Nini kifanyike kuondoa tatizo hili?

Sima70

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
427
317
Wakat nasoma chuo kikuu kimojawapo hapa nchini niligundua kuwa wengi wa wahitimu hupata GPA kali (za madesa) bila kuwa na utalaam wa kiwango husika kivitendo kama ambavyo wengi wao wamekuwa "waki-underperform" pindi wanapopewa nafasi kama wataalam

Kitendo hiki hunifanya mimi niwaze mambo mengi sana kuhusu mfumo wetu wa elimu

Kufuatia mfumo huu, mimi binafsi huwa najiuliza hivi hatuwezi kubadilisha huu mfumo na kuufanya kivitendo zaidi?

Kwa mfano, inasikitisha msomi wa chuo kikuu tena anaesomea IT anashindwa kudesign hata program moja tu ya kompyuta

Hii inamanisha kuwa tuna wasomi wengi lakin hatuna wataalam kama tunavyofikiria na kwa maana hiyo nchini yetu itaendelea kujivuta katika suala zima la maendeleo kwa kukosa wataalam

Je, nini kifanyike ili kuondoa tatizo hili?

Naomba kuwasilisha
 
Yaani hasa hawa ITs ni full mzigo. Hapa kazini kwetu Virus wankula Laptop za ofc wapo tu, Internet ya wireless tatizo huku org inalipa hela za kutosha, Wanaomba mfanyakazi asipeleke computer kwa ajili ya mainteinance, Websibe mbovu kama nn!!, complaints from clients/customers too much!! Yaani ni zaidi ya majanga.

Engineer anasoma hata tape, wala drawings, etc humuoni nazo. Wala kumwona anapima ukuta hamna!! Yaani wao Mapenzi, pombe, Libarary, madftari,na darasa tu.
 
Back
Top Bottom