Nini ilikuwa kusudio la rais kukutana na wazee wa CCM Dar?

Hivi mpaka sasa wapinzani hawajatoa hotuba yao kujibu/kufafanua ile ya mh JK? Maana at least ina upotoshaji flani. Kuhusu kuchagua hadhira yake cjui kwa nini isiwe wasomi wa vyuo na badala yake akachagua "wazee" wa ccm ambao anawaita wa DSM.

kukanusha peke yake haitoshi...wakanushe watoe na ratiba ya maandamano
 
kambarage alikuwa pia na tabia ya kuongea na wzee wa DSM mbona hamkohoji .....

acha mambo ya kijinga..una tuambia mbo ya kambarage leo tuko mwaka gani kambarage alifanya hivyo mwaka gani...huo ujinga tafuteni makundi ya kuwaeleza na kujaribu kufananisha miaka ya 70 na leo..
 
Je tutegemee siku aseme anaongea na vijana wa DSM or any were in TZ? Najua aliumiza akili jins yakukwepa maswali ambayo yatamfanya ajibu sijui ni kwanini
 
Mkuu utaumiza kichwa bure, raisi hakutaka kuongea na wazee wa dar la-hasha, mara zote ambazo anaongea na wazee wa dar si kwamba kweli anaongea na wazee wa dar, kifupi alitaka kuongea na wananchi wote na hasa aliwalenga chadema... jiuliza kama nia ni wazee wa dar? kwa nn irushwe TBC wakati wazee wote aliowataka na hasa walotaka kumsikiliza walikuwepo ukumbini? TBC ilikuwa inaruhsha matangazo kwa nani tena? Au wazee ukumbini walikuwa hawamwoni mkulu hadi ziwepo screen za TBC? hii ilikuwa ni kisingizio cha wazee tu lakini wala hakuwa na mpango na wazee
 
Songíto;2852398 said:

nikweli rais alikua anaadress taifa, lakin hakusema jinsi atakavyo adress matatizo yanayowasibu watz kwa ujumla. Amedhubutu kulaumu na kusingizia mtikisiko wa uchumi na cdm. Mheshimiwa haja onyesha kuguswa na matatizo yaliyoko na ndio maana hajasema mbinu alizonazo kama serikali.
Ninaamin rais anaguswa zaid na harakat za cdm kutatua tatizo kuliko tatizo lenyewe. Viongozi wasome alama za nyakati, wakinyamaza cdm watanyanyuka wengine kudai haki hiyohiyo kwa jina na itikadi nyingine. Nadhani hatujamsahau mrema alivyokubalika miaka ile!? Chadema na njia sahihi ya wananchi inayotumiwa kwa sasa kama ilivyokua kwa nccr enzi za mrema. Viongozi wakubali mabadiliko yakatiba sasa kwasababu kwa manufaaya taifa
 
wale walikuwa si wazee bali na wauni wa dsm,,,,,wazee wa ukweli wapo vijijini kwenye njumba za tembe
 
wale walikuwa si wazee bali na wauni wa dsm,,,,,wazee wa ukweli wapo vijijini kwenye njumba za tembe :shock:
 
Wadau inasikitisha sana kuona watu wanachanganya madawa na kushindwa kukaa kwenye mada ya msingi, kiasi wengine mnaonekana kuandika tu na kulaumu tu lakini maandiko yenu na lawama zenu zinawasuta kuwa hamjui kinachoendelea.

1. Raisi kuunda tume, hiyo ni kanuni ya katiba.
2.Raisi atakabidhiwa Rasimu iliyokamilika, ikiwa na maoni ya wananchi.
3.Akishaipitia ataikabidhi kwa Bunge maalum (Bunge la katiba)
4.Bunge la katiba litaijadili, mpaka waiafik na maafikiano ya waraka huo bado hayajawa katiba. Mpaka
5.MIMI na WEWE, Watazania wenye haki ya kupig kura tuipitishe katika kura ya maoni.

Sasa hapa kisichooeleweka nini? au ndio hayo mazowea, hapa kila mtu ana FURSA: CCM, CHADEMA, CUF, NCCR nk, wewe na mimi tusio na Vyama bila kujali Dini zetu, Rangi zetu Makabila wala jinsia.

Tujengeni hoja kwa kuisoma katiba iliyopo, tuone matatizoyaliyomo na tuhakikishe tunayatolea maoni na maoni hayo ni LAZIMA tuhakikishe yanaingia katika Rasimu mpya kwa mfano:

Kipengele 46. (1) (2) (3) na 46A mpaka ni wazi vimempa Rais madaraka yanayochupa mipaka.
Jambo ambalo yanapotokea maswali fulani ni rahisi kwa rais awe au asiwe madarakani kujificha nyuma ya vifungu hivyo (JF Mkapa above the LAW?)

Ili ufanane na Great thinkers you must perform and act like One.
Kwa hiyo tujikite kwenye hoja za msingi, sio vijembe na kudokoana! Tumetaka na kudai Katiba mpya, tumepewa uwanja tucheze kama wachezaji wa kulipwa. Tutumie Elimu tulizonazo, hasa kwa ndugu na jamaa zatu ambao tunadhani watakuwa au wana uzito katika kaelewa maswala haya.
Hili ni la TAIFA na vizazi vijavyo.
Mungu ibariki Tanzania.
 
acha mambo ya kijinga..una tuambia mbo ya kambarage leo tuko mwaka gani kambarage alifanya hivyo mwaka gani...huo ujinga tafuteni makundi ya kuwaeleza na kujaribu kufananisha miaka ya 70 na leo..

Nyie katafteni wa kuongea nao kama hamtaki kuongea na wazee. Mlilazimishwa? kinawauma nini anapoongea na wazee au watoto wa wazee waliokuwa mstari wa mbele kudai Uhuru / Madaraka ya nchi hii?

Unamjuwa yule mzee aliyekuwa pembeni yake? unawajuwa wale wazee waliokuwa pale mstari wa mbele? Nna uhakika huwajui na sina haja ya kukupa faida.
 
Wadau inasikitisha sana kuona watu wanachanganya madawa na kushindwa kukaa kwenye mada ya msingi, kiasi wengine mnaonekana kuandika tu na kulaumu tu lakini maandiko yenu na lawama zenu zinawasuta kuwa hamjui kinachoendelea.

1. Raisi kuunda tume, hiyo ni kanuni ya katiba.
2.Raisi atakabidhiwa Rasimu iliyokamilika, ikiwa na maoni ya wananchi.
3.Akishaipitia ataikabidhi kwa Bunge maalum (Bunge la katiba)
4.Bunge la katiba litaijadili, mpaka waiafik na maafikiano ya waraka huo bado hayajawa katiba. Mpaka
5.MIMI na WEWE, Watazania wenye haki ya kupig kura tuipitishe katika kura ya maoni.

Sasa hapa kisichooeleweka nini? au ndio hayo mazowea, hapa kila mtu ana FURSA: CCM, CHADEMA, CUF, NCCR nk, wewe na mimi tusio na Vyama bila kujali Dini zetu, Rangi zetu Makabila wala jinsia.

Tujengeni hoja kwa kuisoma katiba iliyopo, tuone matatizoyaliyomo na tuhakikishe tunayatolea maoni na maoni hayo ni LAZIMA tuhakikishe yanaingia katika Rasimu mpya kwa mfano:

Kipengele 46. (1) (2) (3) na 46A mpaka ni wazi vimempa Rais madaraka yanayochupa mipaka.
Jambo ambalo yanapotokea maswali fulani ni rahisi kwa rais awe au asiwe madarakani kujificha nyuma ya vifungu hivyo (JF Mkapa above the LAW?)

Ili ufanane na Great thinkers you must perform and act like One.
Kwa hiyo tujikite kwenye hoja za msingi, sio vijembe na kudokoana! Tumetaka na kudai Katiba mpya, tumepewa uwanja tucheze kama wachezaji wa kulipwa. Tutumie Elimu tulizonazo, hasa kwa ndugu na jamaa zatu ambao tunadhani watakuwa au wana uzito katika kaelewa maswala haya.
Hili ni la TAIFA na vizazi vijavyo.
Mungu ibariki Tanzania.

Umenena vyema sana natafuta kakifungo cha like sikaoni/ Pokea hug.
 
Back
Top Bottom