Nini kinachokwamisha utekelezaji wa ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi jiji la Arusha?

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,768
21,246
Dar Es Salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha haya ndiyo majiji yetu pendwa hapa nchini na kuna (Dodoma) na (Tanga) haya huwa kama siyaelewi hivi.

Dar Es Salaam kuna Magufuli Bus Terminal, Mwanza kuna kituo Matata sana soon kinafunguliwa, Mbeya pia kipo kizuri hata hayo majiji mawili nayo as dodoma kile sijui cha ndugai labda na Tanga pale Kange ni vituo maridadi sana vya mabasi nchini.

Jamani waheshimiwa hapa namtaja Gambo, alipokuwa mkuu wa mkoa kulikuwa na sinema flani mpaka aliyekuwa waziri wa ardhi kwa wakati ule, mzee wa Isimani alienda kuangalia eneo la kujenga kituo kipya.

Huyu Gambo akiwa mkuu wa mkoa hadi alitoa kauli kuwa anampigia jeshi la mtu mmoja atoe pesa, bahati mbaya wkt ule Arusha ilikuwa chini ya mbunge wa CDM so ikasemekama haiwezekani na haitafanyika ujenzi kisa mbunge ni CDM!!.

Leo mbunge ni CCM hadi madiwani 99% ni CCM nini kinasababisha jiji la arusha kukosa stendi ya mabasi ya maana?.

Kiwanja kipo tayari na kilishasafishwa hadi malori, greda na mkandarasi tuliona kama yupo site ila baadaye na gafla hamna kitu, sijui ilikuwa geresha au nini!.

Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa, makamu wa Rais Mh. Philip Isidory Mpango, Waziri wa Ujenzi Makame Mbalawa pia mkuu wa mkoa wa Arusha mzee John Mongella, na ndg Gambo nakutaja nara ya tatu hapa sababu huu mchezo unaufahamu.

Nauliza, Nini kinachokwamisha utekelezaji wa ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi jiji la Arusha?
 
Habari bila picha hainogi
BLOG.jpg
 
Ubishi wengine walitaka ijengewe hapohapo stand ya zamani wengine walitaka iamishwe..
Ndio kuzozani miaka..

hadi waziri wa ardhi kuingilia kati.
Sasa hadi serikali kutoa eneo na waziri wa ardhi wakati ule, mh Lukuvi akaja na kamati ya bunge ya miundombinu wakafika ilipo hii ya sasa na safari ya kwenda kule VETA karibu na kijiji cha Laroi ambako waliangalia.

Alafu unakuja na stori ya ubishi wa wananchi kupinga mmh sijaelewa hapo!.


Karibu mikoa yote walipoamishia vituo vipya upinzani ulikwepo hadi raia walisema kule mbali hatutaenda, mwishoe nini kinachoendelea?.
 
Back
Top Bottom