Nini kimekufanya ukawa baba/mume bora?

Nini kimekufanya ukawa baba/mume bora?

Samedi Amba

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2018
Posts
227
Reaction score
178
Dunia yetu ya leo inawiwa na baba wote ambao wameonyesha ubora. Ambao wamewalea watoto wao katika maadili mema. Ambao pamoja na kuwa ndoa zao sio kamilifu, walikataa kuwa wanyanyasaji, kuwapiga wake zao, au kutafuta michepuko. Wanawapenda wake zao jinsi walivyo, na kuweka mazingira bora nyumbani.

Je, unaamini kuwa wewe ni baba bora? au mtaani/kazini kwako kuna baba ambaye anakuinspire? Naomba kujua kile kinachomfanya mtu kuwa mwamba wa kweli, mwanamume aliyesimamia maadili toka ndani hata nje...
 
Shida ya humu kila mtu atajifanya baba bora, ukileta mada ya micharuko kila mmoja atadai anao wakutosha. Uwezi kupata ukweli wa watu humu wengi wanafake. Binafsi yangu sijawai funja uwaminifu kwenye mausino yangu japo kipepo cha ngono hakiko mbali sana na mimi kila siku shobo zinakua nyingi (sijui kwanini ukiwa kwenye mausino hii hali inakuwepo mara nyingi tofauti ukiwa single)
 
Wapo wanaoweka mazingira mazuri sana nyumbani na nje wanamichepuko
 
Uzi unawasuta mioyo yao kamwe awawezi jitokeza....funga karatasi mpee muuza vitumbua afungie wateja hakuna mchangiaji hapa🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom