GE2025 Nini kimempata Fatma Karume?

GE2025 Nini kimempata Fatma Karume?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Ozon

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2024
Posts
2,366
Reaction score
3,687
Hivi karibuni, Fatma Karume ameonekana kubadili mwelekeo wa mijadala yake ya kisiasa kwa namna ambayo imeibua maswali miongoni mwa watanzania, hasa wale wanaoamini katika harakati za mageuzi ya kweli.

Mwanzo, alivamia vikali kauli za Askofu Gwajima aliyekuwa anapinga matukio ya utekaji na ukiukwaji wa haki unaodaiwa kufanywa na vyombo vya dola, akimtuhumu kuwa anatafuta "attention" ya kisiasa, licha ya kwamba hoja za Gwajima zilikuwa na uzito wa kulinda utu na uhuru wa raia.

Sasa, ameibukia tena kwenye mtandao wa X (zamani Twitter), akizibeza juhudi za CHADEMA na sera yao ya "No Reforms, No Elections", akikariri kuwa kusitisha uchaguzi ni kosa la jinai. Kauli hii imechukuliwa na wengi kama kejeli isiyoakisi hali halisi ya mazingira ya kisiasa nchini, ambapo haki za msingi, uhuru wa kisiasa na uhuru wa kutoa maoni vinaendelea kukandamizwa.

1751952289004.png

Moja ya post ya Fatma Karume

Cha kushangaza zaidi, kauli hizi za Fatma Karume zinatolewa wakati ambapo Tundu Lissu, mmoja wa viongozi wa upinzani na mwanasheria mwenzake, yuko rumande akikabiliwa na mashtaka ya uhaini, ambayo kisheria adhabu yake ni kunyongwa hadi kufa. Hali hii imezidi kuzua maswali: je, Fatma Karume bado yupo upande wa watetezi wa haki, au amebadili msimamo kwa sababu ambazo bado hazijafahamika wazi?

Ikumbukwe kuwa katika utawala wa Hayati John Magufuli, Fatma Karume alijitokeza kuwa mmoja wa sauti thabiti zilizokuwa zikikemea dhuluma, ukandamizaji, na matumizi mabaya ya madaraka. Lakini katika utawala wa sasa, ambao nao umeonesha mwelekeo wa kukiuka misingi ya demokrasia, sauti yake imekuwa ya mashaka, wakati mwingine ikisikika kama ya kukubaliabiana na mfumo badala ya kuukosoa.

Je, ni mabadiliko ya kiitikadi? Ni mkakati wa kisiasa? Au kuna mambo ya ndani zaidi ambayo bado hayajawekwa wazi kwa umma? Kwa vyovyote vile, hatua na kauli za Fatma Karume zinahitaji tafakari, hasa kwa wale wanaoamini katika dhana ya "principled activism" yaani, kupigania haki bila kujali nani yuko madarakani.
 
Hivi karibuni, Fatma Karume ameonekana kubadili mwelekeo wa mijadala yake ya kisiasa kwa namna ambayo imeibua maswali miongoni mwa watanzania, hasa wale wanaoamini katika harakati za mageuzi ya kweli. Mwanzo, alivamia vikali kauli za Askofu Gwajima aliyekuwa anapinga matukio ya utekaji na ukiukwaji wa haki unaodaiwa kufanywa na vyombo vya dola, akimtuhumu kuwa anatafuta "attention" ya kisiasa, licha ya kwamba hoja za Gwajima zilikuwa na uzito wa kulinda utu na uhuru wa raia.
Sasa, ameibukia tena kwenye mtandao wa X (zamani Twitter), akizibeza juhudi za CHADEMA na sera yao ya "No Reforms, No Elections", akikariri kuwa kusitisha uchaguzi ni kosa la jinai. Kauli hii imechukuliwa na wengi kama kejeli isiyoakisi hali halisi ya mazingira ya kisiasa nchini, ambapo haki za msingi, uhuru wa kisiasa na uhuru wa kutoa maoni vinaendelea kukandamizwa.
Cha kushangaza zaidi, kauli hizi za Fatma Karume zinatolewa wakati ambapo Tundu Lissu, mmoja wa viongozi wa upinzani na mwanasheria mwenzake, yuko rumande akikabiliwa na mashtaka ya uhaini, ambayo kisheria adhabu yake ni kunyongwa hadi kufa. Hali hii imezidi kuzua maswali: je, Fatma Karume bado yupo upande wa watetezi wa haki, au amebadili msimamo kwa sababu ambazo bado hazijafahamika wazi?
Ikumbukwe kuwa katika utawala wa Hayati John Magufuli, Fatma Karume alijitokeza kuwa mmoja wa sauti thabiti zilizokuwa zikikemea dhuluma, ukandamizaji, na matumizi mabaya ya madaraka. Lakini katika utawala wa sasa, ambao nao umeonesha mwelekeo wa kukiuka misingi ya demokrasia, sauti yake imekuwa ya mashaka, wakati mwingine ikisikika kama ya kukubaliabiana na mfumo badala ya kuukosoa.
Je, ni mabadiliko ya kiitikadi? Ni mkakati wa kisiasa? Au kuna mambo ya ndani zaidi ambayo bado hayajawekwa wazi kwa umma? Kwa vyovyote vile, hatua na kauli za Fatma Karume zinahitaji tafakari, hasa kwa wale wanaoamini katika dhana ya "principled activism" yaani, kupigania haki bila kujali nani yuko madarakani.
Mtu aliyeponea Rehab baada ya kuwa na uraibu wa dawa za kulevya ni wa kumwamini?

Yule ni mpuuzi kama wapuuzi wengine tu. Wanaomsikiliza nao wana shida ya akili.
 
Kuna post aliwashutumu chadema kwa udini,kashtuka,kaujua muundo wa wadini,kajiweka kando, kupitia mitandao fitna inageuka,wadini na walioweka misingi hiyo hawatofika kokote
Lakini mbona inaonekana kama yeye mwenyewe ndiye anayetoa taswira ya udini kwa namna alivyojenga hoja zake dhidi ya shutuma alizozitoa Gwajima? Badala ya kujibu kwa msingi wa hoja au ushahidi wa kimantiki, hoja zake zinaonekana kujengwa juu ya misimamo inayogusa hisia za kidini.
 
Duh! Atashika jani au shela!? Lakini huyu si anatokea katika ukoo wa kifalme?
Ni kama watoto wa princess Diana tu. Ufalme wameudhibiti mikononi mwao? Wana uhakika wa kesho yao? Yule kamuoa Katherine, akatengwa kiaina. Huyu akakosoa serikali na kuegemea upande wa ukimzani, akachukiwa. Wote wameanza kurudi na kukumbuka kudeka kwenye miguu ya "baba" zao. Nadhani tupo wote!
 
Ni kama watoto wa princess Diana tu.Ufalme wameudhibiti mikononi mwao?Wana uhakika wa kesho yao?Yule kamuoa Katherine,akatengwa kiaina.Huyu akakosoa serikali na kuegemea upande wa ukimzani,akachukiwa.Wote wameanza kurudi na kukumbuka kudeka kwenye miguu ya "baba" zao.Nadhani tupo wote!
Kazi kweli kweli… mtaani kwa moto
 
Back
Top Bottom