Nini hutokea kichaa kisababishwacho na mapepo kinapompata Mwanadamu?

Nini hutokea kichaa kisababishwacho na mapepo kinapompata Mwanadamu?

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
25,938
Reaction score
41,098
Salaam, Shalom!

Aina ya ukichaa ninayoiongelea Leo, ni tofauti, SI Ile inayotibika hospitalini,

Aina hii ya ukichaa ni Ile ambayo madaktari hupima Kila kitu na kuona kipo sawa, wasione ugonjwa wowote, lakini mgonjwa Hali ni Tete.

NINI HUTOKEA KATIKA AINA HII YA UKICHAA.

Pepo au jini aliyetumwa na sangoma, ndio maana Hawa wapiga ramli wanatakiwa wafutwe wote ikiwa tunataka Hali njema mitaani, masangoma hutumia mapepo ili kumfanya awe kichaa, Pepo akimwingia mtu, huingia ndani ya mtu na kukaa ndani ya ufahamu na kushika maamuzi na Network zote za mtu,

Wakati hayo yakiemdelea, mtu halisi, nafsi huwa imefungwa mahali pengine asikumbuke chochote muda wote ambao Pepo atatumia mwili ule, na hii hufanyika kwa kuchukua nafsi kwa kutumia sample kama nywele,mate, nguo nk nk.

Kumbukumbu ya mtu aliyetawaliwa na Pepo la ukichaa hufutika jumla, atakumbuka yote kabla ya ukichaa haujamdaka, na ikitokea amerudia utimamu wake, atakumbuka tu hatua ya mwisho kabla ya kuwa kichaa kurudi nyuma, hii ni uthubitisho kuwa ndani yake, alikuwa replaced na Pepo ambalo ndio hasa hufanya yote afanyayo kichaa wakati watu wakidhani ni Yeye afanyaye ilhali siyo.

HIZI NI TABIA ZA VICHAA WALIOSABABISHIWA NA MAPEPO.

1. UCHAFU.

Mapepo ni viumbe vilivyolaaniwa, UCHAFU ni tabia zao kuu, haogi, hupenda UCHAFU na kukaa majalalni na kula UCHAFU, huko ndiko makazi ya mapepo ndio maana yakishaingia ndani ya mtu, yatampeleka jalalani, ndio maana wengi waokota makopo,huishia kuwa wachafu baadae ukichaa huwaingia polepole, wanaokota Roho hizo majalalani.

Ufugaji wa Rasta ni ukichaa mmoja wapo, witch doctors wapiga ramli huo ndio mwonekano wao asili sababu ya kukaliwa na mapepo, sasa unayefuga Rasta, jua inakaribisha ukichaa.

2. KUTEMBEA KWA KURUDI NYUMA.

Nadhani umewahi ona kichaa anapiga hatua mbili mbele Kisha anarudi hatua Tano nyuma, hii ni tabia mojawapo ya mapepo, SI mtu yule,

Mapepo yaliyolaaniwa, mengi hufanya na kutenda kinyume na wanadamu, ndio maana vichaa, misukule hula kwa kutumia nyuma ya kiganja Cha mkono, ni mapepo ya ukichaa Yale.

Utakutana na mtu atembea kwa kurudi nyuma na hajikwai, ni Pepo lile ndio laana yenyewe.

3. HASIRA.
Vichaa wengi huonekana na hasira, violent, utashangaa anakuwa na tabia ngeni, SI Yeye ni Pepo Hilo, mkeo akikasirika kupitiliza au mumeoo, stuka, ni Pepo Hilo, hata maandiko yameandika, hasira isiyo na kiasi ni ukichaa, mtu anakasirika Hadi anapiga kichwa ukutani kwa hasira, ni hatua za kwanza za ukichaa.

(Mathayo 8:26-33)

Yesu alikutana na aina hii ya ukichaa nchi ya wagerasi, mtu yule alikuwa hatari mkali usiweze hata kumfunga kwa pingu za chuma ,alizikata, alikaa pekeake makaburini bila kula chochote na hakufa. Ndipo ukumbuke kauli ya Yesu kuwa, mtu hataishi kwa mkate tu, Bali... Yesu alipotoa kundi lile la mapepo, nafsi ya mtu yule ilimrudia, akawa timamu Tena.

4,5..6,7.............jazia mwenyewe.

ANGALIZO:
Kumtoa Pepo wa kichaa ndani ya mwili wa mtu, ni shart tuhakikishe nafsi ya mtu huyo imefunguliwa huko illikofungwa Ili irudi kuchukua Nafasi ya Pepo lililovamia, ukishindwa Kurudisha nafsi na Pepo limetoka, mtu huyo ndo atakuwa amefariki kirahisi tu hivyo🤔.


Ikiwa unapenda kumkaribisha Yesu Maishani mwako Ili upate nguvu na mamlaka ya kushinda nguvu za Giza, fuatisha sala hii,

EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINA KUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU,NIPE UWEZO WA KUSHINDA NGUVU ZA GIZA,DHAMBI ISINISHINDE, UOVU USINISHINDE, ULEVI USINISHINDE, UZINZI USINISHINDE, UCHAWI USINISHINDE, NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU. AMEN


MUNGU AWABARIKI SANA 🙏
 
Moderators, mada hii iende habari mchangannyiko🙏
 
No. 2 nimeshuhudia.

It was so sad to see my loved one in that situation.

We tried to help him out of that situation unsuccesful till his death 2014

And all this started the moment he accept GOD, Till today i don't understand what message GOD was communicating to us.

Rest easy Sambilangwa, You fought it well, Perhaps we shall meet again if there will be another life.
 
Nafahamu Kuna mstari mwembamba sana kati ya utimamu wa akili na kuwehuka( ukichaa). Kila binadamu anaweza akawehuka ila inategemea na sababu nyingi kuanzia mazingira, uwezo wake wa kuhimili msongo, historia ya familia alipotoka, imani yake, matumizi ya vilevi n.k.

Pia kuna ukichaa ambao sababu zake zilizosababisha hali hiyo hazijulikani bado mpaka sasa.

Kitaalamu kila binadamu ana ukichaa wake uliojificha na anaweza akalipuka na kuwa kichaa au kuwehuka kukiwa Kuna visababishi vitakavyofanya avuke kutoka mstari wa utimamu.

Kuhusu uhusiano wa mapepo na ukichaa ni jambo linalohusu imani kwa maana ya kuamini kitu ambacho hakipo ila ni cha kufikirika tu. Tunaweza kuongelea uhusiano wa vichaa na familia walizotoka, ulevi, vinasaba, jiografia n.k kwa sababu tunajua na kufahamu ila ni ngumu kuoanisha uhusiano wa mapepo ambayo hayapo ila ni nadharia tu na visababishi vya kuwehuka.
 
Aina hii ya ukichaa ni Ile ambayo madaktari hupima Kila kitu na kuona kipo sawa, wasione ugonjwa wowote, lakini mgonjwa Hali ni Tete.
 
Aina hii ya ukichaa ni Ile ambayo madaktari hupima Kila kitu na kuona kipo sawa, wasione ugonjwa wowote, lakini mgonjwa Hali ni Tete.
 
Hata kuteka, kutesa, kufira,kupoteza na kuua wakosoaji ni ukichaa, nchi inayoongozwa na kichaa lazima inatumbukia shimoni tu.
 
Back
Top Bottom