Nini kinaendelea ndani ya Club ya Simba?

Nimeona hii taarifa kwenye official page ya Club,mwenye kujua kwa undani nini kimefanyika huko Bunju.

View attachment 3641956
Mangungu ni mfa maji haachi kutapatapa anataka amrudishe tena Salim Abdallah 'Try again ' ili amsaidie kushinda uchaguzi wa mwakani

Mkutano uliopita Mangungu alidanganya kuwa serikali imeamua wawekezaji lazima wawe watatu kitu ambacho serikali ilikanusha kupitia naibu waziri wa michezo.
Lakini hata mapendekezo hayo hayakupigiwa kura kama utaratibu unavyotaka.

Mangungu na 'Try again' ndani ya miaka mitano Simba haijachukua ubingwa wa ligi kuu.
 
Kushanuka huko
 

Attachments

  • 1785687324585.jpg
    113.3 KB · Views: 8
Tajiri ajatoa pesa ya usajiri wa maana kila wakimgusa yeye anawakumbushia deni lake naona wakaamua kubadili uongozi kijanja huko Bunju na hao waliotemwa wametangaza hicho kikao ni batili wametangaza kikao rasmi kesho ngoja tusubiri kinachoendelea huko tutapata majibu tu..
 
Mangungu ameshafafanua waliokutana ni viongozi wa wanachama ambao Magori hausiki maana yeye ni upande wa Bodi ya mo.
Kwa kifupi Magori anatapatapa.
Nafikiri kuna shida kwa Mangungu.
Kwa Katiba ya Simba, viongozi wa wanachama hawawezi kuidhinisha majina ya wajumbe wa bodi ya wadhamini.

Inawezekana yeye ndio asiopenda utulivu ndani ya Simba. Huyo Try Again kila mwaka yeye, kabakisha nini Simba?! Bila shaka kuna zengwe wanalisuka.
 
Unazungumzia katiba gani?
Swala la wadhamini ni swala la wanachama na wale ni viongozi waliochaguliwa na wanachama labda kama wadhamini wanatakiwa kupitishwa na mkutano mkuu wa wanachama.
 
Unazungumzia katiba gani?
Swala la wadhamini ni swala la wanachama na wale ni viongozi waliochaguliwa na wanachama labda kama wadhamini wanatakiwa kupitishwa na mkutano mkuu wa wanachama
Wadhamini wanatakiwa wapitishwe na mkutano mkuu, huo mkutano mkuu umefanyika lini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…