Nini kifanyike??!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini kifanyike??!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Eiyer, Dec 27, 2011.

 1. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Thread ya Lizzy(Zawadi ya ngono) imeongeza sintofaham kwenye ubongo wangu,hasa michango ya waliochangia.Nilikua najiuliza maswali mengi sana.Hivi tutaweza kurudisha nidham kwenye mahusiano kama haponyuma?Siku hizi watu wanabakana hovyo(watoto na mateenage wa kike na kiume ndo wahanga wakubwa)ubinadamu umeisha?Zamani ndoa zilikua zinafungwa wahusika walikua hawajagusana(sex)tena wengine walikua hawajuani yaani walikua hawajaonana!Unaijua sura ya mkeo/mumeo siku ya harusi,na ndoa inadumu miaka zaidi ya 70!

  Leo vijana wa kike na kiume wanapeana miili tena wengine kwa shukrani baada ya kusaidiana hesabu darasani!Ukikataa kushiriki tendo la ndoa unaonekana mshamba na hujui ladha ya maisha.Bikra ilikua na thamani hapo kabla leo binti akiwa nayo anaonekana mshamba,vijana wa kiume nao wanataka kuolewa,wanakimbizana mitaani na mabinti wakigombea wanaume.

  Nidhamu ya kale aliyokua anapewa mama imefutika mithili ya mshumaa kwenye moto,sijui sababu ni yeye mama kukataa kumlea mwanae na kwenda kutafuta vibarua baada ya mumewe kutokuacha hela ya matumizi na kuipeleka baa!Heshima ya baba haipo,sijui ameipoteza mwenyewe kwa kufanya mambo ya kijinga kama ulevi,kutelekeza familia na kwenda kula nyama choma na kina dada poa?Yaani ni vurugu.Jamani tufanye nini?Tutaweza kuurudisha utu wa kale unaoisha leo?Nilipokua nasoma wachangiaji wa thread ya Lizzy(Zawadi ya ngono),baadhi waliunga mkono rushwa ya ngono,very SAD!Kali zaidi ni kwenye thread ya Kaunga(aliyemfumania mumewe akimbaka HG)wapo waliomtetea mbakaji,inakera sana.Tumefika hapa.Tuifanye nini jamii yetu?
   
 2. Heart

  Heart JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2011
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 2,660
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Mi nadhani kila kitu kinategemea nidhamu binafsi ya mhusika mwenyewe...Couple ikishindwa kujua nini wanataka kwenye mahusiano yao then hamna kitu kitaendelea. Mambo ya kufanya mapenzi kabla ya ndoa ni makubaliano tu,wanaweza wakakubaliana wasifanye though ni very rare case...so hata kile anachochangia mtu humu JF juwa ana mantiki yake,pengine yamemfika ya kumfika!!....#ila ndo kuna wengine wanapenda kuchangamsha baraza.
   
 3. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Mh!HEART sidhan kama nimekuelewa,hebu dadavua!
   
 4. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #4
  Dec 27, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  kizazi hiki headache sijui maharibiko yanaanzia nyumbani au peer group!!!!!!! si kazi rahisi kurudisha heshima..........
   
 5. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #5
  Dec 27, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  So tuendelee tu!Kwa mtindo huu sidhani kama tutafika!
   
 6. Heart

  Heart JF-Expert Member

  #6
  Dec 27, 2011
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 2,660
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Nidhamu binafsi kwa wanandoa au wachumba nikuheshimiana,na kutekelezeana yale ya msingi...vitu kama kuanza kufanya mapenzi kabla ya ndoa imezoeleka tu sasahiv kama formula but sio lazima hao couples wanaweza kuamua wasifanye until marriage..though ni mara chache kusikia kesi kama hizo.
  Mambo ya Utandawazi yamebadilisha mamabo mengi especially katika jamii zetu za kiafrika...ndo maana kitu kama kutoa zawadi ya ngono au kuomba rushwa ya ngono ni kawaida saanaaa..coz watu si wanaona movies au porn sites..
  So..hata kile mtu anachangia whether ana-support rushwa ya ngono or otherwise then ana maana yake...pengine yamemfika binafsi au ameona kutokana na mazingira aliyoishi...
   
 7. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #7
  Dec 27, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  tutafika ila kwa mbinde..........

  kizazi hiki ambacho watoto wanalelewa na housegirl?
  kizazi hiki chenye utandawazi?
  kizazi hiki chenye boarding school kuanzia darasa la kwanza?
  kizazi hiki ambacho wanadai mtoto wa mwenzio mkubwa mwenzio?
  kizazi hiki cha walimu wasiokuwa na haiba na uadilifu?

  kazi yake kubwa haswa

  zamani ilikua hata ukipita barabarani mtoto akikosea unaweza kumuadhibu, hivyo nidhamu kila mahali... siku hizi mseme mtoto wa mtu uone....
   
 8. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #8
  Dec 27, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  HEART,sasa nimekuelewa(kama nimekuelewa sawasawa)naweza kuwa sina tabu sana na kufanya ngono kabla ya ndoa coz kila mtu ana tafsiri yake ya ndoa,shida ni sababu ya kufanya hiyo ngono.Mtu anapochangia anawakilisha kile anachofikiri kama ni cha kijinga ni hatari kawa jamii inayomzunguka,ndo hayo ya kubaka yanatokea,kumbuka mtu anaanza kufikiri halafu kinafuata kitendo!So mtu anaposapoti hatari nafikiri unajua matokeo!
   
 9. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #9
  Dec 27, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  BADILI TABIA umeongea mambo ya msingi sana,najiuliza kawa Yesu alikiita kizazi cha enzi yake kizazi cha nyoka,leo hiki chetu sijui angekiita kizazi cha nini!Itafika mahali safari ya kizazi hiki itazimika kama umeme wa Ngeleja unavyozimika!
   
 10. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #10
  Dec 27, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  BADILI TABIA umeongea mambo ya msingi sana,najiuliza kama Yesu alikiita kizazi cha enzi yake kizazi cha nyoka,leo hiki chetu sijui angekiita kizazi cha nini!Itafika mahali safari ya kizazi hiki itazimika kama umeme wa Ngeleja unavyozimika!
   
 11. Kbd

  Kbd JF-Expert Member

  #11
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 9, 2009
  Messages: 1,264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Kila kitu kinawezekana kama tukiamua na kusimamia maamuzi yetu. Tunaweza kuamua kuwa chachu ya mabadiliko na tukaweza kushawishi na wengine. Mmomonyoko wa maadili umefika mahali hata siwezi kufikiria miaka 5 baadae itakuwaje. Zaidi sana juhudi binafsi zinahitaji kuweza kufikia lengo. Tusiache kumuomba Mungu kuhusu kizazi chetu.
   
 12. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #12
  Dec 27, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  cha kwanza kufanyika
  ni kuanza kufundisha hayo nyumbani kwako
  pandikiza mbegu ya mazuri unayayoyaamini kwa familia yako na hasa watoto wako.

  Kila mtu akifanya hivyo kwa nafasi yake, dunia itakuwa mahali pazuri zaidi pa kuishi
   
 13. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #13
  Dec 27, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Ok,tunaweza,tuanzie wapi ndugu yangu?
   
 14. Heart

  Heart JF-Expert Member

  #14
  Dec 27, 2011
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 2,660
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Ni kweli ulichosema...Ukiangalia sasahiv jamii nzima kwa sasa,inauelewa mkubwa kuhusu janga la UKIMWI kama semina zishatolewa sana lakini bado watu wanaendekeza ngono zembe..kwa mfano hapo nani alaumiwe..? Mtu anajua kabisa nikibaka ntapata kifungo cha miaka kadhaa jela lakini bado anafikiria kubaka..tena wengne wanabaka watoto under 5years... hiyo mifano midogo tu,lakini utasema jamii haina uelewa wa consequences za hayo mambo..
   
 15. BORNCV

  BORNCV JF-Expert Member

  #15
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ipo haja kwa watumishi wa Mungu kulivalia njuga suala hili maana haya yamesabishwa na utandawazi/umagharibi kwenye jamii zetu. Lakini tukianzia kwenye ngazi ya familia, mimi, wewe na yule tusimame katika malezi bora ya watoto na ndugu zetu.
   
 16. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #16
  Dec 27, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Yes,HEART uko sahihi,but hao wanayotenda hayo tuwasaidieje?Mtu anapoelimishwa hatari ya kubaka halafu anabaka lazima kutakua na tatizo mahali,ukimwi umeshindwa kuwafanya watu waache ngono zembe,jela zimeshindwa kuzuia watu wasibake,sasa tufanye nini,kama tulivyoweza kugundua jela kwanini tusitafute suluhu nyingine kama hii imekua useless?
   
 17. Kbd

  Kbd JF-Expert Member

  #17
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 9, 2009
  Messages: 1,264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133

  Twaweza kuanzia kwetu na ikafuata kwa watoto wetu. Hebu msome kongosho hapo juu, inahusu pia.
   
 18. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #18
  Dec 27, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Yes nimekupata,is it easy as it sound?
   
Loading...