Nini hatma ya CCM baada ya Rostam... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini hatma ya CCM baada ya Rostam...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkandara, Jul 16, 2011.

 1. M

  Mkandara Verified User

  #1
  Jul 16, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nimemsoma Rostam vizuri sana ktk waraka wake wa kujiuzuru na hakika mwandishi wa hotuba yake ni mzuri na anaijua kazi yake. Pamoja na mapambo mengi jambo moja ambalo lenye ukweli na Rostam kashindwa kuliweka wazi ni pale aliposema kwamba mpango wa Kujivua magamba ulikuwa viongozi wa kamati kuu na sekretariet kujizuru na kumpa nafasi rais kuchagua viongozi wapya...

  Lakini ukweli tunaoufahamu ni kwamba Makamu mwenyekiti wa CCM aliwatumia RACHEL barua za kujiuzuru. Haikuwa uvumi wala maneno ya Chiligati na Nnauye bali kamati iliamua na majina haya halitolewa kwenye mkutano wa NEC uliopita ambapo nakumbuka vizuri sana Sophia Simba alijaribu sana kuwatetea. Rostam amefukuzwa na kujiuzuru ilikuwa kufunika kombe mwanafaramu apite lakini Rostam kalifunua..

  Sasa napomsoma Rostam kwa madai yake ambayo yanaonyesha wazi kwamba kuna mgawanyiko ndani ya chama na hakika mapokezi ya Rostam yameweka doa kubwa kwa chama tawala sii tu kwa jimbo la Igunga bali mkoa mzima wa Tabora ambao ulituma wajumbe wake toka kila jimbo kumpa mkono wa kwa heri na kionyesha masikitiko yao kwa kuondokewa na Robin hood..

  Katika majumuiko ya maswala yote haya najaribu kufikiria hatma ya chama hiki hasa pale watakapo jiuzuru Lowassa na Chenge ambao kati yao nina mashaka makubwa na Lowassa kwa sababu huyu baba kesha jifunza angamizo lake alipojiuzuru kama waziri mkuu na shidhani kama safari hii atakubali kuondoka biila kufukuzwa kama chama kilivyoatoa maagizo..

  Na iwapo hawa wote wataondoka, nashindwa kuelewa nguvu ya Jk itatoka wapi ikiwa The brain, financer na wakili wake watajiondoa na kumwacha yeye pekee kama Alpacino ktk mchezo wa Scarface, au Robert DeNero ktk Al Capone! huku akibakiwa na mtu mmoja tu ktk kundi lake la kwanza - mzee Sitta!

  Kweli ameweza kuwacheza akili wengi waliotangulia toka baraza lake la kwanza la mawaziri kina Msabah, na watu wake wa karibu sana kama marehemu mzee Ditopile wote wameondoka kwa huzuni achilia mbali wale walioshughulika sana ktk kampeni za kumweka Ikulu na akawaacha solemba kama kina mzee Janguo.

  JK atabakia Mpweke huku wimbi kubwa la Upinzani ukidai mambo magumu sana ambayo yalishindikana toka enzi za mwalimu...Miaka minne mizima imebakia kabla ya uchaguzi ujao na JK yuko kiti kikubwa, Sijui ya kesho, Mungu pekee ndiye anajua lakini Uhai wa CCM upo ICU wataweza vipi kupita mtihani huu...
   
 2. O

  Omr JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Maneno mengi lakini hakuna hata moja lenye maana..CCM ni kubwa kuliko kina Rostam au umesahau kuwa wametajirikia kupitia CCM.
   
 3. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2011
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Hawa watetezi wengine wanaotumwa hawajui hata wanatetea nini ukiwaambia CCM wezi wanatetea hapana, sasa hapa wenyewe wanasema ametajirikia CCM. Hivi mnatetea nini hasa, maana hatuwaelewi!.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Jul 16, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mzee.. kuna kitu kingine ambacho nimekifikiria sana; je, nguvu ya Rostam ilitokana na kuwemo katika nafasi za uongozi wa CCM? Kwamba baada ya kujitoa katika uongozi huo basi nguvu zake nazo zimekwisha. Hili likanikumbusha simulizi la Samson, Delila na Wafilisti walipokata Nywele zake na kuondoa "asili ya nguvu zake" waliamini kabisa kuwa wamemamliza? In a sense they did.. but did they?
   
 5. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  rostam amesema hana kinyongo lkn kama ataamua nae aharibu basi ccm hapatakalika, anajua mengi yule, eti rostama balali alikufaga au yupo mbele?
   
 6. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #6
  Jul 16, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Kumbe mwanakijiji ni msomaji sana.

  Ukweli ni kuwa kama Rostam kaondoka kwa maneno aliyotumia kujivua gamba, basi CCM iko mahututi sasa hivi, which is what I have been dreaming of. Ila kama ametanganza kwa sababu ya kuifanya CCM ya kikwete ionekane iko siriasi ilhali status quo iko pale pale, basi sijui la kusema. Tanzania is still one of the most unpredictable societies in the modern world !!
   
 7. k

  kijiichake JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2011
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 285
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Ccm ni ccm na ni chama cha vichaa, wezi, na matapeli, kimepoteza mwelekeo, mfa maji haachi kujitapatapa, joka limepondwa kichwa hivyo limebakia likirusha rusha mkia. Hata angeondoka jk,el,ra,ac,st, nk' haingewezeka kurudisha imani kwa wanaichi wenye maisha duni. Waliosema kidumu chama cha mafisadi sasa wajue wazi hakuna cha kidumu wala cha kindoo. Tumewasoma kiburi walicho nacho tokea bungeni hadi kwa halimashauri tutawatema tuu.
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Jul 16, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hahaha Mwalimu.. kuna column/ hotuba moja Nyerere aliwahi kuandika (sikumbuki title yake) lakini ilikuwa inahusiana na "furaha ya kujisomea" .. nadhani ilikuwa wakati akifungua ile Library yetu hapo Dar.
   
 9. N

  Nyamizi JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2011
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 1,401
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Mimi naona CCM iko mahututi tayari,sasa hivi wametaharuki,wao walidhani jamaa ataachia U-NEC peke yake ndani ya chama,lkn kitendo cha kuwarudishia hata na ubunge wengi wao hawakutarajia na ndio maana mpk sasa hivi kina Nape wamepigwa ganzi,hawajui what is the next move ya RA,time will tell.
   
 10. The dirt paka

  The dirt paka JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  wanasema eti ni ukomavu wakisiasa does it sense?
  Mwizi anapofikia mwisho hana ujanja anaonekana shujaaaa! CCMMMMMM,...! Wamedondokea pua.
   
 11. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  RA is very strong man especially in his field(international b'ness man) dont expect kwamba kuacha Ubunge atakuwa amefilisika: kweli tunaweza kusema kwamba RA kapata utajiri pengine kwa kuchakachua pesa na mali za watanzania akiwa kama mbunge ndani ya miaka 18 lkn kumbuka ameishajiwekea mtandao mzito-ni international figure: mimi nina imani akiamua kuwa mkweli kwa watanzania wote ukiachilia wa Igunga waliokua wanatoa machozi waliposikia kuwa mbunge wao ameachia ngazi, basi CCM hapatakalika, RA kwa ujanja ujanja wake alikuwa anakibeba sana Chama.
   
 12. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #12
  Jul 16, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0

  Atabaki mpweke vipi wakati ana maliza muda wake na kula pension.. Kwanza mi nahdni JK anatamni hata 2015 iwe kesho aanze kusafiri huku vyombo vya habari vikiwa havimmuliki

  Pili Jahazai la CCM linakwenda kwa upepo. Haya yote tunayoona ni kama jahazi likifika watu watamsifia rubani( JK)lakini ukichunguza rubani yeye anategemea upepo na maijinia wake( Nape, Mukama Msekwa).

  sometime nashindwa kumuweka JK kundi fulani. Ni mnafiki??, au ni Muoga???, au Hajui uwezo na wajibu wake kama mwenyekiti wa chama , rais na amiri jeshi mkuu.??? Kwa nini hawi center ya haya mambo. ?

  yote hayot isa kwa wataka mabadiliko tunafurahi sijui hao waleta mabadiliko kama nao wanajipanga au wanabweteka.
   
 13. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #13
  Jul 16, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Nadhani wanatetea hii generalization ya kipumbavu, haiwezekani CCM wooote wawe wezi, hii ni sawa kuita CDM wooote wavuta bangi eti kwa sababu Mbowe anavuta.
   
 14. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #14
  Jul 16, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Mi wasi wangu ni hii kadi ya CCM anayoing'ang'ania!! Kulikoni? Inawezekana vp analalama siasa uchwara na za hovyo ziszo na tija ndani ya CCM yeye haziwezi na bado kadi ya chama ipo mkononi maana yake ni nini?
   
 15. M

  Mwadada Senior Member

  #15
  Jul 16, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  It's still a drama. Its my hope that only time will tell the real truth and everything will be out. Therefore every move should be careful watched.
   
 16. m

  mtimbaru Member

  #16
  Jul 16, 2011
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 74
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kujiuzuru kwa RA ni pigo kubwa sana kwa CCM na viongozi wengi aliowaweka kwenye madaraka kwa kutumia influence,
   
 17. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #17
  Jul 16, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,649
  Likes Received: 4,750
  Trophy Points: 280
  Avatar yako imemaliza kila kitu,ndivyo ulivyo.
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Jul 16, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hakuna asiyejua kwamba CCM ni chama kubwa, na Rostam amepata umaarufu wake akiwa ndani ya chama wala sio Utajiri kama wanavyodai maanake utajiri ndio umemwezesha Rostam ktk nafsi hizo. Rostam ni sawa na volcano inayowaka chini ya bahari! ni vigumu kwa mtu asiyejua kuambiwa moto unaweza kuwaka ndani ya maji ya bahari na usizimike ndivyo ilivyo vigumu kufahamu nafasi ya Rostam ktk chama kubwa (bahari).

  Kuondoka kwake ni mpasuko wa volcano hiyo ambao unaweza kusababisha mtikisiko wa ardhi (earthquake) chini ya bahari na matokeo yake ndio Tsunami kama la Japan! na hata kwa udogo wake lile la Indonesia kwani bahari ikichafuka waarithika sio samaki tu hadi viumbe wa nchi kavu ambao tulidhania tuko salama.

  Kama alivyosema Mtazamaji, yawezekana kweli CCM ni jahazi linalokwenda kwa nguvu ya upepo, hivyo kuondoka kwa mvuta kamba hakuwezi kuzuia safari lakini sidhani kama tutashindwa kuelewa tobo aloliacha Rostam na linaingiza maji chomboni..Labda ingekuwa vizuri ningeuliza hatma yake yeye Rostam baada ya kujiuzuru lakini dukuduku letu wengi ni kutazama hatua gani zinafuata baada ya kujiuzuru kwake kwani imeonyesha wazi kuwa chama kubwa kimekubali RACHEL ni lazima waondoke kwa sababu ya tuhuma za UFISADI..Na asikudanganye mtu, ktk nchi maskini ukiondoka ktk picha ya kisiasa ama utawala basi na nguvu yako ktk jamii inaondoka na hutathaminiwa tena maishani.

  RACHEL wanalijua hilo na zaidi ya yote wanafahamu kwamba wananchi wana machungu nao kutokana na scandals za RADA, EPA na Richmond wakati utawala wa JK unakwisha miaka minne ijayo!. Sidhani kama huu ni mchezo mdogo kama mnavyoufikiria.
   
 19. N

  Nyamizi JF-Expert Member

  #19
  Jul 16, 2011
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 1,401
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Mkandara,ninaamini RA hawezi kukubali kuporomaka kirahisi hivi hasa ukizingatia power aliyokuwa anaenjoy akiwa ndani ya chama kufikia status ya kuitwa King Maker,believe me,he will strike back na uchaguzi ujao ndani ya chama ndio utatoa picha kamili ya move hii aliyoianzisha ya kusurrender powers zake.
   
 20. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #20
  Jul 16, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  mzenji umeharibika sana, huko nyuma haukua hivyo...
   
Loading...