Ni lazima yawe magumu!... Tulikuwa tunamiliki sehemu ya ziwa hilo hata kabla ya makubaliano ya mwaka 1890 kati ya mjerumani na mwingereza. Kando ya ziwa kulikuwa na wanyasa upande wa malawi na wamanda, wanyakyusa, wakisi, n.k. upande wa Tanzania - kando ya ziwa. Makubaliano ya wageni yananyang'anya haki za wenyeji!!!!!!............. NINAWATAKIA KILA LA KHERI WATANZANIA WANAOSHIRIKI VIKAO HIVI WATETEE HAKI YA WATANZANIA!.. ...Inaelekea matokeo siyo mazuri, maana siku ya kwanza mbwembwe zilikuwa nyingi. Baada ya hapo media za Tanzania na Malawi ziko kimya, walioenda kujadili nao wako kimya! Hata balozi wetu aliyenza kwa majigambo sasa yuko kimya!!!
Naomba kwanza u declare interest kuwa wewe ni mnyasa maana post zako zote hazina uzalendo nashindwa kukuelewa wewe nimtanzania waina gani!hata kama kweli ziwa ni la wamalawi tunatakiwa tuonyeshe dunia mpaka saa ya mwisho kuwa tulilidai ziwa hilo hatuwezi kuliacha likachukuliwa kiholela hata wakichukua wawe wametoa jasho!Lakini wewe inaelekea hata walivyofukuzwa City water uliuzunika ndugu yangu Nikupateje maana swala lauzalendo nikama yangeyange na kupe!Hebu waeleze, internet imekuwa forum ambayo mtu anaweza kujionyesha ujinga wake mradi tu ID imefichwa.
Hapo kwenye RED ni RED kweli kweli. Kaaazi ipo!Mie napata hisia kuwa huu mpango ni wa muda mrefu hasa baada ya ile ramani kuonyesha hilo ziwa liko Malawi.Then hizi chokochoko zilipoanza,huyu mama alikubali haraka sana wazo la mashoga.kisha mama Clinton kapay visit huko,saa hizi Blair.Pengine ni mapema sana kuliongelea hili ngoja tusubiri.Lakini nina wazo moja.Kuna yule mzee aliandika vitabu vya Jiographia na alitengeneza ATLAS, anaweza akatusaidia.Kwa watu walo karibu naye wanaweza kutusaidia kwa hilo.Anaitwa Mzee Mbando.anaweza naye akatupa mchango wake,wakati wa kuchora ile ramani ya Tz,alielekezwa mipaka ni ipi.Ni wazo langu tu.
hakuna mwafaka wowote uliofikiwa mpaka sasa
Blair ni ugly monster, there is a blood plan behind the scene!
Umeongea kinyume hapa mkuuKukubali kupeleka shauri mahakamani ni ishara ya kutokuamini umiliki wa ziwa letu.
Umeongea kinyume hapa mkuu
Wamalawi wanalitaka ziwa lote. Wamekaa na kupata mtazamo wetu.Sasa kama wanaona hoja zetu ni dhaifu na wana ushahidi wa kuishawishi ICJ, kwanini wanasuasua kufanya hivyo?
Na sisi Tanzania kama tunaona tuna ushahidi wa ngoma dro kwanini tusipate ujasiri wa kuruhusu Malawi wapeleke hili suala ICJ
Suluhisho la haki hupatikana mahakamani.Na maamuzi ya mahakama yataheshimiwa na sisi sote
MY TAKE:Ziwa limeshauzwa hilo. Kinachofanyika hapo ni pre-emptive measures. Wanasheria hao wa nchi mbili wakutane ili wajadili ni jinsi gani Werema atajitetea kama mwanasheria wetu mkuu iwapo atatakiwa afanye hivyo siku za mbele
Mkuu, hili swala siyo la kupeleka mahakamani.
Hivi wakenya wakisema mlima Kilimanjrao ni wao na wanataka tupeleke kesi mahakamani, utakubali?
Ndio maana nasema kukubali kupeleka shauri mahakamani ni kukubali kuwa hatuna uhakika na umiliki wetu.
Kesi ikienda mahakani ni kuipunguzia Tanzania nguvu na kuwaongezea nguvu wamalawi.
Dah! Wakenya wakisema mlima ni wao hatutawapuuza tutajiuliza ni mamlaka gani inawapa nguvu ya kudai hivyo
Mkuu mahakama zimeundwa ili zitoe haki.
Unaonekana ukiwa kiongozi hutojali rule of law. Utakuwa dikteta.
Leo utapigana na Mmalawi, kama ulivyosema hata mlima Kilimanjaro ni controversial, kuna uwezekano wa kupigana na MkenyaConclusion yako siyo sahihi. Nikiwa kiongozi sitaruhusu mahakama za nje zipewe nguvu kuamua mipaka ya Tanzania.
Kiongozi anachotakiwa kufanya ni kulinda mipaka siyo kubargain mipaka.
per diems zitaliwa weee hadi basi
Leo utapigana na Mmalawi, kama ulivyosema hata mlima Kilimanjaro ni controversial, kuna uwezekano wa kupigana na Mkenya
Kagera nako Waganda wanasema yao. Utapigana vita ya tatu hiyo.
Rwanda/Burundi nao watasema kabla ya mkataba wa Ubelgiji na Mwingereza wa mwaka 1920 Kigoma ilikuwa upande wao.
Je utaweza kupigana vita hizo zote nne?
Mahakama ndiyo suluhisho. Migogoro mingi ya namna hiyo imetatuliwa na mahakama
Unaweza ukatetea mipaka yako kwa vita hata tukiwashinda wanaweza wakaamua kwenda ICJ
Mkuu mahakama zimeundwa ili zitoe haki.
the end justify the means. wakifanikiwa hamna tabu!
Hiyo ni nadharia tu. Unadhani wanaoshiriki kutatua mgogoro wa waisrael na wapalestina ambao ndio mgogoro mkubwa wa ardhi duniani hawajui kama kuna mahakama?