Nini hatima ya wanasheria vodafasta?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini hatima ya wanasheria vodafasta??

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Leornado, Jan 14, 2011.

 1. L

  Leornado JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mkupuo wa kwanza zaidi ya 300 wamekuwa mawakili binafsi, bado mikupuo mingine ya Law school. Nini hatima ya hii taaluma nyeti kwa hapa TZ??
   
 2. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  ‘We marked 49 years of independence on December 9 but it is a shame that some regions do not have even a single advocate to defend the people's rights …this is unacceptable and we lawyers should take note of that," the CJ said. Tanzania needs at least 7,000 to 8,000 advocates in order to meet the growing population and minimize the current ratio of one advocate to attend to 36,000 people before the admission of the 337 advocates. Kenya has more lawyers than us.
   
 3. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  hivi do we need lawyers to develop? ni swali tu. maana hata gharama zao ni vigumu kwa mlalahoi kama mimi kuwa na advocate kusimamia kesi zangu. they end up defending mafisadi and in the end hata wao wnaishia kuwa mafisadi.
   
 4. F

  Ferds JF-Expert Member

  #4
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 1,267
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  hata kama wangeapishwa wawili kama ni maji ni maji tu, siju watanzania mnataka nini, kelel kila leo lawyers hawatoshi, juhudi za kuziba pengo zinafanyika mnawaita vodafasta, miswahili inakera hii
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  Jan 14, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sijaelewa hii notion ya "voda fasta" inatoka wapi! Kwa sababu ni wengi (quantity) au ubora (quality) sio mzuri? Na kama ni habari ya ubora, nani aliyefanya research kuufahamu ubora huo?
   
 6. akajasembamba

  akajasembamba Senior Member

  #6
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 161
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hatima ya taaluma nyeti kama hii ni kushuka thamani yake na wanasheria wenyewe kudhalilika, swala si kushindana na Kenya cha muhimu ni kuboresha elimu, sasa anybody can be a Lawyer ada yako tu, mtu tangu chekechea hadi secondary hajawahi kupata VEMA katika daftari lake ati na yeye leo ni Lawyer! what a shame what a disgrace,! haya mambo ni sawa na WALIMU WA UPE.Kama Sheria ingekuwa sawa na URUBANI kama hujui ndege inadondoka nadhani wasingekurupuka na kuproduce quantity bila kuangalia quality, ila tutaona wanasheria wakizidisha mikataba mibovu, na kushindana kushinda kesi kwa KUTOA RUSHWA mana kujenga hoja zenye mantiki hawana uwezo, Mikoa haina wanasheria kutokana na umaskini wa mikoa hiyo there is simply no market who will pay them, they aint charitable organisations! kuzidisha idadi ya wanasheria hakutawafanya waende Mtwara au Lindi wakati hakuna kipato cha kuwawezesha waishi.
   
 7. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #7
  Jan 23, 2011
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Nadhani hii taalum ya sheria inatakiwa iangaliwe upya. Ifanywe professional degree ili kupunguza idadi ya wanasheria makanjanja. Mtu asiruhusiwe kusomea sheria hadi awe na degree nyingine.

  Hivi mwanasheria wa Tanzania anaweza kusimamia kesi inayohuasiana na utabibu, biashara za kimataifa, au sayansi ya mazingira, au kemikali wakati hajui a wala be ya tasnia hizi?
   
 8. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #8
  Jan 23, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Una hoja nzuri.
  Vipi upo nje kwa dhamana au! maana naona nembo yako bado ina maandishi ya Ukonga.!
   
 9. S

  SHINENI Member

  #9
  Jan 31, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nashukuru watanzania wachambuzi mpaka wanashindwa kuwa na ukomo wa upembuzi,ivi kupitia law school unaona is a Joke?kama kati ya candidates 300 wanafaulu 25-35 huoni kama ni kama ilivyokuwa awali kuwa wanaapishwa mawakili 20-40 kwa intake moja ya CLE.Mimi kwa mtazamo wangu ni kuwa legal proffessional is a performance and not not been big headed on the way brought others in the field
   
 10. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #10
  Jan 31, 2011
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Lini tena wanaapishwa mawakili wengine na wanaweza kuwa wangapi kwa idadi? pls mwenye hii info anijuze, am serious
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #11
  Jan 31, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,527
  Trophy Points: 280
  Bongo ni matatizo kweli, kutokana na uchache wa mawakili waliokuwepo, wakafanya demand iwe kubwa, hivyo legal fees zikawa juu sana watu wa kawaida wakashindwa kumudu enzi hizo, UDSM ndio chuo pekee kikitoa LL.B, tena admission ilikuwa only 60 students tena wote ni wa Div One.

  Mzumbe, Tumaini, Dodoma, Morogoro na Zanzibar, wakajoin team, sasa LL.B zinamwagwa kama njugu, na mawakili kibao. Hili ni jambo jema sasa huduma za kisheria zitakuwa more reachable na more afordable kwa kila mtu. Itafikia wakati, mawakili watabisha hodi kwako, wakiomba kukupatia huduma za kisheria bure, ukishalipwa ndipo uwalipe!. Hili ni jambo la kheri, wewe unalitilia shaka?.

  Angalizo: Kusomea sheria na kupata LL.B ni jambo moja, kusajiliwa na kuwa wakili ni jambo jingine, lakini pia kuwa wakili mzuri, nalo ni jingine kabisa!. Kuna mawakili tena wengine vichwa na 1st class zao, lakini mahakamani ni sifuri wakati kuna mawakili wa kawaida tuu, mahakamani ni moto!.
  Katika ya mawakili wote wa Tanzania, mfano wa Murtaza Lakha sijamuona mwingine!.
   
 12. S

  Sumu Baridi Member

  #12
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nilisoma Lawschool Cohort ya 4(2009/2010) katika masomo/mitihani kama 13 nina Supplementary ya mitihani miwili mmoja Core na mwingine ni Non Core,and here i am,sija apishwa kuwa wakili,hadi pale nitakapo faulu masomo hayo ndo ntapata fursa ya kula kiapo baada ya kufanya petition,sasa ninaomba anayedhihaki juhudi za ongezeko la mawakili aende akaicheze ngoma ya LST ili apate cha kunena humu jamvini...
   
 13. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #13
  Feb 5, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  kwakweli mimi naombea wawe wengi mana ss hivi kama wachache sana kiasi kwamba garama zipo juu sana angalau wakiwa wengi ushindani utakuwa mkubwa na bei itakuwa cheep
   
 14. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #14
  Feb 6, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mimi sina tatizo sana na mbinu zinazotumika na Law School kuchuja wanasheria japo kuna mapungufu hapa na pale yanayotokana na uzoefu. Kwa mfano, walimu wengi wa full time ni academicians zaidi kuliko practitioners na nafasi ya shule ya sheria ni practice zaidi kwa vile wanafunzi wanakuwa wameshamaliza mambo ya nadharia vyuoni. Hili naona ni tatizo la uchanga wa shule lakini kadili muda unavyokwenda mabadiliko yanafanyika.

  Jambo ambalo ningependekeza litizamwe huko mbele ni kuongeza muda wa mafundisho ya vitendo. Kijana anatoka chuo leo anakaa mwaka miezi kadhaa katika Law School na baadae kukaa kwa miezi kadhaa katika office za mawakili hata bila kufuatiliwa vya kutosha baadae anapewa mitihani ya darasani na mahojiano kidogo anakuwa mwanasheria.

  Tatizo nililoliona ni kwa wale ambao hawakupita Law School kwa sababu walimaliza vyuo kabla Law School haijaanza. Tofauti na kipindi cha nyuma ambacho Bar Examination ilikuwa inampima mtahiniwa vya kutosha, kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita Bar Examination imekuwa kama suala la formality tu. Watu wengine wanafaulu Bar examination anakuja ofisini hata kuandika Demand Letter hawezi. Sera ya Kitengo cha Elimu ya Uwakili imekuwa ni kuhakikisha wale wote waliotangulia Law School wanakuwa enrolled ili utaratibu wa kupitisha mawakili uwe mmoja.


  Tatizo lingine ambalo ni kubwa sana ni aina ya digrii za sheria zinazotolewa na vyuo vyeti vya siku hizi. Kwa kweli kuna idadi nzuri tu ya wahitimu wa shahada ya sheria wa siku hizi ambao ukiwatathimini kwa uadilifu wako chini kwa viwango ukiwalinganisha na wahitimu wa vyeti vya sheria katika Chuo Kikuu cha Dsm na Chuo cha Mahakama Lushoto. Mtu anakuja na gamba la digrii ya sheria tena hana pasi mbaya sana lakini hata elemenary concepts za sheria za mwaka wa kwanza hazijui. Ndio maana siwalaumu sana Law School kutulia umhimu katika mafunzo ya nadharia pia maana wahitimu wengine wanaowapokea inabidi wawarudishe kwanza kwenye ABC za sheria ili wawe katika nafasi ya kufundishika kivitendo.sijui katika fani zingine lakini ninashaka kwamba tatizo hili litakuwepo.Tuombe Mungu lisiwepo katika fani ya udakitari maana itakuwa hatari sana. Tatizo kubwa ni kwamba baadhi ya vyuo vinajali zaidi biashara kuliko ubora wa elimu. Wakifeli sana utakosa masoko na wakifaulu sana utakuwa kimbilio la wateja wengi. Serikali iangalie hili litakuja kututia aibu. Utapeleka wakili katika soko la Afrika Mashariki hajui hata kudraft Plaint na matokeo yake wataajiliwa kama makarani katika maofisi ya mawakili wa kikenya na kinyarwanda
   
 15. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #15
  Feb 6, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Labda wakiwa wengi gharama zao zitapungua
   
 16. d

  damn JF-Expert Member

  #16
  Feb 7, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 585
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  na rushwa kuongezeka mahakamani
   
 17. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #17
  Feb 8, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Ni kweli mawakili wakiwa wengi gharama zinaweza kupungua. Lakini kama uwingi ni bora kuwa wengi tu bila kujali kiwango kuna hatari ya mtu kulipa gharama ndogo kwa huduma hewa. Kama wakili hatakuwa hajafikia kiwango cha uelewa kinachotakiwa itakuwa vigumu kutoa huduma inayotakiwa. Matokeo yake unaweza kujikuta unakwepa gharama kubwa huku unapoteza haki yako. Badala ya kupata haki-gharama kubwa unakosa haki + gharama ndogo.
   
 18. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #18
  Feb 8, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Sioni shida hata wangekuwa mkupuo mmoja 10,000 as long wamekuwa well trained/educated na wamefaulu hiyo Bar Exam.
   
 19. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #19
  Feb 9, 2011
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Itakuwa kama shule za kata na matokeo ya mtihani wa kidatu cha nne
   
 20. Sita Sita

  Sita Sita JF-Expert Member

  #20
  Feb 9, 2011
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 1,196
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  The problem is not the Number (Quantity)

  Hata kama wakiapishwa 1000, Majority watabaki in Big Cities like DSM, Ars, Mwz and Mby

  Lets look at Ubora wa Mawakili wa Serikali and Not hawa private lawyers


  Ni kesi ngapi wanasimamia na ni asilimia ngapi kati ya kesi hizo wameweza kushinda.


  Mwenye takwimu tafadhali.

  I dont think kama kuna lawyer anayeamua kushndwa unless there is corruption involved
   
Loading...