Ni kipi kianze kati ya Katiba Mpya au Kuitoa CCM Madarakani?

RNA

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
1,584
2,683
Habari wana JF

Nimewaza sana nikagundua CCM kuwepo madarakani ni tatizo kubwa kuliko hata hii katika tunayo hitaji. Hivi kwa hii CCM tunaweza pata Tume huru ya Uchaguzi?

Sasa tunayo katiba lakini tumeshuhudia mara kadhaa ikivunjwa na Kwa mizizi kiliyo nayo hiki Chama mnadhani ni rahisi Katiba ikafuatwa?

Mi nadhani CCM ni Tatizo katika hii Nchi zaidi ya Katiba.

Elimu, Elimu na Uzalendo ndio nguzo pekee za kuikomboa hii Nchi kutoka Mikononi mwa hiki.

Elimu inahitajika sana, watu wengi wanaishi maisha magumu ila hawajui ni kwa namna gani Serikali inaweza saidia maisha yao kuwa bora hivyo hawaoni haja ya Mabadiliko.

Uzalendo ni kitu kikubwa sana watu wengi hawana uzalendo wako radhi washinde mitandaoni au majukwaani kusifia serikali hata ambapo haistahili. Hakuna kitu kibaya kama machawa.

Kama tukikataa CCM kwa umoja wetu, akili zetu na nguvu zetu hakika itatoka Madarakani na Katiba Mpya itafuatu.

Haihitaji Kuingia barabarani na kuhatarisha Amani ili kuitoa ila kama kila mtanzania kwa akili na uzalendo wake atamua kuitoa itatoka.

CCM husafirisha watu kuja mikutanoni na mambo mengine ili ku-justify kitacho kwenda kutokea. Watu wakiwa na elimu hawawezi kutumika kama sehemu ya mchezo, watujua ni mkusanyiko upi wa kwenda na kutokwenda.
 
Tunawaza kuitoa CCM kisha tukiweke chama gani madarakani?

Chama gani kipo imara kimisimamo, kiitikadi, demokrasia ya kweli na Ilani yake ina tija ktk maendeleo ya taifa letu!?
 
IKvCW.png
 
CCM bado inao mtaji mkubwa mnooo wa wananchi kwa upande wa bara na ndio maana kuna baadhi ya majimbo ubunge ccm unachukua bila ya figisu zozote ila kwa upande wa znz CCM hawana mtaji wa wananchi wa kuweza kupitisha ata diwan na ccm itaendelea kukaa madarakan kwa upande wa bara kwaa mda mrefu sana.
 
Ni ile Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba pekee ndiyo ina uwezo wa kuitikisa CCM, na hata kuitoa kabisa madarakani kupitia nguvu ya umma.

Ndiyo maana hakuna Mwana CCM anaye itamani ile Rasimu. Maana wanajua kile ni kitanzi chao cha kujinyongea.
 
Mimi sina shida na CCM kuwatoa madarakani je chama kitaingia ambacho kina kwaajili ya kusimamia maslahi ya wananchi, kina demokrasia nzuri, chenye viongozi wenye vision na pia chenye viongozi wenye maadili.
 
Back
Top Bottom