Nini kimesababisha CHADEMA wajitenge na UKAWA?

Nini kimesababisha CHADEMA wajitenge na UKAWA?

Sio tu harusi imefanyika tarehe 25 Oktoba 2015 lakini waume waliingia ndani na harusi ikajibu(kizinda kuraruliwa).Ndoa haikuvunjika isipokuwa mwari kakimbizwa kuikimbia fungate! Huko aliko tuna lala tukiamka nae!
Vigezo vilivyotumika ni vya Mirembe,Dodoma Makao Makuu ya CCM!

Masele kawaumbua leo bungeni, hio ndio story iliyopo, inayohit na jana ni Jenista kuzomewa na wabunge wa CCM.
Muda si mrefu UKAWA utatumika kuwamaliza CCM na Mamluki wao.
Sawa mkuu, lakini kwa taarifa nilizo zipa kupitia yule njiwa mpeleka salamu, kwamba bwana harusi alipomfunua mwali akakuta sio yule aliyemtolea posa, bwana harusi akakasirika na kuanza vunya vunya chupa zote za vinyaji ikawalazimu waliokuwa kariku kutimua kila mtu kwake na harusi ikavunjika nadhani tukio hilo lilitokea tarehe 5/11/2015 kama sikosei.
 
Lizaboni umechuja sana maana kila saa kila dakika ni wewe na chadema na UKAWA. Masele kawaumbua leo bungeni, hio ndio story iliyopo, inayohit na jana ni Jenista kuzomewa na wabunge wa CCM. You better keep quiet Madame
Madame tena?

Kumbe huyu jamaa-LIZABONI ni mwanamke?

Basi ndiyo maana ana maneno mengi!
 
Ukawa wamebaki na chadema Huku msemaji akiwa ni Mbatia Halafu Lengo ni kuitoa au kuifuta cuf kwenye ramani ya siasa Tanzania ghafla mtu mwenye uwezo MKUBWA ambaye pia Cv yake waliobaki ukawa Hata robo hawaijui na ni Pekee aliyeitwa kujadili kinachoitwa na wanoijiita Wataalam ku-stabilize Anguko la uchumi wa marekani si mwingine ni Profesa wa uchumi ndugu Ibrahim lipumba kukinusuru hapo ndipo...... Jamani nitamalizia baadae nikiruhusiwa na lizaboni
Huyo Lipumba alikuwa CCM kipindi cha Mwinyi alikuwa mshauri wake wa uchumi na ana CV kali kushinda Marais wote wa Tanzania. Kwanini CCM hamumchukui kuwa Mwenyekiti wenu wa Chama mna mpa kazi za kijinga tu, na mmewaagiza Askari polisi wampigie Saluti anapozoa taka. Tuambi mmempa cheo gani huko ccm?
 
Sawa mkuu, lakini kwa taarifa nilizo zipa kupitia yule njiwa mpeleka salamu, kwamba bwana harusi alipomfunua mwali akakuta sio yule aliyemtolea posa, bwana harusi akakasirika na kuanza vunya vunya chupa zote za vinyaji ikawalazimu waliokuwa kariku kutimua kila mtu kwake na harusi ikavunjika nadhani tukio hilo lilitokea tarehe 5/11/2015 kama sikosei.
Hadithi hiyo niliisikia, tena ni nzuri yakupigiwa makofi, lakini siku iliotokea sio tarehe 25 Oktoba 2015. Iliotokea tarehe nyengine,pengine ulioitaja kama ni sahihi

Ni kuwa Bwana harusi kwa kuogopa vishindo vya kungwi na wifi wakati wa kuingia ndani akalazimisha harusi iwe ya siri na waalikwe watu kidogo wenye usuhuba wa karibu tu. Lakini hilo halikusaidia kitu,alipotaka kuingia ndani "jongoo" kagoma. Mambo yakabidi kufichwa fichwa kuinusuru siku!

Wako waliosema Ndoa haikusihi kwa vile mikaha haikufanyika, wengine wakasema ni batili, wengine wakasema inajuzu hata kama Jongoo hakupanda mtungi kwa vile ilikuwa huru na haki na kwa mujibu na maelezo ya kungwi.Allahu ya'alamu.
 
Wabunge wa CCM washachoshwa na usanii wa serikali ya baba Jes.ca. Umemsikia mbunge wa Msolwa aliichana serikali yenu huku akishangiliwa na wenzi wake?
 
Back
Top Bottom