Nini kilipelekea mpaka ukajiunga katika jukwaa la jamii forums?

Nini kilipelekea mpaka ukajiunga katika jukwaa la jamii forums?

Holoholo-Baba Kijacho

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2023
Posts
6,950
Reaction score
14,422
Wakuu,
Kila mmoja wetu humu jukwaani ana stori yake ya kuvutia,kusisimu na kushangaza ya kwa nini alijiunga jf!

Wapo waliovutiwa na stories za mapenzi,siasa,michezo nk.

Kwa upande wangu stori yangu iliyosababisha nikajiunga kujiunga jf ni ndefu ila ya kuvutia,niliwahi kumsimulia mshamba_hachekwi katika uzi flani,atakuja asimulie hapa.

Dondosha chanzo cha wewe kujiunga jf.
 
Mimi kusema ukweli jf nimeifahamu mwaka 2012 nilikuwa naingia kupitia kompyuta za chuo.
Kuna memba nilikuwa nawakubali kama mshana jr,otorong'ong'o, rala 1, Ambiele kiviele , gentamycine(popoma aliyetukuka) Nilikuwa nafurahi sana .
 
Nakumbuka nilikuwa natafuta matario fulani mtandaoni hapo chuoni ndio nikaiona jf nikaanza kusoma
 
Mimi kusema ukweli jf nimeifahamu mwaka 2012 nilikuwa naingia kupitia kompyuta za chuo.
Kuna memba nilikuwa nawakubali kama mshana jr,otorong'ong'o, rala 1, Ambiele kiviele , gentamycine(popoma aliyetukuka) Nilikuwa nafurahi sana .
stori yako inavutia.
 
Nimeifahamu jf toka nipo shule ya msingi kule kivinje..
Kipindi hiko natumia free basic alafu nina kiswaswadu...

Nilikua naingia kwenye ule uzi wa picha za vichekesho sijui....

But kujiunga rasmi nilijiunga baada ya kuvutiwa na huyu mwamba wa physics afrika masharik na kati Baba Swalehe...

Kwa kuwa physics ndo alikua kama mtu wangu wa karibu kipindi hiko nikaona bora niingie deep huku.

Lakini pia kipindi hiko nilikua navutiwa sana na mada za kule jamii intelligent ambako kuna mada nilikuta ipo hot sana ile ""proof binadamu katengenezwa na allien"" pale kuna jamaa anaitwa lifecode huyu jamaa alikua hatarii mnooo

Huku na kule nikawa navutiwa sana na mada za Kiranga the unorthodox kipindi hiko jamaa alikua ajajikita sana kwenye kumkataa Mungu ila alikua mtu wa kuchangia kuhusu science mambo ya physics nikasema lazima nijiunge...

Hao niliowataja ndio walikua main character wa kufanya mimi niwe hapa leo....

Lakini mwaka 2021 nikaanza rasmi kupenda mashangazi hapo nikawavutia mashangazi kama wawili kuanza kufatilia huu mtandao na wale mbwa wakajiunga bila hata kunipa username zao i don't know sijui kwanini walifanya vile....
 
2010 siasa za jf, nikiwa high school kuna madame rafiki yangu saana alikuwa Kila nikienda ofisini namkuta anasoma jf
 
Ilikuwa kila nikitafuta kitu Google kina niletea na option ya jamiiforums!, nikawa naingia nasoma kikichonileta naondoka!.. sasa nilivyoona mbona kila mara Google wananiletea hili li jamiiforums kwani lina nini ndo nikaamua kulifukunyua ndo nikakutana na mada kemkem haswa kule jamii intelligence!. Nikawa nafuatilia kwanza kama anonymous bila kujiunga!.. baadae nikawa naona watu wanauliza vitu na watu wanakomenti nikaanza kupata hamu yakuanza ku komenti nikasema msinitanie Nyie namimi nikazama ndani nikalianzisha sasahivi nimekubuhu nabishana hata na moderator wakati mara yakwanza member tu wa humu nilikuwa nawaogopa!...😂
 
Wakuu,
Kila mmoja wetu humu jukwaani ana stori yake ya kuvutia,kusisimu na kushangaza ya kwa nini alijiunga jf!

Wapo waliovutiwa na stories za mapenzi,siasa,michezo nk.

Kwa upande wangu stori yangu iliyosababisha nikajiunga kujiunga jf ni ndefu ila ya kuvutia,niliwahi kumsimulia mshamba_hachekwi katika uzi flani,atakuja asimulie hapa.

Dondosha chanzo cha wewe kujiunga jf.
Mijadala ndio burudani yangu
 
Startv kipindi cha habari asubuhi, kama sikosei kilikua kinaitwa "Tuongee Asubuhi" katika mada ya siku hiyo kuna muda ukifika lazima wasome maoni ya jf. Ila kujiunga rasmi nikaja kujiunga baadae sana lengo likiwa kusoma nondo mbalimbali
 
ivi inawezekana tv kusoma maoni ya wadau wa jf ya sasa?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom