Uchaguzi 2020 Sababu ya kushindwa kuungana kwa ACT-Wazalendo na CHADEMA

JF Member

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
7,385
9,651
Nimefuatilia kwa ukaribu na kufahamu sababu nyingi sana zinazofanya ACT-Wazalendo na CHADEMA kuchelewa kuamua kuungana na kuunga mgombea mmoja wa Urais ama hata kutoungana kabisa.

Kwa sasa nitaweka hapa chache ila nikipata mda nitaandika Zaidi.

1. Sababu kubwa kabisa ni nani asimame kati ya Membe ama Lissu. Membe ametumia mda mwingi kujiandaa na anaonekana kuwa na nguvu kule kusini na hata baadhi ya wana CCM wanampatia matumaini ya kushinda Urais, wakati huo Lissu amekuja ghafla bila maandalizi. Japo Lissu anaonekana kuwa na nguvu kuliko Membe lakini wachambuzi ndani ya ACT Wazalendo wanasita kuelewa ni wapi hasa ataipeleka Tanzania iwapo watamuunga mkono na kushidwa Urais.

2. Sababu nyingine ni Mda wa maandalizi. Mda wa maandalizi ya kukaa mezani unaonekana kuwa mdogo. Kuna nguvu kubwa sana kutoka kwa wapenda mabadiliko kuona hivi vyama vikiungana lakini inaonekana mda ni kidogo hivyo kushindwa kufikia muafaka kwa baadhi ya mambo nyeti.

3. Uzoefu wa chaguzi zilizo pita hasa 2015. ACT-Wazalendo na CHADEMA vinashindwa kuungana hasa baada ya kuona UKAWA ilivunjika na hakuna hata faida ilipatikana kwa baadhi ya vyama katika muungano huo. Iwapo chama kimoja kitapeperusha bendela ya Urais na kushinda basi chama kingine kitakuwa chama pinzani baada tu ya uchaguzi.

4. Muungano. Swala la Muungani nalo linawekwa mbele. Mnajua ACT-Wazalendo kinanguvu Zanzibar na CHADEMA kinanguvu bara pekee. Iwapo CHADEMA itapeperusha bendera ya Urais bara na ACT-Wazalendo visiwani, ikitokea wote wameshinda basi Muungano utakuwa matatani hasa pale Maalim la Lissu wasipoelewana katika utendaji kazi. Ikumbukwe kila chama kina mlengo tofauti kuhusu Zanazibar.

5. Suara la Kuachiana Majimbo. CHADEMA kinataka Majimbo Mengi bara ili kikishika dola kisipate shida ya kufanya maamuzi pale bungeni. Ikumbukwe Rais anaweza akaondolewa kupitia bunge. Wakati huo ACT Wazalendo kinahofia kufutika bara iwapo tu kitakubariana na uamuzi huu hivyo kukifanya kuwa chama cha visiwani pekee, hii itakifanya kipoteze muelekeo huko mbeleni.

Nawatakia uchaguzi mwema.
 
Umepotosha sana mkuu.

Nisikilize vizuri, Mkakati wa Tume na Chama cha Mapinduzi ni kumwondoa eidha Membe au Lissu kwa technicalities.

Kwa sasa wote Membe na Lissu wameshachukua form. Wakipitishwa wote lazima mmoja amwachie mwenzie, akipitishwa mmoja lazima mwingine ashiriki kumsaidia aliyepitishwa. Kwa sasa wanaishi kama hawana mpango wa kuungana kwa sababu hata sheria inakataza.

Muda wa kuungana kama ilivyofanyika kwenye Ukawa ulishapita. Ndio maana kila mmoja ana fight kivyake, sasa subiri tume itakapo toa majina na mapingamizi kusikilizwa ndipo utajua kama wanaweka mgombea mmoja au la!
 
Kajifunze kuandika Kiswahili fasaha.Muombe akusaidie hata huyo mumeo uliyelala naye jana usiku.

Suara ndio nini?

Swala ndio nini Mnyama au?
 
Back
Top Bottom