Nini Faida ya u fake katika maisha?

Nini Faida ya u fake katika maisha?

Hivi kumkataa mwanaume ni mpaka uvunje ndoa yake... Au hujui kuwa kuna njia nyingine za kumpotezea mwanaume bila kuathir ustaw familia yake ???
Halafu mimi sikumkataa hapo Mwanzo bali baada ya kujua ana mke.
 
Mkuu hii I'd mpya ya early last year. I'd hiyo anayoijua zimejaa pm.
Kikubwa hujui nimeumia jitihada kiasi gani kumkwepa.
Halafu kwanini umuache mkewe practically?
Huoni tatizo na kiufupi nilivomwambia namweleza mkewe yeye hata hajutii anaona raha tu ili mkewe a give up.
We huoni tatizo kwa huyu ndugu. Nimeleta huu uzi uwaponye na wengine jamani. Huyu jamaa si bure atakuwa na spirit mbaya zimemuingia ati. .nasisitiza sijavunja ndoa yake hata kidogo anataka kuivunja yeye na mkewe yuko tayari waendelee yeye hataki anasisitiza mungu wake kamuonyesha mimi
Sawa Ila kitendo cha kumvulia tu chupi jamaa ilikua tayari ushaharibu Ndoa Yake.. Na Hilo halifutiki.. Na nikuulize, ulimwambia Mkewe Kama jamaa Amekula mzigo Mara kadhaa and he is so sweet???
 
Nimeivunjaje hiyo ndoa ilihali mwenyewe amefanya majaribio kadhaa ya kumwacha mkewe hata kabla sijamjua mkewe na ndio maana hakunieleza ana mke coz alijua atafanikiwa kumwacha kabla hajanioa?
Mie nimekuja baadae sana na hata hajali coz anataka tu amwache mke

Huon njia uliyoichukua so far ni better kuliko ulivyokuwa unafanya kama kumpigia simu mke wake n.k...

Halafu bado unajiona ni mwema na mshika dini kumbe na wewe ni joka lenye makengeza... Na umeshaandika kuwa jamaa umetembea nae wakat unajua tendo hilo kabla ya ndoa ni dhambi... Unajitoaje kuwa nyie wote sio kenge ...

Amin kilio na manunguniko ya mwanamke mwezio kwa sasa yatakutokea puan..

Huyo mwanaume kuwa muongo kwako hakujustfy upumbavu wako
 
Sawa Ila kitendo cha kumvulia tu chupi jamaa ilikua tayari ushaharibu Ndoa Yake.. Na Hilo halifutiki.. Na nikuulize, ulimwambia Mkewe Kama jamaa Amekula mzigo Mara kadhaa and he is so sweet???
Nilijua niko peke yangu kama alivoniaminisha ndipo nikampa ladha za bongo.
Huyo jamaa ana jifanya ana upako yaani huwezi mkataa kama uko serious
 
Mkuu natumai utakua umejifunza kufikiri kwa makini zaidi.
Matumizi ya jina la Mungu yakiambatana na zinaa yana walakini ndani yake.
Unalaumu jamaa kujidai mtumishi wakati mmegegedana bila ndoa,hukuona dosari kwenye utumishi wake mpaka hapo mkuu?
Next time bwana akimuonyesha mtu kwako na mkalana kabla ya ndoa shtuka,hamna mtumishi hapo.
 
Niliamua kufanya kimya kiroho safi lakini jamaa alivozidi kunikomalia na ujue kuna vitu vingi katikati vilitokea. Alivozidi kunikomalia hata kuelekea kumtafutia mwenzie talaka nikaona isiwe shida Acha nidhihirishe ukweli huu. Maana wakati wa mawasiliano yangu na mkewe pia alikuwa akimention uhusiano wangu na mumewe kuwa ni kichochezi. Alikuwa anasema mumewe anwasiliana sana na mwanamke huko bongo na anaomba sana huyo mwanamke ajue ukweli pasipo yeye kujua kuwa huyo mwanamke ni mimi. Nikamjuza jamaa aachane nami ili a Lee family yake hakunielewa.
Better apate mwanamke mwingine na sio mimi.
Amevunja ndoa yake mwenyewe ingawa anaweza kuokoa coz mkewe bado anampenda sana na mimi nikizidi kumkataa jamaa ndipo nairudisha hiyo ndoa though mkaka mlokole anaweza kuwa ana jini mahaba coz si bure uwe tayari kumwacha mkeo just because of mimi Aaahhh
ila wewe baada ya kujua jamaa kaowa,ungemwacha juu kwa juu ,ulifanya kosa kumwambia mkewe.wEWE UNGEMWACHA TU HUYO JAMAA KIMYA KIMYA
 
Huon njia uliyoichukua so far ni better kuliko ulivyokuwa unafanya kama kumpigia simu mke wake n.k...

Halafu bado unajiona ni mwema na mshika dini kumbe na wewe ni joka lenye makengeza... Na umeshaandika kuwa jamaa umetembea nae wakat unajua tendo hilo kabla ya ndoa ni dhambi... Unajitoaje kuwa nyie wote sio kenge ...

Amin kilio na manunguniko ya mwanamke mwezio kwa sasa yatakutokea puan..

Huyo mwanaume kuwa muongo kwako hakujustfy upumbavu wako
Mimi mdhambi sana tu au hujasoma uzuri bandiko langu? Ndio maana jamaa alipokuja kwangu ki dini nikajua sasa naokolewa mie mwana mpotevu.
Kumbe nae anataka anayo ya taka. Ila kaniweza sana kuniaminisha kuwa kaagizwa na bwana
 
Mkuu natumai utakua umejifunza kufikiri kwa makini zaidi.
Matumizi ya jina la Mungu yakiambatana na zinaa yana walakini ndani yake.
Unalaumu jamaa kujidai mtumishi wakati mmegegedana bila ndoa,hukuona dosari kwenye utumishi wake mpaka hapo mkuu?
Next time bwana akimuonyesha mtu kwako na mkalana kabla ya ndoa shtuka,hamna mtumishi hapo.
Hapo ndipo palinifanya nimfukunyue mtumishi na utumishi wake ikizingatiwa mimi ni mdhambi tu. Nikaanza kutaka kujua hivi na watumishi nao swaga zao za ki dhambi kama sisi wa duniani? Mtumishi baana aliniweza sana
 
Wakuu habarini za jumapili.
Leo napenda kuzungumzia suala la mtu ku pretend na kutaka kuonekana katika jamii kwamba ni mtu fulani smart lakini anachokionyesha yeye hayuko hivo hata kidogo .
Suala hili lipo sana hapa jf na mtaani yamkini. Na huu ufake unapelekwa hadi kwenye mahusiano. Kwanini usiwe wewe halisi? Wapungukiwa nini? Ya nini kujitia mzigo kwa sababu mwisho wa siku hutoweza ku maintain hizo dramas kwa muda mrefu wenye upeo watakuumbua tu.
Kisa kamili. .....
Niliwahi kutafuta rafiki hapa jf na kwa bahati nzuri niliwapata wengi kisha nikafanya uchambuzi yakinifu nikaibuka na mchumba hapa .
Ukaribu wangu na jf ingawa sichangii sana mada nimekuwa msomaji zaidi kutokana na ukulima wangu unaniweka busy sana lakini nimeweza kufahamiana na wadau wengi humu nje ya jukwaa lkn ni members wa jf.
Katika kuwafahamu na kuwasoma nimegundua ufake mwingi sana kwa wanajamii humu ndani. Anyway ni fantasy zao no objection.
Ila kinachonipelekea leo nilete mada ni juu ya wale ma fake kiasi cha kumshirikisha hata Mungu ku justify ubazazi wao. Hapo nawachoka kabisa yaani.
Yaani unamkuta mtu anajipambanua humu ndani kuwa ni bonge la mcha Mungu na anaandika vitu full contents unamwamini kumbe . ...ni chui katika ngozi ya kondoo.
Jamani badilikeni na mbebe uhalisia mnalinajisi jina la Mungu tafadhali. Bora ijulikane kuwa wewe si mlokole kuliko kujifanya mwema mbele za watu ilhali matendo yako hata shetani anakushangaa.
Hii imetokana na kisa halisi kilichonitokea. Kama nilivoanza mwanzo kuwa nilipata rafiki humu ndani ambaye tulianza mahusiano tukiwa na malengo ya kufika hatua ya ndoa. Kimsingi huyu kaka ni anajipambanua humu ndani kuwa mcha Mungu sana na maandiko yake yanajidhihirisha ivo na hata alipokuwa nami amekuwa akijionyesha mwema sana. Ajabu akawa ananambia yeye kukutana na mimi ni Kaonyeshwa na mungu ili nitende nae huduma hapo ndipo nilipoanza kumuundia tume though mwanzo nilimuamini kiaina. Akawa ni mtu mwenye kunishauri sana juu ya uchaji Mungu. Mie nikaanza kuona kweli huyu katumwa kuja kuniokoa coz kiukweli mimi nimekuwa sio msafi kiroho yaani ni mdhambi tu.
Nikaendelea nae ktk hali ya uchumba hivo but alipohitaji nimpeleke home kidogo nikawa mzito sijui sababu. Akanitambulisha kwa rafiki na baadhi ya ndugu zake. Baada ya kama 3months jamaa huyu akarudi US coz anaishi huko na huku alikuja likizo ingawa ana mpango wa kurudi bongo akimaliza masomo yake . Huku akaniachia rasilimali zake kadhaa nizimiliki nami kiroho safi nikachukua maana alizibadilisha hata majina akaweka yangu.
Alipofika Marekani akawa anafanya mchakato niende kule nimfuate nami nikataaa kwakuwa alisema anamalizia masomo atarudi bongo so hakuna haja mie niende badala yake niboreshe hapa home. Akaniambia baba yake ambae ni anafanyia kazi huko na maisha yake kiasi kikubwa amefanya huko amemshauri asiondoke upesi that's why anataka niende. Nikamwambia anipe muda nijipange.
Wakati huo mimi mbali na kumwamini nikawa namfutilia kimya kimya kuanzia kanisani anakoabudu nikawa nimepata contacts za baadhi ya waumini pale, ndugu zake wengine pia nikawa nimepata contacts zao ili niwafukunyue details kadhaa za Bwana kaka. Mimi nina tabia ya ufukunyuku sana
Basi kupitia hizo contacts si ndio nikagundua mkaka kaoa na anaishi na mkewe na ana watoto ingawa kuhusu watoto alishanitonya alidai mama yao alimkimbia. Kumbe mkewe wanaishi pamoja. Nilipogundua nikatafuta muda nikamweleza akakiri ni kweli lkn mke ana matatizo hataki kujirekebisha ivo ameamua kumwacha na ana process divorce. Nikaishiwa nguvu why aniongopee. Nikaanza kumshauri ili asimwache. Akawa haelewi anakomaa tu bwana kamwonyesha mimi. Nikaona huyu analeta drama kwangu. Nikapata namba ya mkewe nikampigia nikijifanya nimekosea namba basi hapo hapo urafiki ukaanza nikaanza kumdodosa uhusiano wake akawa ananieleza yuko poa na mumewe na anampenda sana. Tukaendelea kuwasiliana na mkewe sana hata akanieleza weakness kadhaa za mumewe nami nikawa namshauri sana.
Huku upande wa huyu bwana humu jf na Facebook haonyeshi kama ameoa na humu jf anajifanya anatafuta mke mwema kutoka kwa Bwana daily na anatoa ushauri humu utajua boongeeee la mlokole na mume mwema ukijaaliwa kumpata. Mwenyezi Mungu atuponye nafsi kwakeli tumekuwa wanafiki mbele za watu.
Yaani naandika natetemeka natamani kama nimtaje mumjue na wapo wengi tu humu wameharibu ndoa zao halafu wanajifanya washauri nasaha wakati wanayoongea hawayaishi.
Basi mawasiliano yangu na mkewe yakanifanya nimuonee imani mwanamke mwenzangu kwani hata zile properties alizonipa huyu kaka huku bongo ni efforts za mkewe. Nikajisikia vibaya sana jinsi huyu kaka anavyomlazimisha mkewe amuache kwa visingizio vya kijinga ili tu atimize adhma yake awe na mimi wakti mimi nimeshamjua. Nikawa natafuta namna ya kumpa ukweli. Baadae nikamweleza lakini hakujali ndio akazidisha dharau kwa mkewe. Ikabidi nimpe mkewe ukweli kuhusu mimi na uhusiano wangu na mumewe na niko tayari kutoa ushahidi amweleze tu na mimi siwezi kuwa nae kwakuwa hakunieleza ukweli na kimsingi yuko na mkewe na kwanini awe analitumia jina la Mungu kuniaminisha kuwa yeye ndie mtu sahihi kwangu maana naamini Mungu hawezi fanya double standard.
Basi nikaibua ugomvi mkubwa kwenye ile familia lkn niliahidi full support kwa mke. Mke akahama pale home kwa muda .huyu mume ndio kama karogwa akazidi kujileta kwangu. Nikamblock kwa simu akawa ananitumia pm tu humu jf simjibu niko karibu na mkewe tu.akaenda mahakamani kufungua kesi ya talaka ili amuache mkewe akisisitiza mungu wake kamwonyesha mimi ndie mkewe. Hali ikawa si shwari habari ikawafikia ndugu zao nami nikawa tayari kuwaeleza ukweli.
Talaka haikutolewa hadi sasa ingawa wawili hawa wanaishi nyumba tofauti lakini wewe jamaa naomba uniache na ukizidi kunifuatailia nakutaja humu humu jf na mengine mengi sijayasema unajua.
Halafu fanya toba ya kweli Acha kujionyesha kwa watu humu kuwa wewe unamjua sana Mungu na unawadanganya watu kuwa una mchumba utamuoa wakati huko unaishi na mkeo na hamjaachana sio vizuri unadhalilisha Ukristo aisee.
Jitafakari upya na ujitathmini.
Mkeo anakupenda sana kamuombe msamaha mlee watoto. Hakuna alie mkuu kuliko Mungu utambue. Jiulize tu mwanadamu ni nani hata ajikweze. Umeaibisha ingawa sio issue bali issue kuwa mkweli na mhalisia. Unawezaje kujiita mlokole halafu unafanya ubazazi mkeo yumo ndani eti unanipenda
Najua mihemko tu inakusukuma na ninakuombea pia utambue ulichofanya ili utubu.
Poleni wanajamii mimi si mwandishi mzuri so hata mpangilio sio mzuri ila ujumbe wangu mkuu ni kwa wale pretenders wabadilike jamani halafu tabia zenu za kudhania kwakuwa mko nje ya nchi basi tunawahusudu na viingereza vyenu muache. Sisi tupo hapa bongo na tunawapiga gap sana kimaendeleo. Kuwa nje kuwafanye mtumie fursa vizuri kukwamua familia na taifa sio kujionyesha.
Muwe na vision lol.
Jumapili njema.
Kaaazi kweli kweli..kitu hua naamini,kumchomoa mume/mke kupitia hii mitandao ya kijamii hua ni kubahatisha sana,ndiyo maana zama zile ulipokua mjini wazazi waliendelea kuamini mtu wa kuishi na mwanao yupo mazingira walipo wao,late say kijijini,tulikua tukiambiwa umekua sasa tunakutafutia mke huku kutoka familia yenye heshima uje uoe!!! na kama ni kijana kweli ataenda bush na kubeba wa ubavu wake alietafutiwa na wazazi wake au wazee wenye heshima wa ukoo wake au hata marafiki.kusudi kujua tabia ya mlengwa na familia yake wana nidhamu ya kibinadamu na hofu ya MUNGU,sasa jambo hlo ni gumu kwa leo hii,utawezaje kumpata wa kweli kupitia jf,fb,insta,tweet na kwingineko?la hasha ndugu zanguni dunia imekua kichaa na huu uzungu tunaouiga.huwezi kutoa mume/mke humu kwenye mitandao na ukimpata utakua nae lakini yamkini siku moja ukalia.ASANTE
 
ila wewe baada ya kujua jamaa kaowa,ungemwacha juu kwa juu ,ulifanya kosa kumwambia mkewe.wEWE UNGEMWACHA TU HUYO JAMAA KIMYA KIMYA
Yaani ungekuwa na huyu jamaa alivokuwa anafanya wakati hajui nimemjua anakaa na mkewe ungecheka na kulia wakati huo huo. Na Nilipomweleza akaanza kulaumu shetani huku akifunga na kuomba aisee. Yaani kama hadithi vile sijui ana nini. Unajua amenikatisha tamaa kuwaamini tena watumishi.
Sikuwa na namna ikabidi nimweleze mkewe very technical na at the mean time zile weakness alivokuwa ananieleza za mkewe nikawa namshauri mkewe pasipo kujua ajirekebishe ili jamaa ampende zaid. Nae mwishowe akawa anasema dah mama fulani siku hizi yuko poa sana. Mimi na furahi huku naumia kumkosa MBEBA box. Anyway nilidhamiria amrudie mkewe.
Na sasa ninataka apunguze drama humu ndani lol.
Nina imani ni kipindi cha mpito na akiniona niko serious kutokuwa nae hadi nimemleta humu anaweza ni Acha kabisa na atambue umuhimu wa mkewe
 
Mapenzi yana nguvu Sana, natabiri utarudi na Uzi mwengine, usiache kunitumia Kadi ya mchango wa harusi.. Me napatikana wilaya ya kinondoni,
Harusi tena?
Na baba mtumishi au na mwingine?
Baba mtumishi arudi kwa mama watoto wake aisee
 
Yaani ungekuwa na huyu jamaa alivokuwa anafanya wakati hajui nimemjua anakaa na mkewe ungecheka na kulia wakati huo huo. Na Nilipomweleza akaanza kulaumu shetani huku akifunga na kuomba aisee. Yaani kama hadithi vile sijui ana nini. Unajua amenikatisha tamaa kuwaamini tena watumishi.
Sikuwa na namna ikabidi nimweleze mkewe very technical na at the mean time zile weakness alivokuwa ananieleza za mkewe nikawa namshauri mkewe pasipo kujua ajirekebishe ili jamaa ampende zaid. Nae mwishowe akawa anasema dah mama fulani siku hizi yuko poa sana. Mimi na furahi huku naumia kumkosa MBEBA box. Anyway nilidhamiria amrudie mkewe.
Na sasa ninataka apunguze drama humu ndani lol.
Nina imani ni kipindi cha mpito na akiniona niko serious kutokuwa nae hadi nimemleta humu anaweza ni Acha kabisa na atambue umuhimu wa mkewe
Hivi Lara 1 Yuko wapi?? Wanaoweza kumuita mnisaidie.. Iko namna atatusaidia ktk Uzi huu.
 
Back
Top Bottom