Nini kinafanya meno kuumia kwa hisia pindi mtu anaponoa kisu au kufikicha majani makavu ya mahindi?

Superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
13,395
33,798
Kuna huu ugonjwa ambao siujui jina iwe la kiswahili au kingereza ila uko hivi...;

Ukichukua kisu ukakinoa chini au;

Majani makavu kabisa ya mahindi uyafikiche au ;

Usugue chuma kwa chuma.

Meno hupata hisia ya maumivu Sana bila hata kuguswa.

Naifananisha hii Hali na maumivu ya mluzi kwenye busha (Kama ni kweli)

Je huu ni ugonjwa gani?
 
Mkuu hiyo mimi ninayo pia mtu akisugua sufuria kwa mchanga naskia meno yanauma kama ngazi ipo kwenye meno😁🤦🤪🏃
 
TEETH SENSITIVITY

If your teeth are particularly sensitive, the fluctuating pressure from sound waves can actually cause the water-filled tubes in your teeth to vibrate, especially at high-frequencies, and painfully irritate your pulp's nerves
 
Application nyingine ya "RESONANCE" ni miluzikwa mtu mwenye rusha nadhani umewahi kuona au kusikia
 
TEETH SENSITIVITY

If your teeth are particularly sensitive, the fluctuating pressure from sound waves can actually cause the water-filled tubes in your teeth to vibrate, especially at high-frequencies, and painfully irritate your pulp's nerves
Waelezee waelewe mimi sio muelezeaji mzuri, iweke kwa kiswahili
 
Hii nadhani maelezo yake yatakuwa yanafanana na wale wenye midadi,inapopigwa honi au ukimjambisha inampa tabu sana,hii ya pili wale wa mikoa ya pwani nadhani watakuwa wanaijua zaidi......
 
Ni kwa watu wachache maana wengine hatuna hio kuna mmoja yeye mkwaruzo wa yale yanayokaa ndani ya boksi jipya mfano umenunua redio kubwa yale meupe basi ukiyaburuza anakosa raha na kujisikia vibaya mno
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom