Nini kimemuua chura?

Boloyoung

JF-Expert Member
Aug 24, 2015
682
652
Ukimweka chura kwenye maji na ukaanza kuyachemsha maji, kadri joto la maji linavyozidi mwili wa chura utakuwa unajibadili joto lake pia kuendana na lile la maji. Chura ataendelea kuongeza joto la mwili wake kadri maji yanavyozidi kuchemka.

Maji yatakapochemka sana ( yakifikia boiling point) chura hataweza tena kuongeza joto lake ili liendane na la maji hivyo ataamua kuruka nje.

Chura atajaribu kuruka lakini hatoweza, kwakuwa atakuwa amepoteza nguvu nyingi wakati akibadili joto la mwili wake pale awali ili kuendana na joto la maji.

Hivyo hatimaye chura atakufa.

Nini kimemuua chura?

Wengi mtasema kauawa na maji ya moto...

Lakini ukweli ni kuwa kilichomuua chura ni kukosa uwezo wa kuamua mapema kuruka nje ya maji.

FUNZO:
Lazima tujifunze jinsi ya kubadilika kulingana na watu na matatizo yanayotuzunguka kila siku.

Tukiruhusu watu kutuvuruga kimwili, kiakili, kihisia, au kifedha basi wataendelea kufanya hivyo daima.

Tunatakiwa kuamua kuruka nje ya maji, tunatakiwa kuruka kabla maji hayajachemka sana.

3aa56c0e981d6e1e1b83937582a8d22b.jpg
 
Mojawapo ya topic adimu na za kipekee ndani ya JF ...imekaa vizuri sana Barikiwa
 
Nimesoma dodoma kuna vyura wakubwa kipindi cha mvua huwa unaweza kumkanyaga ukidhani ni jiwe.

Wenyeji wa huko wanawatumia kama kitoweo, wanamchukua mzima wanaweka katika sufuria vyura kadhaa wanaweka maji inabandikwa jikoni kisha juu ya mfuniko wa sufuria linawekwa jiwe zito sana. Maji yakianza kuchemka vyura hufurukuta na kama mafika au jiwe uliloweka sio zito basi unaweza kukosa kitoweo siku hiyo.

Wakiiva wanatolewa ndio wanakatwa fresh na kuchanganywa kwenye mboga, siku ukienda kwa mgogo ukila unaweza kula chura.

Wenyeji wa dom njooni mtuambie fresh
 
Back
Top Bottom