Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,886
- 2,766
- Thread starter
- #41
Sikubaliani na wala siamini maneno yanayotolewa kwamba Profesor Mwakyusa alimpuuza Mwalimu Nyerere wakati wa ugonjwa wake uliopelekea kifo. Tutambue kama daktari bingwa Mwakyusa hakutarajiwa kumfanyia "Nursing" mgonjwa wake kwa kukaa naye masaa 24. Pia Mwakyusa Kama daktari bingwa aliendelea kumfanyia uchunguzi wa vipindi (periodic check ups) bila kuhitajika kuhamia Butiama na kuyaacha majukumu yake mengine na wagonjwa wake ( Uzi huu unataka kutuaminiisha kuwa hicho ndicho alichotakiwa kufanya). Kwakua Mwalimu alikua anaishi Butiama ni dhahiri alikua anaonwa na daktari aliye karibu Kama huyo daktari anaye tajwa.
Wakuu tuache kuchokonoa mambo ambayo hakika hatuna uthibitisho nayo na wala hatuna nia na wala uwezo wa kupata ukweli. Tunajivunjia hadhi kudakia mambo ya hisia za WATU ambao baadhi Yao afya ya akili zao inautata.(questionable mental health).jamii yetu inajiongezea ujinga kutokana na uvivu wa kuzisaka na kupata taarifa sahihi mfano kuna WATU wanaamini kwamba babu Seya alisingiziwa wakati wangeweza kwenda mahakama ya kisutu kupata mwenendo wa kesi na kusoma ushahidi wa watoto tisa wenye umri kati ya miaka 8 na 12 halafu ndio waseme amesingiziwa au la.
kwa mfano wako wa mwisho unataka tuamini kuwa Mwakyusa hasingiziwi sio? Jambo ambalo ni ujinga kwako, kwa mwenzio ni elimu tosha, so kuwa mpole na ukweli utajulikana hapa