Nini Faida ya u fake katika maisha?

Nini Faida ya u fake katika maisha?

ungetumia busara2 kuachana nae kimyakimyaaaa.,..
umeshaharibu then baadae ndo unamblock na kufuta mawasliano nae
na kumpotezea,...umeharibu dada seriously
hukuwa fair
ndoa na iheshimiwe na watu wote,....we ulipojua anamke nini kilikupelekea utafute had namba ya wife wake wakat
ulichotafta tyr ulijua kuwa ameoa had kumtafta mkewe hukujua effect zake,...#
umeharibu dada
 
Wakuu habarini za jumapili.
Leo napenda kuzungumzia suala la mtu ku pretend na kutaka kuonekana katika jamii kwamba ni mtu fulani smart lakini anachokionyesha yeye hayuko hivo hata kidogo .
Suala hili lipo sana hapa jf na mtaani yamkini. Na huu ufake unapelekwa hadi kwenye mahusiano. Kwanini usiwe wewe halisi? Wapungukiwa nini? Ya nini kujitia mzigo kwa sababu mwisho wa siku hutoweza ku maintain hizo dramas kwa muda mrefu wenye upeo watakuumbua tu.
Kisa kamili. .....
Niliwahi kutafuta rafiki hapa jf na kwa bahati nzuri niliwapata wengi kisha nikafanya uchambuzi yakinifu nikaibuka na mchumba hapa .
Ukaribu wangu na jf ingawa sichangii sana mada nimekuwa msomaji zaidi kutokana na ukulima wangu unaniweka busy sana lakini nimeweza kufahamiana na wadau wengi humu nje ya jukwaa lkn ni members wa jf.
Katika kuwafahamu na kuwasoma nimegundua ufake mwingi sana kwa wanajamii humu ndani. Anyway ni fantasy zao no objection.
Ila kinachonipelekea leo nilete mada ni juu ya wale ma fake kiasi cha kumshirikisha hata Mungu ku justify ubazazi wao. Hapo nawachoka kabisa yaani.
Yaani unamkuta mtu anajipambanua humu ndani kuwa ni bonge la mcha Mungu na anaandika vitu full contents unamwamini kumbe . ...ni chui katika ngozi ya kondoo.
Jamani badilikeni na mbebe uhalisia mnalinajisi jina la Mungu tafadhali. Bora ijulikane kuwa wewe si mlokole kuliko kujifanya mwema mbele za watu ilhali matendo yako hata shetani anakushangaa.
Hii imetokana na kisa halisi kilichonitokea. Kama nilivoanza mwanzo kuwa nilipata rafiki humu ndani ambaye tulianza mahusiano tukiwa na malengo ya kufika hatua ya ndoa. Kimsingi huyu kaka ni anajipambanua humu ndani kuwa mcha Mungu sana na maandiko yake yanajidhihirisha ivo na hata alipokuwa nami amekuwa akijionyesha mwema sana. Ajabu akawa ananambia yeye kukutana na mimi ni Kaonyeshwa na mungu ili nitende nae huduma hapo ndipo nilipoanza kumuundia tume though mwanzo nilimuamini kiaina. Akawa ni mtu mwenye kunishauri sana juu ya uchaji Mungu. Mie nikaanza kuona kweli huyu katumwa kuja kuniokoa coz kiukweli mimi nimekuwa sio msafi kiroho yaani ni mdhambi tu.
Nikaendelea nae ktk hali ya uchumba hivo but alipohitaji nimpeleke home kidogo nikawa mzito sijui sababu. Akanitambulisha kwa rafiki na baadhi ya ndugu zake. Baada ya kama 3months jamaa huyu akarudi US coz anaishi huko na huku alikuja likizo ingawa ana mpango wa kurudi bongo akimaliza masomo yake . Huku akaniachia rasilimali zake kadhaa nizimiliki nami kiroho safi nikachukua maana alizibadilisha hata majina akaweka yangu.
Alipofika Marekani akawa anafanya mchakato niende kule nimfuate nami nikataaa kwakuwa alisema anamalizia masomo atarudi bongo so hakuna haja mie niende badala yake niboreshe hapa home. Akaniambia baba yake ambae ni anafanyia kazi huko na maisha yake kiasi kikubwa amefanya huko amemshauri asiondoke upesi that's why anataka niende. Nikamwambia anipe muda nijipange.
Wakati huo mimi mbali na kumwamini nikawa namfutilia kimya kimya kuanzia kanisani anakoabudu nikawa nimepata contacts za baadhi ya waumini pale, ndugu zake wengine pia nikawa nimepata contacts zao ili niwafukunyue details kadhaa za Bwana kaka. Mimi nina tabia ya ufukunyuku sana
Basi kupitia hizo contacts si ndio nikagundua mkaka kaoa na anaishi na mkewe na ana watoto ingawa kuhusu watoto alishanitonya alidai mama yao alimkimbia. Kumbe mkewe wanaishi pamoja. Nilipogundua nikatafuta muda nikamweleza akakiri ni kweli lkn mke ana matatizo hataki kujirekebisha ivo ameamua kumwacha na ana process divorce. Nikaishiwa nguvu why aniongopee. Nikaanza kumshauri ili asimwache. Akawa haelewi anakomaa tu bwana kamwonyesha mimi. Nikaona huyu analeta drama kwangu. Nikapata namba ya mkewe nikampigia nikijifanya nimekosea namba basi hapo hapo urafiki ukaanza nikaanza kumdodosa uhusiano wake akawa ananieleza yuko poa na mumewe na anampenda sana. Tukaendelea kuwasiliana na mkewe sana hata akanieleza weakness kadhaa za mumewe nami nikawa namshauri sana.
Huku upande wa huyu bwana humu jf na Facebook haonyeshi kama ameoa na humu jf anajifanya anatafuta mke mwema kutoka kwa Bwana daily na anatoa ushauri humu utajua boongeeee la mlokole na mume mwema ukijaaliwa kumpata. Mwenyezi Mungu atuponye nafsi kwakeli tumekuwa wanafiki mbele za watu.
Yaani naandika natetemeka natamani kama nimtaje mumjue na wapo wengi tu humu wameharibu ndoa zao halafu wanajifanya washauri nasaha wakati wanayoongea hawayaishi.
Basi mawasiliano yangu na mkewe yakanifanya nimuonee imani mwanamke mwenzangu kwani hata zile properties alizonipa huyu kaka huku bongo ni efforts za mkewe. Nikajisikia vibaya sana jinsi huyu kaka anavyomlazimisha mkewe amuache kwa visingizio vya kijinga ili tu atimize adhma yake awe na mimi wakti mimi nimeshamjua. Nikawa natafuta namna ya kumpa ukweli. Baadae nikamweleza lakini hakujali ndio akazidisha dharau kwa mkewe. Ikabidi nimpe mkewe ukweli kuhusu mimi na uhusiano wangu na mumewe na niko tayari kutoa ushahidi amweleze tu na mimi siwezi kuwa nae kwakuwa hakunieleza ukweli na kimsingi yuko na mkewe na kwanini awe analitumia jina la Mungu kuniaminisha kuwa yeye ndie mtu sahihi kwangu maana naamini Mungu hawezi fanya double standard.
Basi nikaibua ugomvi mkubwa kwenye ile familia lkn niliahidi full support kwa mke. Mke akahama pale home kwa muda .huyu mume ndio kama karogwa akazidi kujileta kwangu. Nikamblock kwa simu akawa ananitumia pm tu humu jf simjibu niko karibu na mkewe tu.akaenda mahakamani kufungua kesi ya talaka ili amuache mkewe akisisitiza mungu wake kamwonyesha mimi ndie mkewe. Hali ikawa si shwari habari ikawafikia ndugu zao nami nikawa tayari kuwaeleza ukweli.
Talaka haikutolewa hadi sasa ingawa wawili hawa wanaishi nyumba tofauti lakini wewe jamaa naomba uniache na ukizidi kunifuatailia nakutaja humu humu jf na mengine mengi sijayasema unajua.
Halafu fanya toba ya kweli Acha kujionyesha kwa watu humu kuwa wewe unamjua sana Mungu na unawadanganya watu kuwa una mchumba utamuoa wakati huko unaishi na mkeo na hamjaachana sio vizuri unadhalilisha Ukristo aisee.
Jitafakari upya na ujitathmini.
Mkeo anakupenda sana kamuombe msamaha mlee watoto. Hakuna alie mkuu kuliko Mungu utambue. Jiulize tu mwanadamu ni nani hata ajikweze. Umeaibisha ingawa sio issue bali issue kuwa mkweli na mhalisia. Unawezaje kujiita mlokole halafu unafanya ubazazi mkeo yumo ndani eti unanipenda
Najua mihemko tu inakusukuma na ninakuombea pia utambue ulichofanya ili utubu.
Poleni wanajamii mimi si mwandishi mzuri so hata mpangilio sio mzuri ila ujumbe wangu mkuu ni kwa wale pretenders wabadilike jamani halafu tabia zenu za kudhania kwakuwa mko nje ya nchi basi tunawahusudu na viingereza vyenu muache. Sisi tupo hapa bongo na tunawapiga gap sana kimaendeleo. Kuwa nje kuwafanye mtumie fursa vizuri kukwamua familia na taifa sio kujionyesha.
Muwe na vision lol.
Jumapili njema.
Kwa makala hii nimekupenda bure
 
Mmh! Ona sasa... kumbe sitaki nataka... na wewe umemzimia pia... wewe mwanamke ni mbaya sasa...

Unampelekesha mlokole alafu unasema ni ujinga wake...
Hadi nilipokubali kuwa nae ujue nilishamzimia na malengo yalikuwa kufika mbali zaidi. Sasa itakuwaje wakati anaishi na mke na sijui ingekuwaje ningekomaa kuenda huko America dah! !
 
Hadi nilipokubali kuwa nae ujue nilishamzimia na malengo yalikuwa kufika mbali zaidi. Sasa itakuwaje wakati anaishi na mke na sijui ingekuwaje ningekomaa kuenda huko America dah! !
Dah, Kumbe ndo yeye Bwana... I know the man.... Ila nimegundua hata wewe unampenda... Ila mistake KUBWA umefanya ni kumshirikisha Mkewe.. Wewe ungesepa Zako Kimya Kimya tu... Amini nakwambia ushavuruga hiyo Ndoa na am very sure Muda si mrefu utabeba mimba ya jamaa... Nisikilizeni Mimi..
 
ungetumia busara2 kuachana nae kimyakimyaaaa.,..
umeshaharibu then baadae ndo unamblock na kufuta mawasliano nae
na kumpotezea,...umeharibu dada seriously
hukuwa fair
ndoa na iheshimiwe na watu wote,....we ulipojua anamke nini kilikupelekea utafute had namba ya wife wake wakat
ulichotafta tyr ulijua kuwa ameoa had kumtafta mkewe hukujua effect zake,...#
umeharibu dada
Hata angemuacha mkewe kimya halafu akawa nami unadhani isingefahamika na huyo mkewe kuwa now yuko na nani? kumbuka wanaunganishwa na watoto hawa watu.
Kwahiyo ningeendelea tu kumwacha na ubazazi wake?
Nilimwambia tuachane kimya hakutaka ningemfanyaje na hata sasa labda akiona hii thread ndio anaweza juwa niko serious sihitaji amwache mkewe kwaajili yangu hata kama anataja madhaifu ya mkewe
 
Nimesoma uzi na comments za wadau + replies za mleta uzi.. Nimegundua yafuatayo

1. Mleta uzi hana tofauti na huyo anaomuona kama shetan
 
Sasa ulimwambia muachane Kimya Kimya Wakati ushamchokoza Mkewe??? Yaani ulipogundua tu jamaa anamke wewe ungekaa Kimya... Umemblock sawa, basi ungeanzisha ID nyingine pia ili usipate usumbufu kutoka kwako kupitia ID hii.. Unajua kinachoonekana hapa si kwamba eti umefanya hivyo kwa maslahi ya familia Yake, umefanya hivyo ili kumkomoa. N umefanikiwa... Uzuri ni kwamba Mungu haendi likizo .. Ataitika tu Muda si mrefu..
 
Mimi humu kuna watu huwa wananishangaza,ogopa sana watu wanaojifanya kondoo daily,who do you want to impress
Yani ukipiga kona mtu kamwagika maushauri jamaniii.... Ngoja nivumilie nimute kwanza ila sioni kwanini watu wakae kuhangaika kuimpress watu,kudraw attention lol....Brenda funga domo lako
 
Dah, Kumbe ndo yeye Bwana... I know the man.... Ila nimegundua hata wewe unampenda... Ila mistake KUBWA umefanya ni kumshirikisha Mkewe.. Wewe ungesepa Zako Kimya Kimya tu... Amini nakwambia ushavuruga hiyo Ndoa na am very sure Muda si mrefu utabeba mimba ya jamaa... Nisikilizeni Mimi..
Yeye anaona raha tu mkewe aondoke ili awe huru. Sasa wewe huoni shida hapo?
Hata haumizwi na kuachwa na mkewe ndio maana analazimisha talaka kwa sababu zake anazozitaja.
Mimi namshauri sana asimwache na namuona huyo mke hana hatia isipokuwa huyu jamaa mihemko tu imemuingia.
Hata kama nilikuwa na plan na jamaa na nilishaamua kumwacha lkn siko tayari kushuhudia ndoa yake ikianguka nami nichukue fursa.
Naheshimu sana ndoa na niko tayari kuilinda kadri niwezavyo nisingependa kuwa sehemu ya uharibifu wa ndoa za wengine kwa kukusudia au kwa bahati mbaya .
Nimegundua niliingia kwa mume wa mtu simple namwacha hata kama nampenda sana huyo si wangu. Najaribu kuvaa kiatu cha mwanamke mwenzangu.
 
Nimesoma uzi na comments za wadau + replies za mleta uzi.. Nimegundua yafuatayo

1. Mleta uzi hana tofauti na huyo anaomuona kama shetan
Kivip mkuu?
Sasa tungekuwa sawa si nami ningepretend tu kiunafiki kuwa nae zaid wakati mume wa mtu?
 
Sasa ulimwambia muachane Kimya Kimya Wakati ushamchokoza Mkewe??? Yaani ulipogundua tu jamaa anamke wewe ungekaa Kimya... Umemblock sawa, basi ungeanzisha ID nyingine pia ili usipate usumbufu kutoka kwako kupitia ID hii.. Unajua kinachoonekana hapa si kwamba eti umefanya hivyo kwa maslahi ya familia Yake, umefanya hivyo ili kumkomoa. N umefanikiwa... Uzuri ni kwamba Mungu haendi likizo .. Ataitika tu Muda si mrefu..
Mkuu hii I'd mpya ya early last year. I'd hiyo anayoijua zimejaa pm.
Kikubwa hujui nimeumia jitihada kiasi gani kumkwepa.
Halafu kwanini umuache mkewe practically?
Huoni tatizo na kiufupi nilivomwambia namweleza mkewe yeye hata hajutii anaona raha tu ili mkewe a give up.
We huoni tatizo kwa huyu ndugu. Nimeleta huu uzi uwaponye na wengine jamani. Huyu jamaa si bure atakuwa na spirit mbaya zimemuingia ati. .nasisitiza sijavunja ndoa yake hata kidogo anataka kuivunja yeye na mkewe yuko tayari waendelee yeye hataki anasisitiza mungu wake kamuonyesha mimi
 
Mimi humu kuna watu huwa wananishangaza,ogopa sana watu wanaojifanya kondoo daily,who do you want to impress
Yani ukipiga kona mtu kamwagika maushauri jamaniii.... Ngoja nivumilie nimute kwanza ila sioni kwanini watu wakae kuhangaika kuimpress watu,kudraw attention lol....Brenda funga domo lako
Sema wewe mama.
Humu ndani shida tena wapo hadi wadada design hizi hizi.
Mtaumbuka halafu mbadili I'd
 
Hivi kumkataa mwanaume ni mpaka uvunje ndoa yake... Au hujui kuwa kuna njia nyingine za kumpotezea mwanaume bila kuathir ustaw familia yake ???
Nimeivunjaje hiyo ndoa ilihali mwenyewe amefanya majaribio kadhaa ya kumwacha mkewe hata kabla sijamjua mkewe na ndio maana hakunieleza ana mke coz alijua atafanikiwa kumwacha kabla hajanioa?
Mie nimekuja baadae sana na hata hajali coz anataka tu amwache mke
 
Back
Top Bottom