Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,944
- 51,080
Kwa ufahamu wangu nimejiridhisha kwamba CCM ndiyo wanahusika wa anguko la jamii yetu watanzania. Kama kuna wizi na ufisadi chanzo ni wao, ukiona ubaguzi wa kikabila, kidini, kikanda,kivyama au kijinsia basi jua hao ni CCM.
Ukiona mfumo wa elimu unavurugwa, uchumi unaendeshwa shaghalabaghala, watumishi wa umma hawalipwi ipasavyo na haki zao zinavunjwa tena kwa vitisho jua chama ni CCM. Ukisikia watu vigeu geu kwenye kauli na matendo yao kwenye medani ya siasa jua ni CCM.
Ukisikia mwanasiasa kauawa kwenye siasa hawezi kuwa wa CCM ila alilkuwa anaipinga CCM. CCM ndiyo wanatamani vyombo vyetu vya dola viwe kama mwanasesere wa chama chao. Kwenye CCM Rushwa na upendeleo vimetamalaki.
Kila hasara ambayo tunaingia na kila mpango wa hovyo tunaufanya na kushindwa kiini kiko CCM. Mkurabita, BRN, na kila ujinga unaoangamiza taifa hili, mzimu wake uko CCM. Ni CCM ndiyo mchawi wa maendeleo ya taifa letu.
Ndani ya CCM hakuna anayewaza mema kwa ajili ya watanzania wote ila CCM huwatumia watanzania kwa maslahi yao binafsi na ya chama chao. Ukisia CCM unasema "maslahi ya Umma" ujue wanamaanisha maslahi ya chama chao.
CCM wanaposema "wananchi" jua wanamaanisha wale tu wanaokiunga mkono chama hicho. Kila siku CCM hutamani wawe wenyewe tu kwenye ulingo wa siasa za Tanzania, na bila shaka wanamlaani sana Mwalimu Nyerere kwa kukushinikiza kwake kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi.
Lakini kama wazalendo wa nchi yetu, ni nini kifanyike kukisambaratisha chama hiki ili nchi yetu ya Tanzania ibaki salama?