Nini kifanyike kuisambaratisha CCM?

Nini kifanyike kuisambaratisha CCM?

Tatizo wapinzani wakipata uongozi wanahongeka kirahisi kana kwamba wapo uwanja wa fisi.

Wangekuwa wasimamizi wa serikali wangehongwa na wazungu na kuuza nchi yote.
 
Kwa ufahamu wangu nimejiridhisha kwamba CCM ndiyo wanahusika wa anguko la jamii yetu watanzania. Kama kuna wizi na ufisadi chanzo ni wao, ukiona ubaguzi wa kikabila, kidini, kikanda,kivyama au kijinsia basi jua hao ni CCM.

Ukiona mfumo wa elimu unavurugwa, uchumi unaendeshwa shaghalabaghala, watumishi wa umma hawalipwi ipasavyo na haki zao zinavunjwa tena kwa vitisho jua chama ni CCM. Ukisikia watu vigeu geu kwenye kauli na matendo yao kwenye medani ya siasa jua ni CCM.

Ukisikia mwanasiasa kauawa kwenye siasa hawezi kuwa wa CCM ila alilkuwa anaipinga CCM. CCM ndiyo wanatamani vyombo vyetu vya dola viwe kama mwanasesere wa chama chao. Kwenye CCM Rushwa na upendeleo vimetamalaki.

Kila hasara ambayo tunaingia na kila mpango wa hovyo tunaufanya na kushindwa kiini kiko CCM. Mkurabita, BRN, na kila ujinga unaoangamiza taifa hili, mzimu wake uko CCM. Ni CCM ndiyo mchawi wa maendeleo ya taifa letu.

Ndani ya CCM hakuna anayewaza mema kwa ajili ya watanzania wote ila CCM huwatumia watanzania kwa maslahi yao binafsi na ya chama chao. Ukisia CCM unasema "maslahi ya Umma" ujue wanamaanisha maslahi ya chama chao.

CCM wanaposema "wananchi" jua wanamaanisha wale tu wanaokiunga mkono chama hicho. Kila siku CCM hutamani wawe wenyewe tu kwenye ulingo wa siasa za Tanzania, na bila shaka wanamlaani sana Mwalimu Nyerere kwa kukushinikiza kwake kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi.

Lakini kama wazalendo wa nchi yetu, ni nini kifanyike kukisambaratisha chama hiki ili nchi yetu ya Tanzania ibaki salama?
Dawa yao ni kueñdelea kuwarekodi tu
 
Hili wazo ni zuri sana, ingawa hata mijini bado wamejaa watu wanaoamini neema itakuja baada ya mwaka 2025, Kwa ivo wanaendelea kuivumilia CCM na kuisapoti!
Mujini kunaongoza kwa kuikataa ccm.
Tupande mbegu bora vijijini, tuzinyweshee maji (tupeleke ushawishi kwa ndugu zetu) somo likieleweka na kutekelezeka "shoka moja mmbuyu chini"
 
Wangekuwa wasimamizi wa serikali wangehongwa na wazungu na kuuza nchi yote.
Hii serikali haijawahi kuongozwa na CHADEMA na kila siku tunasikia viongozi wetu wakituhumiwa kuhongwa. Aliyejichukulia bilioni moja ya ununuzi wa Radar alikuwa ni CHADEMA ama CCM?

Kila ripoti ya nchi hii kuhusu ufisadi ni wana CCM peke yao wanaotajwa, Ule mkataba wa Buzwagi uliosaini Hotelini London nani alihongwa? Lile pande la dhahabu aliyepewe alikuwa ni CHADEMA na waliompa si wazungu ambao leo mnawaita wezi?
 
Ujinga wa walio wengi katika nchi hii ndiyo mtaji namba moja wa chama cha makinikia. Kwa bahati mbaya sana, kwa maoni yangu, mfumo wa elimu uliopo siyo wa kumuondoa mtu ujinga bali wa kumfanya mtu aendele kuyakabili mazingira ili aendelee kusavaivu. Ni wachache sana wanaoondoa ujinga kwa kuelemika ndiyo maana hata 'mtukufu' ba' bashite anasema vyeti si ishu kivile cha msingi tufanye kazi.

Yaani ukiona siku zote mwenyekiti wa chama cha makinikia anatoa hotuba ile ile ya kabla na baada ya uchaguzi na kushangiliwa na maprof hata anapomwaga upupu au uharo, ujue elimu haikusaidia sana kuondoa ujinga. Labda elimu imepunguza ujinga kidogo tu.

Sasa basi, sisiem haiondoki kama ujinga usipoondoshwa. Na kama wa kusaidia kuondoa ujinga huu ni yule yule anaetegemea ujinga kwa walio wengi ili kuendelea kusavaivu basi inabidi wajinga wawe vichaa fulani wafanye kituko kitakachoiondoa sisiem na serikali once and for all.

Kituko gani kifanywe na wajinga walio wengi? Huo ni ubashiri wa yeyote!
 
Hii serikali haijawahi kuongozwa na CHADEMA na kila siku tunasikia viongozi wetu wakituhumiwa kuhongwa. Aliyejichukulia bilioni moja ya ununuzi wa Radar alikuwa ni CHADEMA ama CCM?

Kila ripoti ya nchi hii kuhusu ufisadi ni wana CCM peke yao wanaotajwa, Ule mkataba wa Buzwagi uliosaini Hotelini London nani alihongwa? Lile pande la dhahabu aliyepewe alikuwa ni CHADEMA na waliompa si wazungu ambao leo mnawaita wezi?
Mimi bado nipo kwenye issue ya wadiwani waliohongwa.Je kama wangekuwa serikalini wasingehongeka?
 
Hoja yangu ni kwamba hao wahongaji walikuwa ni wazungu ama ni CCM wenzenu? Yaani mhongaji anawezekanaje kuonekana yuko sahihi dhidi ya mhongwaji?

Hao madiwani ni watanzania ambao wanaamini kwamba CCM inawezeka kujenga ama kubomoa maisha ya mtu. Unakumbuka yule kiongozi aliyehongwa suti, si alikuwa CCM tena kiongozi mkubwa tu!
 
Kwa ufahamu wangu nimejiridhisha kwamba CCM ndiyo wanahusika wa anguko la jamii yetu watanzania. Kama kuna wizi na ufisadi chanzo ni wao, ukiona ubaguzi wa kikabila, kidini, kikanda,kivyama au kijinsia basi jua hao ni CCM.

Ukiona mfumo wa elimu unavurugwa, uchumi unaendeshwa shaghalabaghala, watumishi wa umma hawalipwi ipasavyo na haki zao zinavunjwa tena kwa vitisho jua chama ni CCM. Ukisikia watu vigeu geu kwenye kauli na matendo yao kwenye medani ya siasa jua ni CCM.

Ukisikia mwanasiasa kauawa kwenye siasa hawezi kuwa wa CCM ila alilkuwa anaipinga CCM. CCM ndiyo wanatamani vyombo vyetu vya dola viwe kama mwanasesere wa chama chao. Kwenye CCM Rushwa na upendeleo vimetamalaki.

Kila hasara ambayo tunaingia na kila mpango wa hovyo tunaufanya na kushindwa kiini kiko CCM. Mkurabita, BRN, na kila ujinga unaoangamiza taifa hili, mzimu wake uko CCM. Ni CCM ndiyo mchawi wa maendeleo ya taifa letu.

Ndani ya CCM hakuna anayewaza mema kwa ajili ya watanzania wote ila CCM huwatumia watanzania kwa maslahi yao binafsi na ya chama chao. Ukisia CCM unasema "maslahi ya Umma" ujue wanamaanisha maslahi ya chama chao.

CCM wanaposema "wananchi" jua wanamaanisha wale tu wanaokiunga mkono chama hicho. Kila siku CCM hutamani wawe wenyewe tu kwenye ulingo wa siasa za Tanzania, na bila shaka wanamlaani sana Mwalimu Nyerere kwa kukushinikiza kwake kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi.

Lakini kama wazalendo wa nchi yetu, ni nini kifanyike kukisambaratisha chama hiki ili nchi yetu ya Tanzania ibaki salama?
CCM haiwezi kusambaratishwa na watu walioko nje yake.
 
Idadi kubwa ya wabunge wa upinzani ndio njia pekee watakuwa na uwezo wa kupata spika wa bunge na hatimaye katiba itabadilishwa itaruhusu chama chochote kuingia ikulu kwa sasa haiwezekani
 
Tuhamasishane kumpigia makofi baba Jesca, tushirikiane kumwambia mwendo wake ni sahihi, tuzidi kumwambia ayafanyayo ni sahihi, tujiunge kumpa support ya kutosha yaani apite kwenye mstari huu huu anaopita sasa mpaka ifike 2020, hapo hatutatumia nguvu tena kuiondoa iwapo atagombea tena 2020.
 
Kwa ufahamu wangu nimejiridhisha kwamba CCM ndiyo wanahusika wa anguko la jamii yetu watanzania. Kama kuna wizi na ufisadi chanzo ni wao, ukiona ubaguzi wa kikabila, kidini, kikanda,kivyama au kijinsia basi jua hao ni CCM.

Ukiona mfumo wa elimu unavurugwa, uchumi unaendeshwa shaghalabaghala, watumishi wa umma hawalipwi ipasavyo na haki zao zinavunjwa tena kwa vitisho jua chama ni CCM. Ukisikia watu vigeu geu kwenye kauli na matendo yao kwenye medani ya siasa jua ni CCM.

Ukisikia mwanasiasa kauawa kwenye siasa hawezi kuwa wa CCM ila alilkuwa anaipinga CCM. CCM ndiyo wanatamani vyombo vyetu vya dola viwe kama mwanasesere wa chama chao. Kwenye CCM Rushwa na upendeleo vimetamalaki.

Kila hasara ambayo tunaingia na kila mpango wa hovyo tunaufanya na kushindwa kiini kiko CCM. Mkurabita, BRN, na kila ujinga unaoangamiza taifa hili, mzimu wake uko CCM. Ni CCM ndiyo mchawi wa maendeleo ya taifa letu.

Ndani ya CCM hakuna anayewaza mema kwa ajili ya watanzania wote ila CCM huwatumia watanzania kwa maslahi yao binafsi na ya chama chao. Ukisia CCM unasema "maslahi ya Umma" ujue wanamaanisha maslahi ya chama chao.

CCM wanaposema "wananchi" jua wanamaanisha wale tu wanaokiunga mkono chama hicho. Kila siku CCM hutamani wawe wenyewe tu kwenye ulingo wa siasa za Tanzania, na bila shaka wanamlaani sana Mwalimu Nyerere kwa kukushinikiza kwake kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi.

Lakini kama wazalendo wa nchi yetu, ni nini kifanyike kukisambaratisha chama hiki ili nchi yetu ya Tanzania ibaki salama?
Hama nchi, ccm uliikuta inatawala na utaiacha inatawala
 
Iwepo Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi
Kwa hatua hizo ccm tuna wamaliza mapema sanaaaa

Ova
 
Back
Top Bottom