Nini kifuate baada ya kuitoa CCM madarakani? Swali hili ni la muhimu sana

SYLLOGIST!

JF-Expert Member
Dec 28, 2007
7,119
6,718
Taarifa huwa haziozi.

Hoja hiyo kwenye mada; Iliibuliwa na siye Mwingine bali Nguli wa Siasa wa CHADEMA.

Unaweza pitia hapa kwa Taarifa
Bila ya Kuharibu shehena.

Hatahivyo nitamnukuu kiunagaubaga.....

Kwa siku kadhaa nilikuwa nimetoweka hapa JF. Kabla ya kutoweka nilishiriki mjadala mrefu kwenye FOCUS 2010 na CHADEMA must reform.
Has Chadema Reformed?
kumezuka hoja ya kuiondoa CCM madarakani- lakini swali la ziada limezuka- kwa ajili gani? Nini kifuate baada ya kuitoa CCM madarakani?

Mjadala huu ni muhimu kwa kuwa naamini kabisa ushirikiano wa vyama kama wa CHADEMA, CUF, TLP na NCCR Mageuzi unapaswa kusikiliza matakwa ya umma kwa kiasi kikubwa. Swali hili ni muhimu kwa kuwa linaweza kutoka na ajenda za msingi za uchaguzi wa mwaka

Mjadala huu ni kwa yoyote ambaye ana Tanzania anayoitaka ambayo anaona bado utawala uliopo haujaweza kuileta.

Imetoka Maktaba.
 
Taarifa huwa haziozi.

Hoja hiyo kwenye mada; Iliibuliwa na siye Mwingine bali Nguli wa Siasa wa CHADEMA.

Unaweza pitia hapa kwa Taarifa
Bila ya Kuharibu shehena.

Hatahivyo nitamnukuu kiunagaubaga.....

Has Chadema Reformed?

Imetoka Maktaba.
Nchi tuirudishe mikononi mwetu wananchi, hizi familia zilizogawana madaraka ili zitajirike tuziweke pembeni kwani hazina nia njema na nchi.
 
Leo ni siku ya huzuni mno msaliti wa taifa Lisu mzee wa MIGA anarudi.

Mwambieni asipande ndege zetu maana alishangilia zilipokamatwa
 
Nchi tuirudishe mikononi mwetu wananchi, hizi familia zilizogawana madaraka ili zitajirike tuziweke pembeni kwani hazina nia njema na nchi.

Kwa aliyoyasema Mh. Tundu Lissu baada ya kuongea Temeke

Sioni kama hilo litakuja kutokea.

Sidhani.
 
Mabadiliko yoyote yale hayajawahi kukubalika Kwa haraka Mkuu. CCM yenyewe imekuwa ikijibadili mara kadhaa Ili kuendana na hali ilivyo.
 
Mi ningekuwa mwanamipango wa ccm tunajirebrand hivi.
Kinaanzishwa chama cha siasa.
.....Kinapewa promo kubwa na wanaccm wanaingia weng.
.....Kinashinda uchaguzi.
......political bussiness as usual.
Kwa sasa tumefikia mahala tatizo sio sera mbovu wala nini bali ni brand ya CCM! Imeshachafuka sana kwa sabab ndo imekuwepo tu.
Ukweli ni kwamba kuna mapungufu ya ccm hata akija wa chama gani yataendelea mana msingi wa maendeleo ni utashi wa mwananchi mmoja mmoja kwanza! Serkali huwa inaweka miundombinu tu.
Pia serkali zetu za kiafrica sio kamili. Kuna wenye dunia ukipiga tambo vibaya ukakanyaga maslahi yao wanakuhujum ndo utajua kama wewe si mkuu wa shule bali monitor wa darasa!
Nchi haijawai kutawaliwa na raia wote, bali kundi la wachache wenye maono. Katika maono kujikuta wmeshiba si ajabu.
Nadhan kwenye kuwa kundi la hao ndo tunaporaruana.
Katika maisha unaamua,..kuwa kwenye wanaokula au wnaoliwa. (The rule of the survival of the fittest)
 
"Hoja ya kuiondoa CCM madarakani", hilo ni lengo moja linalojitosheleza kabisa, hata bila kuwa na malengo mengine ya ziada kwa sasa.

Tabia ya kung'ang'ania kukaa madarakani kwa gharama yoyote iliyojitokeza ndani ya chama hicho ndiyo sababu muhimu ya kuwaondoa, hata ikiwa kwa kutumia nguvu.
 
Nimeandika, Nimefuta.
tokea saa moja asubuhi na haya ndiyo nimepata...

CHADEMA has a lot of Convincing to do!

Huruma zikiisha potea, kwa Mh.Mbowe na Kwa Mh.Tundu Lissu, yaani shauku za kumwona mtu aliepona risasi na aliyotoka Jela zikaishia sijui nini haswa kitaja tokea.
Just saying.
 
Dah!

Inasikitisha, lakini inabidi kukubaliana nawe kwa hayo uliyoandika hapa.

Lakini, kama nilivyoeleza kwenye mistari uliyoi'quote' hapo, kama CHADEMA watakuwa na vinguvu vya kutosha, kabla ya "huruma" za wananchi kwa hao viongozi hazijafifia, wakaweza kuiondoa CCM madarakani, hiyo itakuwa ni kazi ya kusifika zaidi kwao kwa wakati huo.

Baada ya hapo, tutaangalia tena ni wapi tuelekee kama CHADEMA hawakutuonyesha njia tunayotaka kwenda kama taifa.

Kwa sasa hivi kazi ni moja tu, kuwaondoa CCM. Haijalishi nani ataiweza kazi hiyo. Awe CUF, ACT, au mzee Rungwe, wote ni sawa tu.
 
Back
Top Bottom