NINI KIFANYIKE?

Quinine Mwitu

JF-Expert Member
Oct 19, 2014
5,528
6,085
Salam Wanajamvi,
Hivi hii kamata kamata ya pikipiki ina tija gani kwa serikali?
Nina jamaa yangu huwa ni dreva bodaboda na huwa anaegesha pikipiki yake macho,na pia anafanya shughuli za ulinzi,sasa juzi nikiwa kazini mchana akanipigia simu kuwa amekamatwa na piki piki,nikashindwa kwenda kumuona kwa sababu muda ulikuwa umekwenda,Na siku kadhaa nyuma aliniambia kuwa alikamatwa pia akiwa coco beach ila akawa amemalizana na jamaa baada ya kumleta hadi hapo macho na gari yao kwa kuwa alikuwa hana kitu mfukoni so akaja kuwaona washkaji wamsaidie amalizane nao
Kwa hyo nikajua ni ishu zile zile za kila siku sikujua atakaa sana,sasa jana pia nikapigiwa simu kuwa jamaa bado yupo ndani na hajatoka so inatakiwa ipelekwe kadi ya pikipik ili iangaliwe na aweze kutoka,
Sasa mi naomba kuuliza,hii operation lengo lake ni nini?
Kama suala ni kuwa pikipiki zinatumika.na waharifu....na zinazokamatwa sana ni boxer,kama ndio zenye madhara kwa nini serikali isipige marufuku importers wa hizo pikipiki wasiziingize nchini? kwa sababu kuwaachia importers alafu ukaja kuwasumbua raia wa kawaida mi naona kama ni unafiki,
Na jee serikali imeshindwa kabisa kutafuta suluhisho la kudumu ili iwaachie vijana wavuja jasho waendelee na maisha yao bila kubugudhiwa? ikumbukwe hawa vijana wengi mwanzo ndio walikuwa ni wezi mtaani nk,na kwa suala hili waliofikwa na madhira mbali mbali kama kufungwa,kuumia wakiwa wanakimbizana na polisi,
Nini kifanyike wadau?
Karibuni.
 
Back
Top Bottom