Nini Hasara na Faida ya kutundika Picha Mtandaoni?

LINCOLINMTZA

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2011
Posts
1,639
Reaction score
519
Hey wana JF!
Kuna tabia naona inakuwa kabisa ya watu kuweka picha zao kwenye mtandao. Baadhi ya picha zinaonyesha watu wakiwa smart katika mapozi mbalimbali, tata na ya kawaida. Hii naiona kwa akina dada na akina kaka.

Nini lengo la kuweka picha hizi mitandaoni?
Nini hasara na faida ya kutundika hizi picha hasa kwenye uso wa kitabu?
Naomba tuelimishana kwani mimi binafsi sipendelei kabisa.
 
Naona wanatafuta umaarufu tu, kama sio masifa.
 
Usichopenda wewe wengine wanapenda, kwanza picha mtandaoni haiwezi kupotea, na nikuulize kati ya wewe na Rais bora nani? mbona Marais na matajili wote picha zao mitandaoni zipo? sembuse wewe takataka tu ambaye hata mtaani kwako hujurikani?
Ptuuuuuuuuu!!
 
Kwenye red nimekuelewa. Ni kame e-Photo Album.
Kwenye blue naona tofauti kubwa ya uwezo wa kufikiri kati yako na mimi. Sihitaji kubishana na wewe kwani hujui unachoandika na hunijui na mimi pia.
 
picha ni kumbukumbu lakin kumbukumbu za siku hizi zinatisha kuogopesha. na baadae ni kukudhalisha tu unaweka picha za ngono mtandaoni ili iwe nini?kizuri cha leo ndio kibaya cha kesho.
 
Hey wana JF!
Kuna tabia naona inakuwa kabisa ya watu kuweka picha zao kwenye mtandao. Baadhi ya picha zinaonyesha watu wakiwa smart katika mapozi mbalimbali, tata na ya kawaida. Hii naiona kwa akina dada na akina kaka.

Nini lengo la kuweka picha hizi mitandaoni?
Nini hasara na faida ya kutundika hizi picha hasa kwenye uso wa kitabu?
Naomba tuelimishana kwani mimi binafsi sipendelei kabisa.

ukijibu kwa nini uliweka hiyo "AVATA" yako hapo juu basi utakuwa umepata jibu sahihi juu ya faida na hasara za kuweka picha mtandaaoni.

Kwa sababu unajikontradikiti wewe mwenewe kwa kusema kuwa eti wewe hupendelei kabisa wakati tunaona picha katika avata yako hapo, sasa hupendi nini?
 
Hakuna contradictions mkubwa katika maelezo yangu. Soma zile reds katika post yangu na katika komenti yako zinatofautiana sana, natumaini utaelewa vizuri. Kwa kuongezea: An avatar is an icon, picture or representation of a user (http://answers.yahoo.com).
Halafu hebu jikite kwenye kujibu maswali yaliyopo mbele yetu.
 
Nyingi ni hasara kuliko faida. Mojawapo ya hasara nyingi za kuuza sura ni pamoja na picha yako kuweza kutumiwa kama Identity katika mitandao ya kiuhalifu.
 
Acha kujiogopesha, kwa vitu ambayo uwezekano wake wa kutokea ni 000000.001%
kuna billions of users ambao wanatumia mitandao, inakuwaje picha zao zisichukuliwe wachukue za kwako?
 
Usichopenda wewe wengine wanapenda, kwanza picha mtandaoni haiwezi kupotea, na nikuulize kati ya wewe na Rais bora nani? mbona Marais na matajili wote picha zao mitandaoni zipo? sembuse wewe takataka tu ambaye hata mtaani kwako hujurikani?
Ptuuuuuuuuu!!

hee?!cheo cha mtu sio kigezo cha mtu kuwa bora kuna watu wana thamani kubwa sana na hawana cheo chochote katika dunia hii., mimi tangu nijitambue sipigi picha ovyo three years nilizokaa chuo hata picha za group sikuwahi kupiga.after all public figure inaanzaj kukwepa kupiga picha au zisiwekwe popote?
 
Sioni ubaya wowote ili mradi hiyo/hizo picha haziko kinyume na maadili ya Kitanzania na Kiafrika kwa ujumla.
Kama wewe huna tatizo na watu ama jamii au serikali unaogopa nini, mfano wewe sio mwizi, si jambazi, sio malaya, sio kibaka nk, kwa nini uogope kuwa na picha kwenye mtandao.

Ila tunatofautiana kimtazamo na kifikra na ndio maendeleo sometimes
 
Uweke ili iweje?tena siku hizi wana mtindo wa kupiga picha chooni na kutundika mtandaoni madai yao eti zatoka vizuri.
 
Si watu wakuone, mbona zamani ukipita nyumba nyingi utakuta wametundika picha zao masebuleni, siku ukiwatembelea unaanza onyeshwa huyu bibi, babu hapa nilikuwa kagera vitani. Na siku zile tulikuwa tunatembeleana sana. Sasa hivi mawasiliano ni kwenye mtandao so kila kitu ni digital ukitaka kumuona babu yangu utamuona kwa mtandao, ukinikumbuka sana ingia kwenye fb utaniona na utafurahi, nadhani lengo ni kama lile la kuweka ukutani sebuleni!
 
Ni vizuri tukaelimishana kwa faida ya wengi kwani matumizi ya mtandao nchini kwetu ni mageni sana.
 
Hey wana JF!
Kuna tabia naona inakuwa kabisa ya watu kuweka picha zao kwenye mtandao. Baadhi ya picha zinaonyesha watu wakiwa smart katika mapozi mbalimbali, tata na ya kawaida. Hii naiona kwa akina dada na akina kaka.
Nini lengo la kuweka picha hizi mitandaoni?
Nini hasara na faida ya kutundika hizi picha hasa kwenye uso wa kitabu?
Naomba tuelimishana kwani mimi binafsi sipendelei kabisa.
wanawake kupata mabwana wengi na wavulana kupata wa kuwalea
 
Si watu wakuone, mbona zamani ukipita nyumba nyingi utakuta wametundika picha zao masebuleni, siku ukiwatembelea unaanza onyeshwa huyu bibi, babu hapa nilikuwa kagera vitani. Na siku zile tulikuwa tunatembeleana sana. Sasa hivi mawasiliano ni kwenye mtandao so kila kitu ni digital ukitaka kumuona babu yangu utamuona kwa mtandao, ukinikumbuka sana ingia kwenye fb utaniona na utafurahi, nadhani lengo ni kama lile la kuweka ukutani sebuleni!

Miaka ya nyuma mtu alikuwa hawezi kuchukua picha ya mtu iliyotundikwa sebuleni bila ya idhini ya mhusika. Siku hizi ni tofauti.

avatar2885_3.gif
 
Inategemea ni picha za aina gani na unazitumiaje.. Kama unajiamini kuwa hauna tatizo ktk jamii uliyopo why uogope? Faida ni utambulisho kwa wengine. Hasara zitatokana na vile unavyotumia hzo picha.
 
Back
Top Bottom