Chief Kabikula
JF-Expert Member
- Jan 1, 2019
- 7,567
- 9,035
Tanzania mpaka sasa tuna marais wastaafu watatu ukiacha Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyetangulia mbele za haki.
Hawa marais wastaafu ni wazoefu na wajuzi sana wa mambo kupitia uzoefu wa kuongoza nchi kwa miaka kumi kila mmoja.
Swali huo uzoefu, maarifa na ujuzi wao umesaidia vipi nchi hii. Baba wa taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Alipokabidhi kijiti kwa rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi hakusita kumkosoa waziwazi pale alipoona mzee Mwinyi anaenda ndivyo sivyo, aliwahi kutamka huwezi kuongoza nchi kwa kushauriwa na mke wako maana hatujui kesho atakushauri nini.
Hilo lilikuwa ni dongo kwa rais Ali Hassan Mwinyi wakati, mpaka Mwalimu Nyerere akaandika kitabu cha uongozi wetu na Hatima ya Tanzania, yote hiyo ilikuwa na lengo moja tu kukosoa utawala kwa manufaa ya nchi.
Wakati wa utawala wa awamu ya tatu ya mzee Benjamin William Mkapa Mwalimu Nyerere hakukaa kimya, alipoona mambo yanaenda ndivyo sivyo alikemea, wakati wa sera za ubinafsishaji, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alimkosoa vikali mzee Mkapa kwa kubinafsisha mali za umma hasa NBC BANK pamoja na uwekezaji wa wageni katika madini wakati huo.
Hiyo yote aliifanya baba wa taifa katika lengo la kuisaidia nchi alitimiza wajibu wake kwa nchi yake.
Leo tuna marais wastaafu watatu ujuzi, maarifa na uzoefu wa kukaa ikulu miaka kumi wapo kimya licha ya kila dalili kuonyesha kuwa uongozi wa sasa umekengeuka na utaleta sintofahamu kama tahadhari hazitochukuliwa.Faida ya hawa viongozi wastaafu nini kwa nchi hii?