Jamani wajasiriamali wenzangu leo nimeona tujadili hili; Tanzania tuna rasilimali nyingi tu lakini tatizo bado tunaagiza vitu nje hata ambavyo tunazalisha hapa mfano nianzie na wakulima supermarket na hoteli nyingi kubwa unakuta vitu kama nyama, maziwa, mayai, nafaka kama mchele wanaagiza nje. Niliwahi kuuliza hili nikaambiwa watanzania hatuwezi kufanya biashara nao kwani tukiambiwa tenda ya kuku 1000 wenye kg 1.3+ kwa siku tunashindwa mara leo wakubwa sana keshokutwa wadogo, kesho kuku 800 au huna kabisa. Wanasema vivyo kwa nafaka mchele mzuri ila mchafu, packing nk.
Mbaya zaidi hata kwa matumizi ya maduka na manyumbani bado kuna vitu toka nje ambavyo mtu wa Tanzania angeweza kabisa kuzalisha au anazalisha isipokuwa tu packing. Jamani hebu tusaidiane hapa nadhani sio lazima mtu mmoja azalishe kuku 1000 kwa siku, lita 1000 za maziwa au kg 1000 za mchele isipokuwa hakuna network kati ya hawa wafanyabiashara, Naweza kutoa mfano wa nchi jirani Kenya wananunua maziwa yetu fresh wanachanganya na wanayozalisha wao wanafanya packing nzuri wanaleta kuuza Tanzania, wananunua handicrafts kama vinyago, sandals na pochi, vikapu wanaviboresha na kwenda kuuza Ulaya kwa bei juu.
je nini kifanyike ili soko la bidhaa Tanzania likue sio hapa bali nje pia. Kwa walio nje hebu tunaomba tofauti kati ya bidhaa zetu na hizo za wenzetu zikoje mbona kila leo vitu vya nje tu sie tunashindwa wapi? Je bidhaa gani ambayo hapa nyumbani tunaweza kuiza nje hata kwa hawa jirani zetu wa East Africa?