Nini kifanyike ili kuiokoa CHADEMA?

Kwahiyo Mpinzani ni lowassa na sumaye ...... Hahahah. Hizi akili za kushikiwa hatari sana.
 
Mafuriko ya watia nia CCM Ni ushahidi tosha kuwa CCM imezidi kuimarika. Hizo ni salamu kwa upinzani. Tatizo wengi wenu hamjui kusoma alama za nyakati.. Hivi vyama ambavyo havina hata ofisi za mikoa unategemea vitakuwa na ushawishi gani kwa wananchi? Tusijidanganye, mwaka huu jahazi la upinzani linazama.
 
Hivi hawa mataga ndo tuseme wamepigwa li mbwata[emoji23][emoji23][emoji23] eti wananchi wana imani na chama kuliko sasa how? Pint zenu ni zilezile ila main point ndege[emoji23][emoji23]
 
Katiba inasema mgombea mwenza atokee zanzibar
 
Umeanza vizuri umemaliza na utopolo
 
Kuimarika kwa CCM ni kwa mabavu ya vyombo vya dola, lakini kama chama siasa CCM imeshakufa bado kuizika rasmi, na aliyeiua ndiyo huyu inamfia mikononi. CCM itapata pigo kuuuuubwa sana pigo moja tu pigo takatifu pigo lililonyooka kabla ya uchaguzi mkuu ujao.
 
ACT waungane na CDM mgombea awe lisu na mgombea mwenza awe Membe,waachiane majimbo pale chama kinapokubalika, Zanzibar na kusini waachiwe ACT bara yote waachiwe CDM.
Labda mmoja wapo aamue kuwa mzanzibari ! Wabara wote hawakidhi takwa la mgombea,na mgombea mwenza!
 
Vyombo vya dola ndo vilikua vinawalazimisha wananchi waipende CCM? Utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM ndo umeifanya CCM iimarike. Mathalani, ujenzi reli ya SGR, Flyovers, Vituo vya Afya na Zahanati, Elimumsingi bila Ada, kupeleka umeme kila kijiji, kudhibiti vitendo vya rushwa na ufisadi n.k. haya yote ndo yamerudisha imani ya wananchi kwa CCM.

Dalili ya chama cha siasa kinachojifia ni pamoja na kukimbiwa na idadi kubwa ya viongozi na wanachama wake, kupoteza imani kwa wananchi na kukosa ajenda na itikadi inayoisimamia. Kuna Vyama tayari vina sifa hizi, sasa nashangaa mnavyosema CCM inakufa sijui mnatumia vigezo vipi? Au mnafanya utani?
 

Miaka mitano ya Magufuli CCM imetoka kuwa chama cha siasa na kuwa polisi,JWTZ,Magereza,usalam wa taifa. Vyama vyote vilimefungwa kamba na kubaki CCM ikipiga propaganda za uongo. Vyombo vya habari vyote vimelazimishwa kuitakuza na kuisifia CCM na Mwenyekiti wake. Hill Joka la Kijanidhohofika kabisa.

Subirini kampeni zianze ndiyo mutajua lichama lenu limekufa otherwise muendeleze siasa za ubabe,ukatili na uonevu hiyo ndiyo salaam yenu kutumia vyombo vya Dola na Tume ya uchaguzi.

Magufuli isipomfia CCM mwaka huu 2020 basi itamfia 2025 pale utakapotaka kutumia ubabe,ukatili na utesaji ili kurekebisha hali ya hewa ndani ya CCM.

Mwaka tusubiri post kura za maoni hali itakuwaje,huu utitiri wa watia nia unaweza kuwamaliza mkashangaa.
 
Umekosea, ACT ni Kama CUF tu siasa zao za udini.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app

Mgombea Uraisi wa ACT ni Mkotoliki mseminari(From Namupa Seminary, unaijua hiyo?)

ACT ni hybrid ya CHADEMA, CUF na CCM.

ACT ni Social Democratic while CHADEMA ni liberal capitalism ,hawa ni Democratic na Republican wa Tanzania. Baada ya CCM kujifia hawa ndiyo watakuwa wanapokezana miaka kumi kumi kuongoza nchi hii,hatutaki tens kuwa na chama dola ndani ya nchii. Watoto wetu wasiishi chini ya utawala wa chama dola ni upumbavu wa kijima.
 
Ha ha haa.. badala ya kuongelea hoja mnaleta vioja.
 
Ha ha haa.. badala ya kuongelea hoja mnaleta vioja.

Najua kwa utopolo wa akili zako hoja ni kumsifia,kumtukuza na kumuabudu Magufuli na lichama lenu chakavu,Joka la Kijani lenye majeraha ya 2015.
Mwaka huu tuantia chumvi,pilipili na ndimu kwenye majeraha ya 2015

Pole sana MATAGA.
 
Hivi unatumi Nini kufikiri? Akili zingine zinakatisha tamaa kabisa hata kuzitekeleza! Eti siyo hisani...kina membe walipokuwa madarakani walishindwaje kuyafanya aliyoweza Magufuli? Mijitu mwingine inachosha mmfyuuuuu!
Kipindi Membe yuko madarakani, Magufuli hakuwa madarakani?. Au Membe alikuwa na madaraka yapi ambayo Magufuli hakuwa nayo mkuu?.Mimi nafaham wote walikuwa manaibu waziri,wakawa mawaziri na wakitumikia serikali moja.Baada ya hapo JP akawa raisi BM hakuwa kwenye serikali yake.Au wewe unaposema wakina BM walishindwa walishindwa yapi na BM alishindwa kama nani ndani yaserikali?.
 
Wafananishe Sasa utendaji kazi walipokuwa mawaziri ndo utajua Magu ni Nani na mende no nani! Unakuwa na akili Kama ya jogoo isiyokuwa na kumbukumbu mfyuuuu!
Mende ni mwizi na mhuni tu mmoja, hatufai Kama taifa! Magu ndio mpango mzima!
 
Wafananishe Sasa utendaji kazi walipokuwa mawaziri ndo utajua Magu ni Nani na mende no nani! Unakuwa na akili Kama ya jogoo isiyokuwa na kumbukumbu mfyuuuu!
Mende ni mwiI na mhuni tu mmoja, hatufai Kama taifa! Magu ndio mpango mzima!
Nimekudharau kwa sababu badala yakushambulia hoja, unashambulia mtoa hoja kwa hilo tu nimekudharau nakujua uduni wafikra zako niwakiwango gani, unapojaribu kuoanisha mafanikio yawizara kuna vitu vingi vinavyoangaliwa , ndio maana mpaka leo hujawahi kuona wizara ya mambo ya nje/wizara ya ulinzi /wizara ya mazingira na muungano vikiwa sawa na wizara ya mambo ya ndani katika ufanyaji kazi, Kuna baadhi ya wizara zina impact ya moja kwa moja katika jamii nanyingine impact yake nindogo au kuonekana nivigum.

Nikupe tu mfano Magufuli huyu kipindi niwaziri alishiriki kuuza nyumba za Serikali, alishiriki kuwambia wakazi wachato kama wanahitaji barabra ya lami wanye kinyesi kisha waiite lami, alishiriki kununua vivuko vibovu, aliingiza nchi hasara katika kesi ya samaki iliyofahamika kama samaki wa Magufuli.

Sasa naomba uniambie kipindi Membe waziri wa mambo ya nje aliiletea serikari hasara zipi?. Kisha ueleze kipindi JPM anafanya mambo mazuri huko ktk wizara je kwa nini sifa hizo asipewe kikwete kwa sababu ndio alikua raisi?. Je kipindi hiki ambacho Magufuli Serikali yake inajenga miundo mbinu kwa nini asisifiwe waziri wa wizara husika kama alivyosifiwa yeye badala ya kikwete?.
 
Sioni shida kudharauliwa na mpumbavu, huo uwekezaji wa bandari ya bagamoyo na mikataba ya kipumbavu nchi ilioingia ya kimataifa ulikuwa chini ya Nani? We na upunguani wako hujui ufisadi ulivyokuwa ukifanywa kwenye balozi zetu, nazo zilikuwa chini ya Nani!? Kupishana kwa viongozi waandamizi angani kwenda nje unafikiri aliyekuwa anashughurika navyo ni nani!
Tusichoshane, sijawahi kuhitaji heshima Toka kwa wapumbafu, na Wala sitaanza leo! Mende wako huyo hakuleta impact chants yoyote nchini kipindi Cha uwaziri wake! Hebu cheki wizara mbalimbali Magu alizohamishiwa uone Kama ipo moja ambayo alifanya vibaya? Unafikiri hiyo ilitokeatokea tuuuu! Magu Hana agenda ya usanii na wiziwizi! Ndio maana Sasa yanafanyika tusiyokuwa tunatazamia yangefanyika ...of course kwa wapuuzi Kama ww hamuiwezi kuona maana kwenu mnaona kinachoingia matumboni mwenu tu kwa kuwaibia watz...na kwa Sasa mtasubiri Sana Kama fisi anayetarajia mkono wa binadamu udondoke!
 
Najua kwa utopolo wa akili zako hoja ni kumsifia,kumtukuza na kumuabudu Magufuli na lichama lenu chakavu,Joka la Kijani lenye majeraha ya 2015.
Mwaka huu tuantia chumvi,pilipili na ndimu kwenye majeraha ya 2015

Pole sana MATAGA.
Sisi tunatukuza maendeleo yaliyofanyika chini ya jemedari JPM na hilo ndo jambo la msingi kabisa kila Mwananchi analifurahia, isipokua nyinyi wachache wenye chuki binafsi ndo mnabeza.

Chama kilichoshinda uchaguzi kinakuaje na majeraha? Au unakiitaje chakavu? Kilipata wabunge 287 Kati ya wabunge 392, kilipata Madiwani 2875 Kati ya 3946. Huku ndo kuchaakaa? Ndo maana nawauliza mpo serious au mnafanya utani au akili zimewaruka?

Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…