Nini kilimpata balozi Humpley Polepole?

Nini kilimpata balozi Humpley Polepole?

Salam zikufikie popote ulipo .

Baada ya kumkumbuka Balozi Humpley polepole usingizi umekata ghafla,Kirjana huyu alikua ni mzalendo ,mpenda nchi yake na mtu mwenye kusema ukweli kwa lengo la kuisaidia nchi yake .

Aliteuliwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Malawi badae Cuba wakati yuko Cuba akatangaza kujiuzuru ubalozi kwa sababu aliona nchi yake inabagazwa,kubanangwa ,kutindinganywa bila huruma hata kidogo.

Badae akaanza kutoa mtazamo wake juu ya Tanzania ,akaeza nchi inavyoendeshwa kama haina mwenywe yaani familia ya Kambale kila mtu ndevu ,akaeleza mambo mengi sana ambayo kila mmoja kwakweli aliyemsikiliza alistaajabu sana kwa maana kiongozi wa juu kama yule kutoka hadharani na kusema mambo yale ilikua Inashutua kidogo.

Badae kidogo Balozi ikasemekana ametekwa nyumbani kwake hapa Tanzania ,ikaonekana michirizi ya damu ,Jeshi la Polisi likasema linaendelea na uchunguzi hadi leo jariida lake nahisi linaendelea kuchunguzwa.

Masawali!
Kwanini balozi aliamua kuacha kazi ya ubalozi yenye malipo mazuri tu akaamua kuipambania Tanzania ?

Balozi alikosa njia sahihi yeye kama kiongozi wa juu za kufikisha ujumbe au alipuuzwa?

Kwa yale aliyokua akiyasema ikiwemo tuhuma za kifo cha Magufuli ,Wizi uliokithiri,Uongozi mbaya ,Wanamtandao kuongoza nchi nk hakuona usalama wake utaua hatarini akiyasema akiwa Tanzania?

Je yupo wapi ? Yuko salama mpaka leo siku zote ?

Hayo ni baadhi ya maswali ambayo hadi leo najiuliza bila majibu.
Alichagua kukosoa zimwi aliloshiriki kuliunda, likamtafuna,
Kakosoa utwaala,ukamteka period
 
Alisema anamtumaInia Mungu wa Mbinguni!
Hakutumia maarifa.
Huwezi kupambana na Shetani ukiwa kwenye ngome yake.
 
Inasikitisha sana na bora waendelee kuweka ugumu wa raia kumiliki "MIKWAJU" maana kwa viongozi washenzi wasiosikiliza wananchi dawa yao ni Pyu pyu pyu.

Kwa TZ hakuna ulinzi wa aina yeyote ,ni easy sana kuua hata rais ,usitishike na mitutu ya wale wanaokuwa wanamzunguka prezzo sema ndiyo hivyo waTZ hatujafikia huku ila wipo siku watatufikisha.
 
Alisema anamtumaInia Mungu wa Mbinguni!
Hakutumia maarifa.
Huwezi kupambana na Shetani ukiwa kwenye ngome yake.
Alifanya kosa kubwa sana ,hawa washenzi hauwezi kupambana nao live ukiwa BONGO ,kwa hapa TZ kina BUYOBE wapo wengi sana.
 
Yuko waaaaaaapi Polepole? Yani tumekuwa kama mbuzi kwenye banda, anachukuliwa mmoja mmoja kuchinjwa na hakuna kitu tunaweza kufanya.

Hivi ndio tumeona iwe hivi, hatuna namna nyingine?, hali hii ya KISHETANI, isiyofuata wala kutambua utaratibu halali wa sheria, itaendelea hata lini????!
 
Back
Top Bottom