Nini hasa maana ya utu?

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
WanaJF,

Jana kuna MwanaJF alianzisha thread akilalamika kuwa Mbunge wake wa Arumeru Mashariki ni mgonjwa sana na hivyo hawana mwakilishi jimboni kwao. Alitaka kujua serikali inaonaje kama Wana-Arumeru wakifanya uchaguzi mwingine ili wapate muwakilishi mwingine. Kwenye ile thread wapo waliosema kuwa wakati mwingine tuweke utu mbele, thamani ya mtu ni utu, ubinaadamu ndio unatangulia na mengine yote yanafuatia. Wengine wakasema kuwa suala sio kubeza ugonjwa wa Mbunge bali ni uwakilishi wa wanajimbo la Arumeru Mashariki full stop.

Pia jana hiyo hiyo, Faiza Foxy alipewa ban ya miaka miwili kwa kwa kutenda kosa dhidi ya UTU ikiwa na maana ya Kukejeli na kubeza marehemu na sababu zilizopelekea kifo chake ni kosa tena kukosa Heshima.

Swali langu ni nini hasa maana ya utu? Ni utu kuendelea kumwacha madarakani kiongozi ambaye ni mgonjwa sana to the extent kuwa hawezi hata kuwawakilisha tena waliomchagua? Je, mtu unaweza kula ban hapa JF kwa kutokuwa na utu? Ni vigezo gani tunavyotumia kujua kama mtu hana utu au amefanya jambo ambalo halina utu?

Nim-quote Gaijin: Utu ndio kitu gani? Utu unau define vipi? Kwa standards za nani? Tunaweza kusemaje nani ana utu zaidi kuliko mwingine kwa kufanya vitendo gani?

MAONI YA WADAU:
-------------
-------------
-------------
-------------
-------------
-------------
-------------
 
Mimi nataka kuanza na msingi kabisa wa neno "utu"

Unapofungua neno "utu" kwenye kamusi linakurejesha kwenye neno mtu ambapo unakutana na definition hii

Utu: Human nature, jumanity, manhood, membership in the human race. Also used to indicate the finer qualities of humanity, i.e gentleness, goodness, & C. mwenye utu, a human, gentle, considerate, kind, person


Sasa kwa tafsiri hiyo ya neno "utu" sielewi unawezaje kwanza kumpiga mtu ban kwa kukosa utu.
 
EMT,

Tuseme kutompokonya mtu cheo chake cha uwakilishi wa wananchi japo hawezi kuwatumikia ni "utu" kwa Mbunge huyo, lakini hawa wananchi tumewafanyia "utu" nao?

Ni "utu" kuwaachia watu katika jimbo wakae zaidi ya mwaka mmoja bila ya mwakilishi wao Bungeni?


Nani ana-define huu "utu"?
 
Reactions: EMT
Mimi nataka kuanza na msingi kabisa wa neno "utu"

Unapofungua neno "utu" kwenye kamusi linakurejesha kwenye neno mtu ambapo unakutana na definition hii

Sasa kwa tafsiri hiyo ya neno "utu" sielewi unawezaje kwanza kumpiga mtu ban kwa kukosa utu.

Katika kutafuta maana halisi ya utu nimekutana na thread moja ya zamani kidogo titled "Ni nini Utamaduni wa Mtanznia" ambapo Azimio Jipya alikuwa anachambua maana ya utu:


"Kwa kina chote kilichowahi kufikiwa ili kujua true value za Mtanzania jibu lilikuja moja. Ni Utu nafikiri kazi kubwa iko kwenye kutafsiri maana ya utu!

Lakini wataalamu wa "elimu ya utu" dhidi ya "elimu ya akili" wanadai kuwa kila binaadamu alizaliwa na thamani inayoitwa UTU na utu unaweza kukuwa (To grow) au kufifia mtu anavyoendelea kuutumia, kuishi na umri kuongezeka. Lakini ukweli ni kuwa ingawa kila mtu anazaliwa na UTU ni wachache wanaulinda, kuukuza, na kuupenda hata kufa nao. Ni Wachache wanakufa wakiwa na UTU. Wengi wanakufa wanyama au karibu na hapo.

Tumbili anaweza kuuliza utu ni nini, lakini sio mtu. Mwanadamu ataulizaje asili yake? Tumbili hakuumbwa kuwa na utu, hivyo anaweza kuushangaa, kuulizia na kutaka kuujua. Mtu anayeuliza maana ya UTU ina maana amesha upoteza..yaani amesha upoteza Utanzania.

Mtanzania ni mtu mwenye utu!

Utu ni character au zaidi unaweza kuwa ni Utamaduni!

Asiye na utu ..ameupoteza Utanzania.

Ni kweli kuna wakati Kiwango cha UTU WA TAIFA LA TANZANIA kilikuwa juu!Hakijawahi kutokea afrika.

Utu Kwenye UONGOZI

Utu kwenye Familia.

Utu kwenye kilimo.

utu kwenye elimu.

Utu kwenye mavazi.

Utu kwnye muziki.

Utu kwenye vyakula

Utu kwenye Biashara

Utu kwenye siasa ya nchi
Utu kwenye mifumo ya kiuchumi ya taifa. Azimio la Arusha? etc

Utu kwenye mahusiano na nchi nyingine

Utu kwenye kuweka mikataba muhimu ya Taifa

Utu ndani ya bunge na wabunge wenyewe!

Utu kwenye sehemu za kazi..(Walikuwa hata na msemo kazi ndi kipimo cha utu)

Utu kwenye muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar

Utu kwenye baraza la Mawaziri

Utu kwenye chaguzi mbalimbali za kitaifa.
Utu kwnye kuwajali wananchi wote kwa pamoja..bila kuwepo kwa matabaka.

Utu kwenye VIONGOZI WASTAAFU WA NGAZI ZA JUU KITAIFA

Utu kwenye kila kitu ilikuwa ndio utamaduni wa Mtanzania. Na Alama za kitaifa zilidhihirisha hivyo. Kauli mbiu mbalimbali zilidhibitisha hivyo..etc

Kujibu swali kuwa UTAMADUNI HUU WA UTU/UTANZANIA unadevelope au ume kwama....Kasi ya kudidimia kwa Utanzania kama utu ni kubwa na inatisha.

Maendeleo bila Utu..? wapi yalishawahi kuonekana hayo? Siasa na uchumi kuwa mikononi mwa viongozi wasio na utu/mafisadi...iyatawezekana vipi?

Kiogozi asiye Mtanzania/asiye na utu anaweza kufanya unyama na kuudhihirisha zadi ya tumbili.

Anaweza kudiriki kuweka saini upande wa kuliangamiza Taifa....badala ya kuweka saini pale pa Kulinda na kutetea Taifa na Maendeleo ya wanachi wake.

Kiongozi asiye na Utu/Fisadi anaweza kuuza Migodi yote ya madili mali ya Taifa kwa robo kilo ya almasi.

Utanzania Ni Utu na Utu umetoweka Tanzania karibu kwenye kila nyanja.

Ndio Maana viongozi wengi waliopo kwenye uongozi wanakufa/watakufa bila UTU! Wanakufa na watakufa wamepoteza asili yao ya kibinaadamu na ya kitanzania.

Swali ..Walizaliwa na UTU Wameupotezea wapi? Ni sahihi kufa kama Mnyama au bila kuwa na heshima ya kiutu?..."

 
Mimi nakubali kuwa miongoni mwa hao waliokwisha kuupoteza utu wao wa asili; hivyo najipa haki ya kuuliza "utu ni nini?" @Azimio jipya

Na ikiwa utu wa taifa umeanza kupotea na wengi wanakufa wakiwa karibu na unyama kuliko utu, utamhukumu vipi mwenzio kwa kukosa utu?
 
Reactions: EMT

Kuna mbunge mmoja huko Kenya alisema kuwa mtu ambaye hana dini hajui utu ni nini. Je, dini inaweza kuwa kigezo cha kujua kama mtu ana utu or at least anajua maana ya utu? Kwamba watu wasio na dini hawana utu?
 
Kuna mbunge mmoja huko Kenya alisema kuwa mtu ambaye hana dini hajui utu ni nini. Je, dini inaweza kuwa kigezo cha kujua kama mtu ana utu or at least anajua maana ya utu? Kwamba watu wasio na dini hawana utu?

Dini ni nini?
 
Reactions: EMT
utu ni kumjali mtu na kumheshimu kila mtu na kuheshimu fikra na mawazo ya kila mtu..

Wakati unajali na kuheshimu fikra za kila mtu, unaruhusiwa kutoa na fikra zako pia japo kama zinakinzana na za hao wengine?
 
Dini ni nini?

Hapo itabidi uwaulize wenye dini. lol. Kwenye kitabu cha Chachage na Cassam titled: African Liberation: The Legacy of Nyerere at page 51 wanasema: "Ujamaa embraced aspects of the Swahili concept of utu or common humanity (or Ubuntu as is called in South Africa). This [utu] is based on the philosophy of forgiveness, reconciliation and willingness to share." Tunaweza ku-define utu kama kusameheana, kusuluhishana na kusaidiana? Japokuwa wapo wengine watasema utu simply mean Uhuru Through Ujamaa. lol
 
katika mazingira ya Ban nadhani walitumia "utu" kwa kumaanisha vitu kama 'compassion, respect for the deceased, support to victims vs oppressors' etc. kumbukeni circumstances za post katika kuisoma Ban yenyewe.

Mnaweza kukaa hapa na kuongelea theoritical concepts kama utu na ubinadam ila kumbukeni kuna watu wanamsiba sasa hivi. nadhani hiyo Ban ni katika kuwasupport hao watu, na kila mtu mwenye kuamini kulikua na 'victim' na kwamba huyo 'victim' anahitaji support.

Kama mnajadili utu kama utu, na haya ya FF mnachukulia kama mfano, ni tofauti na basi nadhani mchango wangu sio wamaana hapa. ila kama mnachukua swala la FF na mnataka kutafuta theory iliotumika/ilitumiwa basi someni mazingira kwanza.
 
lol. tunajaribu tuu kutafuta maana hali ya utu. Tumekuwa tukilitumia hili neno mara nyingi, lakini tunajua maana yake hasa ni nini?
 

Hapo kwenye tafsiri ya [utu] umeruka neno moja muhimu-falsafa.

[utu] kwa mujibu wa Nyerere ni falsafa nzima ya usuluhishi, usamehevu na usaidizi-lol

Ikiwa hiyo ndio definition ya [utu], kwenye kesi ya Mbunge Vs wana jimbo, [utu] unahusikaje?
 
Reactions: EMT
Mwali,
Mwali dhumuni la mada ni kujadili utu kama utu. Ban ya FF nimetoa kama mfano tuu, b'se kigezo chake ni FF kutokuwa na utu. For the avoidance of double ndio maana nilitoa pia mfano wa hali ya uwakilishi ilivyo kwenye jimbo la Arumeru Mashariki. Kwa hito tunaomba mchango wako juu ya utu kama utu. Unaweza kutumia mifano mingine ambayo haimhusishi FF.
 
Hapo kwenye tafsiri ya [utu] umeruka neno moja muhimu-falsafa.

[utu] kwa mujibu wa Nyerere ni falsafa nzima ya usuluhishi, usamehevu na usaidizi-lol

Ikiwa hiyo ndio definition ya [utu], kwenye kesi ya Mbunge Vs wana jimbo, [utu] unahusikaje?

Thanks for the correction. Should have been "This philosophy blal bla bla." Kama tu-apply hiyo definition ya Nyerere kwenye kesi ya Mbunge Vs wana jimbo sijaelewa kama wahusika watakuwa wanasuluhisha nini. Kwani kuumwa kwa mbunge ni kosa kwamba asamehewe?

Hapo kwenye usaidizi labda watakuwa wanamsadia kimapato? Kwa sababu kuumwa kunahitaji matibabu na matibabu yanahitaji fedha? So, wakimwondoa watakuwa hawana utu kwa sababu atakosa fedha za matibabu? But vipi wao hawahitaji usaidizi wa kuwakilishwa?
 
"Ubepari ni unyama, Ujamaa ni utu"-RTD

"Nchi imepoteza utu na heshima yake"-Tanzania Daima

Nchi imepoteza utu na heshima yake!

Interesting article. Naiweka hapa yote.

Nchi imepoteza utu na heshima yake

Na Bakari M Mohamed.

Nchi ni watu; wala si eneo la ardhi, maji na anga linalotanda! Nchi inaundwa na watu wenye mila na dasturi zilizojengwa kwenye misingi ya heshima na utu wa kibinadamu. Tanzania, kama nchi, iliamua kwa dhati yake kuweka misingi ya "kila mtu anastahili heshima ya kuthaminiwa na kutambuliwa utu wake."

Utu na heshima ya binadamu ndio inayoweza kuwatofautisha binadamu na wanyama (hayawani). Binadamu hujitofautisha na mnyama kwa kule kuthamini utu na kutenda matendo yenye heshima mbele ya binadamu wengine kwa jinsi ambavyo yeye (binadamu) anavyotaka athaminiwe kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za kimaumbile.

Hata hivyo, si mara zote watu (binadamu) wanafanya kwa mujibu wa misingi ya utu na heshima ya binadamu. Tanzania ina madadiliko makubwa ya saikolojia ya kisiasa! Kwa kuwa siasa ndiyo maisha yanayoendesha uchumi na jamii sawaiya; na kwa kuwa siasa ndiyo inayoathiri maisha ya watu kwenye kada zote na sekta zote za maisha ya kila siku ya wananchi; kuna haja ya kuyaangalia mabadiliko ya saikolojia ya siasa; chanzo chake; na madhara yanayojitokeza kwenye maisha ya watu ya kila siku.
Hata hivyo, falsafa ya kupotea kwa utu na heshima yetu kuna sababu nyingi na matokeo yake ni mengi pia!

Uchambuzi huu unaandikwa baada ya mwandishi kutafakari matokeo ya kupotea kwa utu na heshima ya wananchi wa Tanzania! Inawezekana msomaji ukadhani kwamba makala haya yamechelewa kuandikwa; na au hata ukadhani kwa nini yameandikwa wakati huu?

Uandishi huu umetokana na wazo (dhana) angavu baada ya ajali mbaya ya kuzama kwa meli (kivuko) yenye jina la "Spice Islander" kilichozama kwenye eneo la Nungwi kisiwani Unguja (Zanzibar) usiku wa kuamkia tarehe 10 Septemba, 2011 (siku ya Jumamosi). Ni msiba wenye huzuni ya kipekee hususan ukiangalia maisha ya usafiri wa bahari kwa kisiwa cha Pemba!

Ukiachailia mbali tukio la Jumamosi (tarehe 10, Septemba 2011) na vifo vya watu zaidi ya mia (100+) waliyekuwamo kwenye meli (kivuko) hiyo; Tanzania imeshapoteza watu wengi kwa ajali za vyombo vya usafiri wa majini na nchi kavu! Kumbukumbu zinaturejesha nyuma zaidi hadi pale ilipozama meli ya "mv Bukoba".

Wapo baadhi ya watu, na kwa nyakati tofauti, wanaodai kwamba, "ajali haina kinga!" Hii ni falsafa iliyozoeleka kwa baadhi ya watu wakidhani kuwa, "kila linalotokea limepangwa na Mwenyezi Mungu; na kutokea kwake ni lazima (wanaita kadari)." Dhana hii inapingana na ukweli kwamba yapo mambo (na au matukio) mengine yanayopangwa na au kusababishwa na au kutekelezwa na watu wenyewe kwa utashi wa nafsi za kifisadi! Tunataja ufisadi hapa kwa vile uharibifu wa nafsi ndio chanzo cha kisaikolojia kinachohusisha akili (ya kishetani) isiyojali mwendo murua (siasa safi) wa kutenda kwa kuzingatia utu na heshima ya binadamu!

Hapa ndipo inaposimamia hoja ya uandishi huu unaousoma! Msongo wa saikolojia ya binadamu wa Tanzania iliyochafuka kwa kukosa utu na kutojali heshima ya utu wake inawafanya watu wengi kuishi kwa jinsi ya kutojali matokeo mabaya (hasi)! Binadamu amechoka na amesongeka na maisha yasiyozingatia siasa murua na amefisidika kisaikolojia! Kama inavyosadifu saikolojia ya watu masikini; kwamba, "wamepoteza haiba ya utu na heshima ya binadamu."

Wengi wa watu masikini wakupitiliza wanafanya chochote pasipokuwa na fikra ya matokeo yake. Na hata wakati mwingine, umasikini uliyopitiliza unawasukuma watu kudhani kwamba: "kufa kufaana; au kufa kupenda!" Wenye vyombo vya usafiri, kama mfano na ukweli ulivyo, hawajali utu! Wengi wanajali faida na masilahi binafsi kuliko utu na uhai wa wengine wanaotumia vyombo hivyo. Huu ni msiba wa kisaikolojia unaohusisha kufa kwa roho (nafsi) ya kibinadamu na kuzaliwa kwa roho (nafsi) chafu ya kishetani isiyozingatia utashi wa utu na heshima ya binadamu.

Kama mfano tu (wala isichukuliwe kama ushahidi wa kimahakama), wenye vyombo vya usafiri hata hufikia kutoa kafara ya damu ya watu kwa imani za "kishirikina" na hata kutafuta jinsi ya kupata faida ya bima kwa ajali za kupanga! Hii ni dhana tu (hata hivyo imeshawahi kutokea kwa nyakati tofauti za miaka mingi nyuma).

Tukiachilia mbali jinsi wafanyabiashara wenye vyombo vya usafiri wanavyoweza kudhani kwamba kwa harakati zao (za kifisadi) za kuweka maslahi binafsi mbele hata kufikia hatua ya kulazimisha matumizi ya vyombo vya usafiri visivyokuwa na viwango kuna kushindwa kwa wajibu wa vyombo vinavyosimamia usalama wa safari ziwe za nchi kavu au za majini.

Ni ukweli kwamba kuna mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu (kama SUMATRA); bado ukweli unaobaki palepale kwamba wanaofanyakazi kwenye taasisi hizo ni binadamu walewale waliyefisidika na kupoteza utu na heshima yao! Kwa sehemu kubwa baadhi yao wanafanyakazi kinyume na utashi wa uhuru, haki na usawa!

Siasa chafu imewachukua kwenye saikolojia iliyovuruga mujtamaa wa akili zao. Kama walivyofisidika kisaikolojia mafisadi wakubwa kwenye mfumo wa siasa ndani ya mzingo wa uongozi wa juu wa serikali na Chama kinachotawala; ndivyo walivyo wale wa chini yao! Wamepoteza utu na heshima yao na hali hii inaonekana kwenye kila sekta ya maisha ya kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Hakuna mtu, kama wapo ni wachache sana wakuhesabika kwa vidole, mwenye huruma na mapenzi ya kuthamini utu na heshima ya binadamu wengine! Kila mmoja na nafsi yake; na ubinafsi umekuwa ndiyo mwendo wa maisha ya kila mtu kivyake! Binadamu wa Tanzania amekuwa hatofautiani sana na wale waliokosa fursa za utu na heshima kwa kufanya kwa vile anataka kufanya bila kutafakari matokeo yake ya sasa na ya baadaye (ya muda mrefu).

Wengi tunaangalia faida ya leo na tunasahau kwamba kesho kuna kuulizwa juu ya nini tulifanya jana na juzi yake. Huu ni mwendo wa maisha yasiyozingatia utashi wa uhuru, haki na usawa wa kimaada, kimaanawi na kiroho. Binadamu wa leo haonyeshi tofauti na mnyama!

Wakati tukio la kuzama kwa "Spice Islander" na taarifa za vifo zinatolewa juu yake; nilijaribu kuzunguka kwenye maeneo ambayo nimezoea kuyatembelea ili kufanya uchunguzi juu ya mguso wa kibinadamu uliyowapata watu wa maeneo mbalimbali (mjini na uswazi)! Hali ilikuwa mchanganyiko; wengi niliowakuta kwenye maeneo tulivu (yenye ustaarabu) walihuzunishwa sana na tukio lile; hakika wengi walikuwa na simanzi na hata kujadili matukio mengine yaliyokwisha tokea, kama vile, Mv Bukoba, Kivuko cha Mto Kilombero, ajali za barabarani za kila mara, na kadhalika!

Hata hivyo, wapo wengine waliyekuwa hawajui lolote juu ya tukio hilo! Niliwakuta wengine wakijishughulisha na shughuli zao; na wengine wakiendelea na starehe zao (kucheza pool na kupata moja moto na moja baridi). Hii ilinikumbusha jambo moja kubwa kwamba ukiachilia mbali habari za kusikia kwenye midomo ya watu; sehemu kubwa ya wananchi wa Tanzania hawasikilizi habari za mara kwa mara (breaking news) kutoka kwenye redio na au runinga (televisheni). Watu wengi wapo "bize" na mambo yao; wanasaka shilingi inayokimbia kwa kasi kwa kuwa "shilingi imeota matairi." Hapa ndipo tulipo; na ndipo tulipofika!

Naandika mtazamo wa kisaikolojia kwa vile wananchi wengi tumepoteza haiba ya utu na heshima wetu, yaani upendo, kujali na huruma! Binadamu tna wajibu wa kiutu kuwa na upendo, huruma na kuwajali watu wengine kwa jinsi ya ubinadamu. Na ndivyo tunavyofundishwa na mafundisho ya asili kwa mujibu wa kanuni za uumbaji (Mwenyezi Mungu ni Upendo; na Upendo unatoka kwa Mwenyezi Mungu). Binadamu tumejisahau na tumepoteza hata saikolojia yetu ya siasa ya kuthamini utu na kuheshimiana! Binadamu tunaonekana kama mbwa mwitu? Hii ni hatari kwa taifa linalojenga watu wake kwa misingi ya kusahau utu na heshima!

Ni kweli umasikini huzaa roho mbaya isiyozingatia utu na heshima. Hata hivyo, kwa nini tumefikia hapa? Na ni nani aliyetufikisha hapa tulipo? Majibu ya masuala haya ni tata (complex) na yanahitaji muda mrefu kuyafanyia utafiti na kudadavua batini iliyomo ndani yake. Tutosheke kwamba utu na heshima imetupotea na sasa tunakwenda ovyo kama alivyowahi kuimba marehemu Marijan Rajab kwenye wimbo wake wa "dunia imani imekwisha." Ni ukweli usiokuwa na shaka kwamba, "kwenye watu kumi binadamu mmoja!"

Angalia zinapotokea ajali za barabarani; ziwe zile zinazotokea kwa kupasuka matairi ambayo yamechakachuliwa (retreading); au zile zinazotokea kwa mwendo kasi usiyozingatia usalama wa barabarani (na ulevi wa madereva); au zile zinazofanywa kwa makusudi ili wamiliki wake wapate bima; zote zinaambatana na utovu wa utu na heshima ya kibinadamu. Ajali nyingi zinazopelekea vifo na majeruhi zimekuwa zikiambatana na matukio ya uporaji wa mali za waliyokufa na manusura! Hili ni somo la kisaikolojia la kujifunza. Ni zao la mabadiliko ya saikolojia ya siasa!

Wanaodai "kufa kufaana" hupata faraja zinapotokea ajali ili kwa munasaba huo waweze kupora mali za abiria. Na hata wengine wamefikia hatua ya kutega mawe na au kuharibu (kuchimba mashimo) barabarani ili kusababisha ajali na hatimaye wapate manufaa ya kifisadi kwa kupora na au kuiba mali zilizomo kwenye vyombo vya usafiri kama fedha, bidhaa na nguo za abiria. Inastaajabisha kuona hata pale inapotokea ajali imesababisha vifo na majeruhi wengi badala ya kutoa huduma ya kwanza kwa manusura; binadamu (aliyefisidika kisaikolojia) huanza uporaji hata wakati mwingine kuwamalizia manusura katika kufanikisha uporaji! Hii ni laana au ndiyo kupotea kwa utu na heshima yetu?

Tumefikishwa hapa! Watu hatuthaminiani na hatujithamini tena. Inasikitisha pale zamani tulipokuwa tunafuata maelekezo na au tahadhari juu ya kulinda na kuhifadhi utu na heshima yetu. Tulikuwa tunafundishwa kuweka tahadhari dhidi ya kutokea kwa majanga na au ajali zinazoweza kuzuilika. Tuliweka utaratibu wa kuogopa ajali; na tulisisitiza kwamba, "kinga ni bora kuliko tiba." Tuliwafundisha wanafunzi (watoto wa shule) na watu wazima juu ya hatari mbalimbali na hata tuliweka matangazo ya tahadhari kwenye maeneo yote yenye hatari na tukaandika (HATARI/DANGER).

Kama mfano (wa kweli), angalia gari la mafuta ya petroli linapopata ajali! Watu badala ya kuchukua tahadhari ya kuokoa maisha yao; wanakimbilia kuchota (kuiba) mafuta bila ya kujali kuwa mafuta ya petroli ni hatari na yanaweza kulipukia mara moja! Hii imetokea Tanzania na kuuwa watu zaidi ya mara moja; bado wananchi wanasubiri malori ya mafuta ya petroli yapinduke (kwenye maeneo yao) ili wao wapone kwa kuchota (kuiba) mafuta! Hapa ndipo alipofika Mtanzania; ndipo alipojifikisha na alipofikishwa; sijui kama atatoka!

Suala la mjadala wa kutoka na au kubaki kwenye msongo wa saikolojia ya siasa iliyofisidika ni kurudi kwenye historia; na si kuirudisha historia nyuma ya wakati, hasha! Tumeshafika hapa tulipo kwenye kudhani kwamba "kufa kufaana" na "fedha mbele" hata tukaacha utu na heshima ya kuthamini utu wetu. Wananchi tumeweka tamaa mbele hata kuacha misingi ya upendo, huruma na kuwajali watu wengine; tumefisidika kisaikolojia na tumekuwa waasi wa nafsi zetu! Hakuna anayemjali mtu mwingine kwa uhuru, haki na usawa; watu wanatafuta faida ya kibinafsi zaidi kuliko faida ya umma!

Wakati ajali mbaya ya "Spice Islander" ilipotokea na Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa - Zanzibar, Dakta Ali Mohamed Shein alipotangaza siku tatu za maombolezo; na hata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete kukatisha ziara yake ya Canada na kutangaza siku tatu za maombolezo (kama ilivyofanywa kwa SUK) hali ilikuwa tofauti. Nilishangaa sana, kwa siku ileile ya tukio (yaani Jumamosi tarehe 10, Septemba 2011) kusikia baadhi ya redio zikipiga muziki wa burudani! Hata maeneo ninayoishi, kwa kuwa ilikuwa ni Jumamosi (siku ya starehe), kulikesha muziki (maarufu kama kigodoro) usiku kucha! Hivi ndivyo tunavyoishi; na haya ndiyo maisha yetu.

Huku wanalia na kuomboleza kule wanaserebuka na kufurahia maisha (starehe kwenda mbele). Inawezekana sana kwamba maisha ni kuiga; na anayeishi kwa jinsi ya kuiga ana kigezo cha kuigiza, siyo? Uongozi wa kisiasa wa maeneo ya wananchi kwenye mitaa (vitongoji), kata (vijiji), tarafa, wilaya na miji wameacha maisha yaende kama watu watakavyo! Sehemu ya sheria ndogo na au hata sheria za nchi hazisimamiwi ipasavyo; sehemu ya watu wanafanya watakavyo na au wapendavyo!

Huu ni msiba wa kitaifa; na kama taifa tuna kila sababu ya kuchukua tahadhari ya mapema kurekebisha hali hii kinyume chake tunaweza kuifanya nchi ikawa mahala hatari kwa maisha ya binadamu mwenye kuhitaji maisha ya utu na heshima ya binadamu kwa kuzingatia utashi wa kimaumbile kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za kimaumbile.

Serikali ina wajibu usioepukika wa kuhakikisha inasimamia misingi ya utu bora na kuweka mkazo kwenye saikolojia ya siasa inayozingatia utu na heshima ya binadamu. Binadamu anahitaji kutambuliwa utu wake na heshima ya ubinadamu wake haiwezi kununuliwa kwa gharama ya faida ya watu wachache wenye roho mbaya na uchu wa utajiri. Tupige vita umasikini kwa nguvu zetu zote! Ni wajibu kwa kila mtu mahali alipo kuhakikisha kwamba mabadiliko hasi ya saikolojia ya siasa hayatumiki kuongeza umasikini. Tuepuke matumizi ya nguvu kubwa ya kifisadi katika kujenga ubinafsi na kubomoa misingi ya umoja, upendo, huruma na thamani ya utu wetu.

Umasikini wa watu usitumike katika kuchochea uasi wa nafsi na kujenga chuki miongoni mwa walalahoi na kuzalisha taifa lenye uadui baina ya watu wenye hali tofauti za maisha. Sisi sote ni ndugu wa damu moja; na tuishi kwa umoja, tukipendana na kuthaminiana kama watoto wa mama mmoja (Tanzania). Mungu ibariki Tanzania; na awalaze marehemu wote waliofariki kwenye ajali ya "Spice Islander" mahala penye stahili zao; na uwape manusura wote nafuu ya haraka, amina!

Source: Nchi imepoteza utu na heshima yake!
 
Alinishangaza sana alipodai kuwa kina mama wajawazito huko Mbeya wapigwe mabomu ili watoto machizi wazaliwe, pia akidai ni sawa wananchi hapo wakiendelea kuuwawa na polisi hao wanyama.

EMT mtu anayekuwa ana mtizamo ya kinyama hana utu.
Utu ni neno lililotokana na mtu.

Utu ni ku act kama mtu,ni sawa na binadamu na ubinadamu...Mtu pasipo utu si mtu.

Hopefully imesaidia...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…