Nini hasa falsafa ya Rais Samia

Nini hasa falsafa ya Rais Samia

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
15,811
Reaction score
36,114
Kila awamu za utawala wa Rais una falsafa zake za kiuchumi
Ila Kwa Sasa naona tunajiendea kama ng'ombe anapelekwa Vingunguti machinjioni

1 Mwalimu JK Nyerere_ Ujamaa na kujitegemea
Nyerere ndo Rais wa awamu ya Kwa kwanza alipokea Taifa likiwa changa kutoka Kwa mkoloni
Falsafa yake ilikuwa Ujamaa na kujitegemea
Hapa alianzisha mashamba makubwa, viwanda vingi vya ngozi na nguo, maduka na vijiji vya ujamaa
Na Kwa kiasi kikubwa alifanikiwa

2 Ali Hasan Mwinyi _ Ruksa
Huyu aliamua kufungua nchi, na kuruhusu biashara huria
Hapa viwanda binafsi, export iliongezeka
Kwangu Mimi binafsi Mzee Mwinyi ndo Rais Bora kuwahi kutokea Tanzania

3 Benjamini Mkapa_ Ubinafshaji na uwezekezaji
"Mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe"
Huyu Rais alikuza sekta ya uwekezaji ambapo Kwa sera zake aliwashawishi wawekezaji wengi kuleta mitaji Yao na kuwekeza TANZANIA
Hii iliinua Uchumi wa Taifa na Kwa mtu mmoja mmoja Kwa kuwapa vijana ajira

4 Jakaya Kiwete_ Kilimo kwanza na Big Results now BRN
Kikwete aliamini kwakuwa kilimo ndo uti wa mgongo wa Tanzania na kilimo kimeajiri zaidi ya 80%
Hivyo alitoka ruzuku katika vifaa na pembejeo kama mbolea na mbegu imara
Hapa wakulima walifaidi
Tukumbuke mchango wa Kikwete katika ujenzi na kutupa cha afya kila kata

5. John Pombe Magufuli _ Hapa kazi tu/ uchumi wa Viwanda
Magufuli licha ya kuwa alikuwa na madhaifu lukuki lakini alijaribu Kwa kipindi alichokuwa madarakani
Alihimiza viwanda vikubwa, vya kati na vidogo
Aliamini katika miundo mbinu kama umeme rejea mradi wa mkubwa Rufiji na umeme wa REA ni matunda yake
Miundo mbinu ya barabara Tanroad alijenga km nyingi
Madaraja n.k

6 Samia Suluhu Hasan_ kazi iendelee
Hapa ni kama tumesimama au tunarudi nyuma
Kazi haziendi
Viwanda vimekufa
Madaraja yanakatika
ATCL imepata hasara kubwa
Ziwa victoria hakuna meli
Bandari imeuzwa
Deni la Taifa ni trillion 97.35
 
downloadfile-18.jpg
 
Falsafa za nini!?..zilisaidia nini!?..maadam gdp inapanda,food security 120%,shule zipo,vyuo mikopo mwamwamwaa basi wacha tusonge, nyerere alikua na falsafa nyingi mara siasa ni kilimo,kilimo cha kufa na kupona lakini bado mkulima alikua duni
 
We ni mgeni hapa Tanzania?
 
Kila awamu za utawala wa Rais una falsafa zake za kiuchumi
Ila Kwa Sasa naona tunajiendea kama ng'ombe anapelekwa Vingunguti machinjioni

1 Mwalimu JK Nyerere_ Ujamaa na kujitegemea
Nyerere ndo Rais wa awamu ya Kwa kwanza alipokea Taifa likiwa changa kutoka Kwa mkoloni
Falsafa yake ilikuwa Ujamaa na kujitegemea
Hapa alianzisha mashamba makubwa, viwanda vingi vya ngozi na nguo, maduka na vijiji vya ujamaa
Na Kwa kiasi kikubwa alifanikiwa

2 Ali Hasan Mwinyi _ Ruksa
Huyu aliamua kufungua nchi, na kuruhusu biashara huria
Hapa viwanda binafsi, export iliongezeka
Kwangu Mimi binafsi Mzee Mwinyi ndo Rais Bora kuwahi kutokea Tanzania

3 Benjamini Mkapa_ Ubinafshaji na uwezekezaji
"Mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe"
Huyu Rais alikuza sekta ya uwekezaji ambapo Kwa sera zake aliwashawishi wawekezaji wengi kuleta mitaji Yao na kuwekeza TANZANIA
Hii iliinua Uchumi wa Taifa na Kwa mtu mmoja mmoja Kwa kuwapa vijana ajira

4 Jakaya Kiwete_ Kilimo kwanza na Big Results now BRN
Kikwete aliamini kwakuwa kilimo ndo uti wa mgongo wa Tanzania na kilimo kimeajiri zaidi ya 80%
Hivyo alitoka ruzuku katika vifaa na pembejeo kama mbolea na mbegu imara
Hapa wakulima walifaidi
Tukumbuke mchango wa Kikwete katika ujenzi na kutupa cha afya kila kata

5. John Pombe Magufuli _ Hapa kazi tu/ uchumi wa Viwanda
Magufuli licha ya kuwa alikuwa na madhaifu lukuki lakini alijaribu Kwa kipindi alichokuwa madarakani
Alihimiza viwanda vikubwa, vya kati na vidogo
Aliamini katika miundo mbinu kama umeme rejea mradi wa mkubwa Rufiji na umeme wa REA ni matunda yake
Miundo mbinu ya barabara Tanroad alijenga km nyingi
Madaraja n.k

6 Samia Suluhu Hasan_ kazi iendelee
Hapa ni kama tumesimama au tunarudi nyuma
Kazi haziendi
Viwanda vimekufa
Madaraja yanakatika
ATCL imepata hasara kubwa
Ziwa victoria hakuna meli
Bandari imeuzwa
Deni la Taifa ni trillion 97.35
Nani alikwambia ana falsafa?
 
Back
Top Bottom