Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,143
- 17,530
Mkuu wa Mkoa wa Arusha na mwanachama nguli wa Klabu ya Simba, Amos Makalla, amepinga vikali taarifa za uteuzi wake kuwa Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la Klabu ya Simba SC, akitangaza kuwa mchakato huo ni batili.
Soma: Magori: Kikao cha Bunju ni batili, haukuwa Mkutano Mkuu rasmi wa Simba
Kupitia ujumbe wake, Makalla ameweka wazi kuwa akiwa mwanachama anayeijua vyema Katiba ya Simba na taratibu zote za upatikanaji wa wajumbe wa baraza hilo, uteuzi uliofanywa umekiuka sheria na miongozo ya klabu.
Soma kuhusu Try Again arejeshwa Simba, aunda Baraza jipya la Wadhamini lililopitishwa na Wanachama Bunju
Kauli ya Amos Makalla: "Nimeona hii habari ya uteuzi kuwa mjumbe wa Baraza la Wadhamini la Simba. Mimi ni mwanachama wa club ya Simba nafahamu vyema Katiba ya Simba na mchakato wa kuwapata wajumbe wa Baraza la Wadhamini wa club ya Simba."
"Uteuzi huu ni batili, kwa sababu Katiba ya Simba haikufuatwa na mimi binafsi sikushirikishwa."