Nini kimetokea kwa ndege yetu ya Bombardier kusukumwa?

H
Hicho Kigari cha kuvutia ndege hakiwezi kuwachanganya wapiga kura. Ila kwakuwa hili tatizo limetokea hicho Kigari kutanunuliwa na viongozi wa dini na wapiga kura wataitwa kwenda kukiombea. Hiyo hafla hawatakosa CDF, IGP & the likes
Hata trekta inatumika pia nimeona sehemu kadhaa, au niwapatie ile trekta yangu nini, 5m per month. Lakini inaonekana wana akili ndogo sana watanisumbua.
 
Tatizo nyie ni washamba, mpaka unakufa utaishia tu kuiona angani basi!

Sent using Jamii Forums mobile app
Huku nilipo ulinibeba mgongoni nadhani wewe na ukoo wako hamjawahi hata kupata free ticket from airline baada ya kukava milage ya kutosha

nimesha enjoy 3 times from the Emirates ambayo nina uhakika hutakaa uipate wewe na jamii yako yote katika maisha yenu hapa duniani
 
Watanzania mmenishinda, huyu raisi MAGUFULI kuna kipindi alikuwa waziri, akasikia Watanzania wakisema CCM imeua shirika letu la ndege, naamini moyoni akaahidi kwamba siku nikiwa raisi nitalifufua, alipoupata uraisi akaamua kulifufua, sasa yanayomkuta nafikiri anajuuta kuwajua Watanzania. HII ndiyo siasa.
Mkuu anafanya mambo lakini hovyo hovyo, badala ya kujenga reli standard gauge ya njia 2 yeye anajenga ya njia 1, makosa.
 
Write your reply...Mna ushajidi kuwa hiyo ndege ni ya Tanzania............ maana nyiye msone kitu....Tanzania.... mnafikiliwa nnnn.......
 
Tumetoa maoni kulingana na clip hiyo ya video inavyo onesha. Ndege inayo andaliwa kuruka inahitaji wasukumaji ili iruke?

Mamlaka ya viwanja ndio imetoa starter kwenye ndege?

Sent using unknown device
Kama hujui utaratibu wa ndege kutolewa apron na kuwekwa tayari kuruka uliza usionekane choko. ndege haina mfumo wa kurudi nyuma yenyewe. Ndio maana kuna magari maalum ya kusukuma inapohitajika.
 
Kama hujui utaratibu wa ndege kutolewa apron na kuwekwa tayari kuruka uliza usionekane choko. ndege haina mfumo wa kurudi nyuma yenyewe. Ndio maana kuna magari maalum ya kusukuma inapohitajika.
Umewahi kupanda ndege za masafa marefu?
 
Zinaitwa terrible teens

Jr
Mshana Daaaah....nimecheka mpaka machozi....Terrible teens.Zikaanza kuanguka kama Maembe ndio tutaelewa maana ya neno Bombadia...Hii nchi ndege kama daladala.Abiria tutakuja tuzisukume sana hizo ngoma..ile sijui Drimulina ina makovu kovu nayo....hahahaha
 
Mkurugenzi wa Air Tanzania amesema kuwa ni kweli kuwa ndege yetu imesukumwa kurudi nyuma katika uwanja wa Ndege wa Zanzibar baada ya Rubani kuingia kwenye Runway iliyokuwa imefungwa.

Kwa Mujibu wa maelezo yake ni kuwa Uwanja wa Zanzibar hauna magari maalum ya kusukuma ndege kurudi nyuma.

TUJIFUNZE.

Kitendo cha kusukuma ndege kurudi nyuma ni cha kawaida kabisa pindi inapolazimu kufanywa hivyo.

Kitendo hiki huitwa "Aviation Pushback" kitaalamu na kwa lugha ya wenzetu hutafsiriwa hivi:-

Aviation, pushback is an airport procedure during which an aircraft is pushed backwards away from an airport gate by external power.

Pushbacks are carried out by special, low-profile vehicles called pushback tractors or tugs.

Kwa nini husukumwa kwa kutumia External power?

Ndege husukumwa Kurudi nyuma kwa kutumia nguvu toka njee kuepuka kuleta madhara kwenye engine. Si kwanba ndege haiwezi kurudi nyuma yenyewe lah Hasha Ila kitaalamu ukitumia gia kuirudisha nyuma huleta madhara makubwa kwenye engine.

Kuna mlolongo wa sababu:-

√. Ndege hurudishwa nyuma kwa External power kuepuka makelele ya engine.

å Hurudishwa nyuma kwa kutumia External power kwa sababu Pilot anakuwa haujui uwanja vizuri kama anavyoujua dereva wa Tugs au Tractor.

å Hurudishwa nyuma kwa kutumia External power kwa Sababu dereva wa Tugs anauwezo wa kuona mazingira yanayozunguka ndege si rahisi kwa rubani kuona nyuma.

å Ni njia nzuri ya kubana matumizi ya mafuta.

å Ni njia nzuri ya kuzuia uharibifu wa engine kwa kuwa kitendo cha kurudisha nyuma kwa kutumia gia engine hufyonza mchanga.

Fuata link link hii kujifunza zaidi..

https://www.quora.com/Why-do-flight...-from-the-gate-then-goes-out-on-to-the-runway

Ndege zetu ni nzima kabisa na Mkurugenzi kathibitisha hilo.

Tuwe mabalozi wazuri wa Mali zetu wenyewe. Tusiwajengee hofu abiria wanaotumia shirika letu la ndege.

Faida inayopatikana ATCL ndio inayotulipa mishahara sisi wafanyakazi, ndio inayonunua madawa, ndiyo inayo tengeneza mabarabara na ndiyo inatumika kutoa Elimu Bure.

Tunaweza kuendelea kupingana kwa itikadi Ila si kuhujumu maendeleo yetu.
 
Ila jamaa wana msuli kusukuma pipa! Labda ile gari ya kuvuta ilikuwa mbali.kawaida sana Ndege kuvutwa
 
Back
Top Bottom