Nini hatima ya kanisa la Mlima wa moto A.G baada ya Mama Getrude Lwakatare (Mchungaji na mbunge) kufariki dunia?

Ni wengi ambao wangetaka kupata majibu yake lakini kidogo corona inawaweka busy..

Kiasili Mama Getrude sio Mhaya kama wengi wanavyodhani... Huyu ni Mpogoro wa Morogoro Ifakara huko... Mumewe ambaye pia ni marehemu ndio Mhaya wa Bukoba Kanyigo nadhani...

Kupanda kimafanikio kwa Mama Getrude kunaanzia miaka ile ya 2000 alipofungua shule ya kwanza ya mkondo wa kiingereza Tabata karibu na mawenzi akiwa na mshirika wake mmoja anayesemekana ni mnaija

Shule iliitwa St. Mary's English medium academy ikafanya vizuri na kupanuka kwa haraka hata kuwa na matawi... Huyu mnaija ndio alimpa connection ya Marekani ambapo alipewa mbinu ya kusema zaidi ya kuwa na shule lakini pia anajihusisha na watoto yatima ambao hawa husoma bure kwenye shule yake.

Wazungu wakahadaika na kummwagia fungu la maana ambapo alijenga shule kubwa huko huko Tabata bima nadhani

Ili kuwaaminisha wazungu akachukua kweli wachache na kuwaingiza kwenye shule yake.. Na akawa anawapiga picha pamoja na wanafunzi wengine na kuzituma ulaya... Kwa mbinu ya kwamba wote hao ni yatima.. Waliosoma St Mary's miaka ile ni mashuhuda wa hili

Shule zikachanganya sana kwakuwa tayari alikuwa na ufadhili wa wazungu lakini vile vile akaenda Kenya na kuwachukua Vijana wa Kikenya kibao ambao ni graduates. Hawa wakaletwa kufundisha lugha ya kiingereza na shule zikaongezeka na kupata mafanikio makubwa

Katikati ya mafanikio makubwa zikaanza skendo na tuhuma za Walimu wake kutokuwa na vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini. Walimu wake wengi kutokuwa na vigezo hafifu vya kuwa walimu. Wanafunzi kuwa na uwezo mdogo kwenye masomo mengine tuhuma za kuiba mitihani.

Siku ambayo serikali imejiandaa kwenda kufanya ambush mama akawa ameshatonywa na hivyo kuwakimbiza walimu wote Wakenya kwa mabus ya kukodi mpaka mpakani.. Ushahidi ukakosekana lakini shule zikayumba sana kwa sababu ya kudhibitiwa na serikali kwenye swala la ajira ya walimu

Hilo lilienda sambamba na wafadhili kupata taarifa kuwa yatima wanaowachangia kila wakati sehemu kubwa ni uongo hivyo wakakata kamba

Kipindi hicho ndio mama alipoona awekeze zaidi kwenye kituo chake cha maombi kilichokuja kuwa kanisa kubwa la Assemblies of God Mikocheni Mlima wa moto.

Huku kwenye kanisa ufuatiliaji wa serikali haukuwa mkubwa kama kwenye shule na hata running cost zilikuwa chini sana kulingananisha na kwenye elimu.

Income ya kanisa ikawa super na inayopatikana kwa wepesi kuliko kwenye shule zake... Hivyo akapunguza nguvu kwenye shule na kuwekeza zaidi kwenye dini.

Dini ikamkuza na kumfanya awe maarufu maradufu huku akiwa ni mmojawapo wa wafadhili na mwanachama matiifu wa CCM.. Hili lilimpelekea kupewa ubunge wa kuteuliwa.. Kwahiyo sasa akawa sio mama Getrude Mchungaji tuu bali na mheshimiwa mbunge pia... Akawa sasa ametimiza cycle ya msingi ya matamanio ya binadamu wengi

  • Umaarufu
  • Utajiri
  • Heshima
  • Fame, wealth and respect (status)

Sehemu ya pili
Kwenye maisha yake ya kutafuta alikuwa na nyakati ngumu pia na mojawapo kazi ya hizo ni kutengana na mumewe Mzee Lwakatare. Kugombana na mshirika wake kibiashara kwenye shule kusitishiwa misaada ya watoto yatima.

Kuzuiwa kuajiri walimu wageni. Kuingia kwenye kashfa ya kununua kiwanga cha Mangula Moro kilichokuwa na eneo kubwa sana na kubalidili matumizi yake huku mashine akiziuza chuma chakavu.

Umaarufu wa kanisa lake ukawavutia na matajiri wengine walioficha maovu yao kwa mlango wa dini... Mmoja wao ni mmiliki wa vituo vya mafuta vya Victoria service stations.. Huyu jamaa mwenye background isiyovutia sana hasa nchini Kenya alianzisha kanisa lake pale Victoria lakini baadae akaja akaunda ushirika na mama Getrude Lwakatare.. Na mara nyingi huonekana kwenye ibada za mlima wa moto kwenye vile vipi MUHIMU

Mama Mchungaji Getrude Lwakatare mbunge inasemekana ana mtoto mmoja wa kiume. Mama ni mjasiriamali na tunaweza kusema ni mwekezaji pia akiwa na vitega uchumi lukuki
Katika uwekezaji wake kuna

Shule za St Mary's
  • Kuna kituo cha radio (sina hakika na TV online)
  • Ana kanisa la Mlima wa moto
  • Ana viwanja na ardhi sehemu tofauti tofauti
  • Ana uwekezaji mwingine usiojulikana na wengi
  • Sehemu kubwa ya uwekezaji wake kwa sasa ana shareholders lakini je vipi pale mlima wa moto alipokuwa amewekeza mpaka moyo wake?
Je, alikuwa na shirika na mtu/ watu wengine?

Je, huyo mtu/hao watu wana maono kama yake?
Je, nafasi ya wanae ni ipi pale mlima wa moto
Huko kwingine je.. Kaweka vizuri kwenye ishu za mikataba ya biashara, umiliki na mirathi?

Mlima wa moto ilikuwa ni taasisi binafsi je ni nani ataweza kuvaa viatu vya mama? Mtoto ataweza?
Mwisho wa yote tunabaki na swali moja muhimu.

Je, ni nini hatima ya kanisa la Mlima wa moto baada ya Mama Getrude Lwakatare mbunge na Mchungaji baada ya kufariki dunia?

Wakati utasema.. Si muda wa kuanza ramli chonganishi.

Jr

Jr
Mama alikuwa tapeli sana yule, aliwalaghai watu kwa jina la dini huku akiwasaliti na wajinga wakamuona ni malaika kumbe ni msanii tu. Walichome moto tu lile kanisa halina manufa yeyote kwetu.
 
Mama alikuwa tapeli sana yule, aliwalaghai watu kwa jina la dini huku akiwasaliti na wajinga wakamuona ni malaika kumbe ni msanii tu. Walichome moto tu lile kanisa halina manufa yeyote kwetu.
Walichome moto tu lile kanisa halina manufa yeyote kwetu.
 
.
 
Attachments

  • IMG-20221117-WA0014.jpg
    IMG-20221117-WA0014.jpg
    33.4 KB · Views: 6
Je, nafasi ya wanae ni ipi pale mlima wa moto
Huko kwingine je.. Kaweka vizuri kwenye ishu za mikataba ya biashara, umiliki na mirathi?

Mlima wa moto ilikuwa ni taasisi binafsi je ni nani ataweza kuvaa viatu vya mama? Mtoto ataweza?
Mwisho wa yote tunabaki na swali moja muhimu.
 
Sio kupotea huyo jamaa huwa anakodi hotel anajifungia anakula ngada ana sizi humo hata even week kula poda.. kwa hio mara nying ndugu zake huwa wana track simu yake wanaenda mchukua
 
Kwa kifupi ni kuwa asili ya neno hili (Walokole) ni uganda ( baganda) na wao walikuwa wanalitumia mwanzoni mwa miaka ya 1940,50 hadi 60 wakiwaita waumini wenye msimamo mkali wa kikatoliki (karismatiki) kwa wakati huo.Hao wakarismatiki walikuwa wanajiita abalokole liliwa na maana watu waliokoka au ongoka kama lilivyokuwa linatumiwa na wakatoliki wa watanzania miaka hiyo hiyo.Na walikuwa na salam zao wakikutana wanasalimiana kwa kugonganisha vifua na kuruka juu baada ya kugonganisha hivyo vifua.Wanawake walikuwa wanavaa magauni marefu sana hadi chini na walikuwa wanafunika vichwa vyao kwa vilemba vyeupe.
Kitu kimoja noticable kwa jamii hii ni kuwa walikuwa hawapendi kufanya kazi ila wala kujishughulika na kutafuta mali wakiamini kuwa hayo ni mambo ya ulimwengu.hali hiyo ilipelekea wengi kuwa maskini sana kiasi cha kuwa wahitaji wakubwa.Muda mwingi waliutumia kushuhudiana wao kwa shuhuda mbali mbali na walipenda kutumia neno kutendeleza wakati wakikutana kwenye kitu kinaitwa faragha.
So jamii hii ilikuwa kwa kasi sana hata watu wengine wa afrika ya mashariki hasa Tanzania waliojitangaza kuokoka waliitwa "walokole" na jamii ya wasioamini.Lakini ikumbukwe kuwa jamii hiyo ya wasioamini iliwaita hivyo kama kwa namna flani ya kuwadharau na kuwakebehi.Hivyo basi kila aliyeokoka miaka hiyo ya 50,60,70 hadi 80 aliitwa "mlokole" kwa kebehi ya wale wasioamini.Waliwaita hivyo wakiwafananisha na jamii hiyo ya wakarismatiki wa uganda ambao walipata sana.
C&P
TUMTENDELEZE wapi Omumyoto?
 
Sio kupotea huyo jamaa huwa anakodi hotel anajifungia anakula ngada ana sizi humo hata even week kula poda.. kwa hio mara nying ndugu zake huwa wana track simu yake wanaenda mchukua
Seriously!?
 
Mlima wa moto ilikuwa ni taasisi binafsi je ni nani ataweza kuvaa viatu vya mama? Mtoto ataweza?
Mwisho wa yote tunabaki na swali moja muhimu.

Je, ni nini hatima ya kanisa la Mlima wa moto baada ya Mama Getrude Lwakatare mbunge na Mchungaji baada ya kufariki dunia?

Wakati utasema.. Si muda wa kuanza ramli chonganishi.
 
Mlima wa moto ilikuwa ni taasisi binafsi je ni nani ataweza kuvaa viatu vya mama? Mtoto ataweza?
Mwisho wa yote tunabaki na swali moja muhimu.

Je, ni nini hatima ya kanisa la Mlima wa moto baada ya Mama Getrude Lwakatare mbunge na Mchungaji baada ya kufariki dunia?

Wakati utasema.. Si muda wa kuanza ramli chonganishi.
Lipo linaendelea kashika binti yake
 
Back
Top Bottom