dibbo
Member
- Feb 18, 2011
- 30
- 1
Wana jf naomba mnipe faida na hasara za mirungi aka gomba
MADHARA YA KIAFYA;
1. Mtumiaji wa mirungi yupo
katika hatari ya kupata
vidonda vya tumbo.
- Kupungukiwa msukumo wa
kufanya tendo la ndoa (low sex drive) na pia kuwahi kumaliza haraka na kutoweza kudumu kwenye tendo la ndoa kwa muda mrefu.
2. Ukosefu wa haja kubwa (constipation)
3. Utumiaji wa muda mrefu
husababisha ini kushindwa
kufanya kazi, pia meno kubadilika rangi, kudhoofika, fizi kuuma na harufu mbaya
mdomoni.
4. Upungufu wa usingizi.
5. Humpelekea mlaji
kutawaliwa nayo. (addiction)
6. Madhara ambayo bado
kinamama walaji Mirungi
hawajagundua ni kwamba
mtoto anayezaliwa na mama
mlaji Mirungi mara nyingi
hukataa kunyonya titi la mama
yake kwa sababu ladha ya
maziwa inabadilika kwa ajili ya
utumiaji wa madawa (pesticides) unaotumiwa na
wakulima wa Mirungi kama
inavyoeleza utafiti uliofanyika
na Chuo Kikuu Cha Aden
(Aden University).
7. Utafiti mwengine kule
Ethiopia unatueleza ya kuwa
mtoto wa mama mwenye kula
Mirungi kwa wingi huwa hana
uzito wa kawaida wakati wa
kuzaliwa.
8. Ukosefu wa hamu ya kula
chakula.
9. Magonjwa ya vidonda vya tumbo (ulcers).
10. Kupatwa na ugonjwa wa futuru/futuri/bawasiri/baasili - nyama inayoota kwenye utupu wa nyuma.
11. Walaji wengi huvuta na sigara, hata yule aliyekuwa havuti kabla ya kuanza kula Mirungi, hujikuta akizama kwenye uvutaji, na madhara huwa maradufu.
source;
polisijamiimafia: MIRUNGI NA MADHARA YAKE