Nini kilimpata balozi Humpley Polepole?

Nini kilimpata balozi Humpley Polepole?

Best home tutor

Senior Member
Joined
May 8, 2026
Posts
194
Reaction score
264
Salam zikufikie popote ulipo .

Baada ya kumkumbuka Balozi Humpley polepole usingizi umekata ghafla,Kirjana huyu alikua ni mzalendo ,mpenda nchi yake na mtu mwenye kusema ukweli kwa lengo la kuisaidia nchi yake .

Aliteuliwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Malawi badae Cuba wakati yuko Cuba akatangaza kujiuzuru ubalozi kwa sababu aliona nchi yake inabagazwa,kubanangwa ,kutindinganywa bila huruma hata kidogo.

Badae akaanza kutoa mtazamo wake juu ya Tanzania ,akaeza nchi inavyoendeshwa kama haina mwenywe yaani familia ya Kambale kila mtu ndevu ,akaeleza mambo mengi sana ambayo kila mmoja kwakweli aliyemsikiliza alistaajabu sana kwa maana kiongozi wa juu kama yule kutoka hadharani na kusema mambo yale ilikua Inashutua kidogo.

Badae kidogo Balozi ikasemekana ametekwa nyumbani kwake hapa Tanzania ,ikaonekana michirizi ya damu ,Jeshi la Polisi likasema linaendelea na uchunguzi hadi leo jariida lake nahisi linaendelea kuchunguzwa.

Masawali!
Kwanini balozi aliamua kuacha kazi ya ubalozi yenye malipo mazuri tu akaamua kuipambania Tanzania ?

Balozi alikosa njia sahihi yeye kama kiongozi wa juu za kufikisha ujumbe au alipuuzwa?

Kwa yale aliyokua akiyasema ikiwemo tuhuma za kifo cha Magufuli ,Wizi uliokithiri,Uongozi mbaya ,Wanamtandao kuongoza nchi nk hakuona usalama wake utaua hatarini akiyasema akiwa Tanzania?

Je yupo wapi ? Yuko salama mpaka leo siku zote ?

Hayo ni baadhi ya maswali ambayo hadi leo najiuliza bila majibu.
 
Kuna mda unafika unasema kuzaliwa afrika ni laana.Nchi hata kusema kuna maendeleo hakuna
Africa kupata maendeleo ngumu sana kwa sababu ya ubinafsi wa watu wachache nchi kama Korea kila kitu ni our mfano our food ,our culture,our nation ,yaani wao uzalendo mbele nchi yatu,chakula chetu kila kitu ni chetu wamejengewa culture hiyo Ila afirca ni nyumba yangu ,kabila langu ,nchi yangu culture ya changu maana yake ubinafsi kwa hyo utajiri unabaki kwa watu wachache .
 
Korea ya kiduku ambaye anaagiza baga na mvinyo toka ufaransa huku wananchi wanaishi kwa shida.
 
S
Sio Korea hiyo mzee south
Nikwambie kitu kimoja .Utawala ni malezi toka kwenye familia ulipozaliwa.Nchi zenye utawala mzuri ndio zina maendeleo.
Nchi kama china kuwa na sheria kali na utawala mkali sababu ya malezi uwezi kuona wana muhukumu mtu ambaye kaona kosa kwa serikali.Ndio maana wanaonyongwa sana ni viongozi wa serikali na waharifu
 
Ndio culture yenyewe hiyo mkuu sisi hatuna culture hiyo sisi uongozi sio kutumikia watu ni fursa ya kuwa tajiri
 
pamoja na yote aliplay harakati kizembe sana hakupaswa kufanya yale akiwa nchini lazima pia mtu uwe makini na hizi serkali zetu na uzuri ye hakuwa jukwaani alikuwa online haswa angeenda huko ulaya
 
Nakumbuka alisema ukiwa na Nida tuu umepiga kura, iliniuma na kususia kupiga kura kbs sitaki.
Mpaka kura yangu iwe na maamuzi.
Hapo ÿeye na mwendazake walitukosea sana.
 
Alianzisha vita kwa wenye nguvu ila yeye akiwa kwenye uzio wa mabua . Nadhani kuna kundi lilimuaminisha kuwa pamoja naye katika harakati zile ndiyo maana alikuwa anajiamini sana ....Daah alishikwa ki zembe sana . Kwenye uzalendo kijana aliipenda nchi yake Mungu amsaidie huko alipo kama bado anapumua .
 
Yaani mtu kaenda Kwa mungu Bado una amini atakuwa mzima😟😟.
Hyo bahati waliipata nabii issa na nabii Idris peke yao
 
Salam zikufikie popote ulipo .

Baada ya kumkumbuka Balozi Humpley polepole usingizi umekata ghafla,Kirjana huyu alikua ni mzalendo ,mpenda nchi yake na mtu mwenye kusema ukweli kwa lengo la kuisaidia nchi yake .

Aliteuliwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Malawi badae Cuba wakati yuko Cuba akatangaza kujiuzuru ubalozi kwa sababu aliona nchi yake inabagazwa,kubanangwa ,kutindinganywa bila huruma hata kidogo.

Badae akaanza kutoa mtazamo wake juu ya Tanzania ,akaeza nchi inavyoendeshwa kama haina mwenywe yaani familia ya Kambale kila mtu ndevu ,akaeleza mambo mengi sana ambayo kila mmoja kwakweli aliyemsikiliza alistaajabu sana kwa maana kiongozi wa juu kama yule kutoka hadharani na kusema mambo yale ilikua Inashutua kidogo.

Badae kidogo Balozi ikasemekana ametekwa nyumbani kwake hapa Tanzania ,ikaonekana michirizi ya damu ,Jeshi la Polisi likasema linaendelea na uchunguzi hadi leo jariida lake nahisi linaendelea kuchunguzwa.

Masawali!
Kwanini balozi aliamua kuacha kazi ya ubalozi yenye malipo mazuri tu akaamua kuipambania Tanzania ?

Balozi alikosa njia sahihi yeye kama kiongozi wa juu za kufikisha ujumbe au alipuuzwa?

Kwa yale aliyokua akiyasema ikiwemo tuhuma za kifo cha Magufuli ,Wizi uliokithiri,Uongozi mbaya ,Wanamtandao kuongoza nchi nk hakuona usalama wake utaua hatarini akiyasema akiwa Tanzania?

Je yupo wapi ? Yuko salama mpaka leo siku zote ?

Hayo ni baadhi ya maswali ambayo hadi leo najiuliza bila majibu.
Kuna chombo cha habari cha nje walisema alifariki kwa majereha aliyopata wakati wanamkamata. Henda hii ni habari sahihi kwa sababu ni chombo cha kuaminika na walisema walipata habari za ndani. Hata mimi nikiangalia kilichotokea 29/10, watu wasio na hatia kuuawa mpaka watoto, waliojeruhiwa kutolewa wodini wakamalizwe, sioni kama atakuwa salama. Siyo yeye tu, wote waliotekwa sidhani kama kuna aliye salama.
 
pamoja na yote aliplay harakati kizembe sana hakupaswa kufanya yale akiwa nchini lazima pia mtu uwe makini na hizi serkali zetu na uzuri ye hakuwa jukwaani alikuwa online haswa angeenda huko ulaya
Nahisi labda kuna watu walikua nae wanamdanganya watamlinda au wako nae pamoja na yeye akaona watu wale wana nguvu na ushawishi akawaamini maana kwa kauli zake kama alikua nchini ilikua lazima Asakwe maana alikua anaenda mbali.
 
Nakumbuka alisema ukiwa na Nida tuu umepiga kura, iliniuma na kususia kupiga kura kbs sitaki.
Mpaka kura yangu iwe na maamuzi.
Hapo ÿeye na mwendazake walitukosea sana.
Hahaha Alisema nchi hii inabagazwa,kubanangwa na kutindinganywa bila huruma mkawa mnamuita super hero sasa hivi ugumu wa maisha umefanya tushaanza kumsahau tuko busy na mkate
 
Alianzisha vita kwa wenye nguvu ila yeye akiwa kwenye uzio wa mabua . Nadhani kuna kundi lilimuaminisha kuwa pamoja naye katika harakati zile ndiyo maana alikuwa anajiamini sana ....Daah alishikwa ki zembe sana . Kwenye uzalendo kijana aliipenda nchi yake Mungu amsaidie huko alipo kama bado anapumua .
Itakua maana kusema yale nahuko Tanzania tena dar es Salaam inashangaza sana ,harakati kama zile unafanya ukiwa na nje ya nchi na huko nje uwe na uhakika haurudi hivi karibuni maana watu aliokua anawataja wamehold nchi ni watu mapapa kwelikweli .
 
Yaani mtu kaenda Kwa mungu Bado una amini atakuwa mzima😟😟.
Hyo bahati waliipata nabii issa na nabii Idris peke yao
Tusubirie uchunguzi wa Jeshi la Polisi kama wameweza kupata kichwa cha James Temba mwanafunzi wa IFM basi hata huyu ayaptikana tu walau hata kama amekufa watapata mwili watu wakazike ,huyu Kijana angeshukuru ubalozi au aliona anakula kidogo? Mbona wenzie hatuna hata rangi kwenye keki nzima Ila tumerizika tu
 
Kuna chombo cha habari cha nje walisema alifariki kwa majereha aliyopata wakati wanamkamata. Henda hii ni habari sahihi kwa sababu ni chombo cha kuaminika na walisema walipata habari za ndani. Hata mimi nikiangalia kilichotokea 29/10, watu wasio na hatia kuuawa mpaka watoto, waliojeruhiwa kutolewa wodini wakamalizwe, sioni kama atakuwa salama. Siyo yeye tu, wote waliotekwa sidhani kama kuna aliye salama.
Nani huwa anafanya hivo unajua kumuua au kumjeruhi mtu ambaye hauna ugomvi nae hata kama umeagizwa ni ngumu sana nahic kama hawa watu wapo ni watu ambao kazi yao ni ngumu sana maana kuwa involved na mambo kama haya tena pengine hata haujui muhusika kafanyaje ni level ya hali ya juu ya ugumu wa kazi.
 
Hakika ndugu balozi alijitoa mhanga, sijui kama bado yupo chini ya jua hili au yupo ahera madukani.
 
Back
Top Bottom