Je, kuna uhusiano kati ya tairi za ndege na injini?

DIDAS TUMAINI

JF-Expert Member
Nov 11, 2014
232
651
Magurudumu (Tairi) za ndege hazina kiunganisho wala husiano na injini za ndege iwe Pangaboi au Jeti.

Gurudumu huzunguka huru kama toroli au au kiti cha kusukuma "wheel chair" isipokuwa tu zimefungwa mifumo ya breki, mifumo wa kona na mifumo ya 'hydraulic' ya kuvuta tairi ndani au kutoa nje kwa ndege zinazoingiza tairi.

Magurudumu ya ndege ni huru 'freewheel' ambayo hufuata ndege inaposukumwa injini hivyo hakuna 'propeller shaft, 'chain' wala 'belt' yeyote na haifanani na mifumo ya uendeshaji wa vyombo vingine vya moto kama magari.

Kazi ya injini za ndege kusukuma upepo nyuma kwa kasi kubwa ambayo hupelekea ndege kwenda mbele (action & reaction)
Unaweza sema injini za ndege za jeti ni mfano wa 'compressor' kubwa za kufua upepo, kukusanya na kusukuma nyuma kwa kuongezwa nguvu ya mafuta na viwashio, na kwa pangaboi pia hutumia panga zake kusukuma hewa nyuma.
Tafuta makala uchambuzi za nyuma inayosema 'aina ya injini za ndege'

Mara nyingine utaona trekta maalumu (tow truck/tug) hutumika kusukuma au kuvuta ndege kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Kama ilivyo panga za meli chini kusukuma maji kwenda nyuma kisha Chombo kuelekea mbele, pia hali ndivyo ilivyo kwa ndege kusukuma upepo nyuma ili ndege kuelekea mbele.

Kwa nguvu ya upepo unaovutwa, kufuliwa na kusukumwa nyuma ya ndege (Jet blast) mfano kwenye Boeing777, Boeing787, Boeing747, Airbus380, Airbus330 n.k unaweza kuangusha Gari la ukubwa wa 'Bus endapo likatiza nyuma ya ndege ikiwa imewasha injini katika nguvu ya mwisho (full power). Kwa binaadamu ni sawa na mbu kukatiza mbele ya feni.

Kumbuka ndege inapopaa tairi hazina matumizi tena hadi wakati wa kutua.Mfumo mzima wa tairi za ndege unaitwa 'Landing Gear'.
 
Asante kwa somo, nilijua wakati wa ku take off ni lazima i accelerate kwa kutumia matairi mpaka pale itakapokua angani.
 
Sawa ila unaweza ukaitembeza kama gari
Yas, kwa kuwa kuna gari na pikipiki za kuvunjia rekodi nazo zinafungaga injini za jet propulsion.

Ila kuna stori, kuna jamaa alifunga hiyo injini kwenye boti. Kaenda spidi kavunja rekodi ya dunia kaenda kagonga wimbi kila kitu kikapasuka afa na kufa. Jet injini sio kitoto mzee

Kwanza inataka kusiwe na watumiaji wengine wa 'barabara'
 
Kwahiyo Ndege Ikiwa Full Power Hairuhusiwi Mtu Kumangamanga Nyuma Ya Engine
Anaweza Kutupwa Mbali Huko
 
Back
Top Bottom