo akili ya kusoma atatoa wapi?
 
Yani kila mwaka lazima hii mikoa iburuze mkia, kwenye shule 10 za mwisho mkoa wa Tanga huwezi kosa kuanzia shule 3 kwenda juu, vivyo hivyo unguja na pemba, unakuta wamelundikana kule chini kwenye mikia, nini shida,

Nimeangalia shule kadhaa za Tanga mjini, korogwe na Lushoto, yani ni balaa, matokeo ni mabaya sana, unakuta shule ina zero karibu watahiniwa wote, Div waliofaulu wana 4 tena wachache.

kuna wilaya kadhaa za Tanga kama Handeni, Kilindi, Korogwe, Lushoto, Muheza, Mkinga, Pangani na Tanga mjini.
Wilaya zote hizi zinakadiriwa kua na watu 2M na ushee, na kusema kweli swala la kielimu kwao si kipaumbele kwa jamii!

Inabidi hii mikoa ijitadhmini kielimu, Ndugu zangu Wasambaa, Wazigua Wabondei, Wadigo, Tafadhali muamke sasa, Mambo yakusifiwa katika mapenzi yamepitwa na wakati.

Na Nyie maafisa elimu wa mkoa, wilaya na kata mjitathmini upya.. mnyanyue hiyo mikoa si kila siku kuburuza mikia!

Mwaka huu naona Kilimanjaro nayo imeingiza shule moja, hahaa naona hiyo shule wamepiga zirotu, hiyo shule imeaibisha mkoa.

Pia na kwa Dar kuna shule moja naona imakamatia kule mkiani, hii nayo yakuamgalia, kama vipi ifute na kuhamishiwa shule zingine kama wanavyofanya mabenk ambayo yameshindwa kujiendesha.

Nikiitoa Tanga, Pemba & Unguja hawachelewi kukwambia Muungano ndo unao wafelisha
 
Back
Top Bottom