Nini hasa Siri ya Namba 3 - Umaarufu wa Namba 3 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini hasa Siri ya Namba 3 - Umaarufu wa Namba 3

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mkaa Mweupe, Mar 3, 2009.

 1. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Waungwana naomba niilete hoja hii hapa jamvini ili tupate kuijadili.

  Nimekuwa nikiwaza kwa muda mrefu sana juu ya kwanini haswa namba tatu (3). Kwani hii namba imekuwa na umaarufu wa pekee kati ya namba nyingine zilizosalia yaani 0, 1, 2,..., 4, 5, 6, 7, 8, 9.

  Nianzie huu umaarufu wa namba tatu kwenye mahesabu.

  1. Wataalam wanatuambia ya kwamba tunaweka koma baada ya tarakimu tatu. mfano elfu moja = 1,000; elfu kumi = 10,000; laki moja = 100,000; bilioni moja = 1,000,000,000 n.k.
  2. Hawa wataalamu wanatueleza ya kwamba, umbo ambalo ni imara zaidi ni pembe tatu, ndio maana mapaa mengi huwa na umbo hilo.

  Umaarufu huu haukuishia kwenye hesabu, unaendelea kwenye nyanja nyingine
  1. Hamna mgonjwa aliyewahi pewa dawa yenye dozi zaidi ya kutwa mara tatu.
  2. Kila mtu anatakiwa kujitambulisha kwa majina matatu.
  3. Waamini fulani wanaamini kuwa Mungu ana nafsi tatu.
  4. Wakati wa mateso ya Yesu, alianguka mara tatu.
  5. Yesu alisulubiwa na watu wengine wawili na hiyo kufanya idadi ya waliosulubiwa kuwa ni watatu.
  6. Imani hii inaendelea kwamba alifufuka siku ya tatu ilivyoandikwa.
  7. Jiko imara lina mawe au maegemeo matatu; angalia hata jiko la mchina na la gesi.
  8. Kabla ya kuanza riadha inahesabiwa moja mpaka tatu.
  9. Katika mashindano wanaong'ara ni mshindi wa kwanza, wapili na watatu.
  10. Waamini wengine kabla ya ibada lazima wajisafishe mara tatu.
  11. Mambo makuu kwa kila kiumbe hai ni kula kuny... na kulala.
  Nadhani haya yote yanatokana na kuwa ulimwengu huu unamazingira ya kuishi ya aina tatu; majini, ardhini na angani.

  Naomba kuwasilisha
   
  Last edited: Mar 3, 2009
 2. Rainbow

  Rainbow Member

  #2
  Mar 3, 2009
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na ktk lugha kadhaa namba hiyo huanza kwa herufi T. Tatu, three, trois, tiin, thalatha, ...
   
 3. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Ajabu nyingine ni kwamba hata hiyo T ina ncha tatu
   
 4. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,165
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana nanyi nyote, hata hivyo nchi yetu nayo ina viongozi wakuu watatu wa Kitaifa. JK, Shein na Pinda
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  Mar 7, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  I’m sure that I will always be
  A lonely number like root three

  The three is all that’s good and right,
  Why must my three keep out of sight
  Beneath the vicious square root sign,
  I wish instead I were a nine

  For nine could thwart this evil trick,
  with just some quick arithmetic

  I know I’ll never see the sun, as 1.7321
  Such is my reality, a sad irrationality

  When hark! What is this I see,
  Another square root of a three

  As quietly co-waltzing by,
  Together now we multiply
  To form a number we prefer,
  Rejoicing as an integer

  We break free from our mortal bonds
  With the wave of magic wands

  Our square root signs become unglued
  Your love for me has been renewed
   
 6. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  nami nitakuja zaa watoto 3
   
Loading...