Niliposoma kuwa kuna waandishi wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka ya tresspass kwa kutaka kuripoti mazungumzo ya mpaka kati ya nchi yetu na Malawi nikapata picha kuwa kunaseriousness katika hili suala. Ni vigumu kubashiri mpaka sasa. Inawezekana barozi wetu ameonywa kwani ktk ule uzi wa Nyasa Times niliona wachangiaji walivyowashambulia viongozi wao wakidai anayepaswa kwa wa kwanza kukamatwa ni barozi watanzania kwa tabia yake yaku-post updates za mazungumzo ktk facebook page yake. Napata picha kuwa kwa hali ilivyo, tutalishwa mengi ya uongo so ni bora kusubiri mpaka official statement itakapotolewa. Kuhusu Blair, pengine siyo vizuri tukajadili ya watu. Ni bora tujadili yetu humu ndani. Tunayo matatizo mengi yanayohitaji maoni yetu kama lile sakata la ndugu zetu wanahujuma sensa ilihali makarani wanatoka dini zote.