Ciprofloxacin.
JF-Expert Member
- Apr 15, 2015
- 1,583
- 2,702
Alikuwa ni mtanzania mzalendo na mwenye uchungu na taifa lake,hakutaka kwenda Namibia au Botswana ili kupata mshahara mkubwa,badala yake akaanzisha hosp kurasini ya kutibu magonjwa ya moyo (THI)Tanzania Heart Institute akijua kuwa ingewasaidia watanzania wenzake maana hapakuwa na matibabu hayo Tanzania nzima,enzi zile umri wangu ulikuwa mdogo nikasikia fununu tu kuwa alikuwa anafanyiwa mizengwe sana na watu waliojua kuwa anaenda kufanikiwa kupitia taasisi yake hiyo,baadae alifariki,jamani kwa mnaojua A to Z na mkanda mzima wa Dr Masako,nini hasa kilijiri na ilikuwaje?