Nini hatma ya ujenzi wa soko la Tarime mjini

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Wafanyabiashara walipewa notisi na Halmashauri ya Mji wa Tarime juu ya kuvunjwa vibanda vyao ili kupisha ujenzi wa soko la kisasa. Pamoja na hayo walitakiwa kulipwa fidia ya vibanda vyao kitu ambacho Halmashauri ya mji wa Tarime hakikufanya.

Wenzao wa Geita walipovunja mabanda katika mji wa Geita waliwalipa wafanyabiashara fidia ya vibanda vilivyovunjwa. Vibanda hivi tangu vivunjwe sasa yapata muda wa mwaka mmoja na hakuna ujenzi ulioanza. Ikumbukwe kuwa wafanyabiashara waliobomolewa waliahidiwa kuwa ujenzi utakamilika kwa muda mfupi na hivyo watarejea kwenye vibanda vilivyojengwa vizuri na kwa mpangilio. Mpaka sasa wafanyabiashara wanataabika sana na wametapakaa na hakuna sehemu muafaka ambapo mnunuzi anaweza kwenda na kununua bidhaa kwa urahisi.

Swali la kujiuliza, Je ni kwa nini Halmashauri ilikurupuka kubomoa vibanda wakati hawakuwa na fedha mkononi? Je ni lini ujenzi utakapoanza ili wafanyabiashara wawe na matumaini ya kurudi kwenye vibanda vyao. Je ni kikao gani kilicholeta hoja hii ya kubomoa vibanda? Tunaitaka Halmashauri ya Mji wa Tarimeione umuhimu wa kuanza ujenzi wa soko haraka iwezekanavyo.
 
MKUU HIVI ILE STEND YA TARIME ILIKWISHA WEKWA LAMI KWELI?? 🤔🤔🤔
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom