Nini Faida ya Kuwa na Serikali ya Tanganyika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini Faida ya Kuwa na Serikali ya Tanganyika?

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by LordJustice1, Nov 29, 2011.

 1. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Humu JF kumekuwa na washabiki wa kuwepo kwa Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano lakini ukiwauliza juu ya faida za kuwa na Serikali hiyo huingia mitini! Wao wanachotaka tu ni "Serikali ya Tanganyika," basi! Hawataki kusikia neno "Tanzania Bara" au vinginevyo. Pia hawajali kwamba kuanzishwa kwa Serikali ya Tanganyika kutatimiza utabiri wa Baba wa Taifa, Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere kwamba kutaua Muungano kwa kuwa "Mafahali wawili hawakai zizi moja!"
  Mimi napenda nifahamu "faida" na "hasara?" za kuanzishwa kwa Serikali ya Tanganyika, kama zipo!
  1. Je, ufisadi ulioishinda Serikali ya Tanzania, sasa "mbabe" wake atakuwa Serikali ya Tanganyika?
  2. Je, umaskini ulioishinda Serikali ya Tanzania, Tanganyika ndiye atakayekuwa "mkombozi" wetu?
  Kwa ujumla nafuu ni ipi hasa? Au tunataka kuwa kama Waisraeli walivyotaka kuwa na mfalme walielezwa hasara zake (1Sam. 8:11-20) wao walidai tu kwamba "tunataka kuwa na mfalme ili tufanane na mataifa mengine?" Je, hapa tunataka "tufanane tu na Zanzibar" kwa kuwa wana Rais wao, bendera, wimbo wa Taifa, nk? Only that?
   
 2. m

  mahangu Senior Member

  #2
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 145
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Mwana jf faida ziko nyiki kama ifuatvyo:-1. itaondoa manung'uniko mengi juu ya Muungano hasa kwa masuala yasiyo ya Muungano2. Serikali ya Muungano haita fikiria tena kuongeza masuala ya muungano kama inavyofanya sasa (toka 11 mpaka 22)3. Kutakuwa na usawa wa matumizi ya rasilimali kwa kila pande ya muungano4. Muungano utakuwa imara zaidi5. Usimamizi wa rasili mali huenda uka imarishwa zaidilakini faida hizi, nazo zina hasara zake1. Kutimia kwa unabii wa Mwl JK kuwa " zanzibar ikijitenga kwa sababu ya ulevi tu wa madaraka hawatabaki wa moja", hata watanganyika huenda tusibaki wa moja kama tunavyodai, tutaanza ukabila na udini hasa katika kuongoza New Tanganyika. Hiyo ndo hasara kubwa ambayo tunaweza ipata.
   
 3. m

  muaminifu Member

  #3
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 28, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwani what do we benefit frm zanzibar katika serikali ya muungano? Ukijibu ,.(kama kuna faida yoyote)..then i'l gv sm adv of tanganyika govnt
   
 4. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #4
  Nov 30, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ulinzi na usalama wa nchi yetu! Bila Muungano tutakuwa tunapambana na "Al Shabaab wa Zanzibar" kila siku na hatimaye kuuangamiza umoja wa nchi yetu!
   
 5. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #5
  Nov 30, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hivi ulinzi wa rasilimali utaimarishwaje na Serikali ya Tanganyika? Tuseme Jina "Tanzania" linatusababisha tukawa maskini na Jina "Tanganyika" ndio litabadili mindset ya Watanzania na kuwa Wazalendo zaidi? Sio kwamba tukishabaguana kwa "Utanganyika" na "Uzanzibari" baadaye tutakuta hakuna kitu kizima kinachoitwa "Watanganyika?"
   
 6. crome20

  crome20 JF-Expert Member

  #6
  Dec 4, 2011
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 60
  TUTAPUNGUZA GHARAMA YA KUENDESHA SERIKALI MBILI . Just think, kuna wabunge wa baraza la mapinduzi, kuna wabunge wa muungano, spika wawili n.k wote hao wanalipwa posho kwa kodi zetu
   
 7. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #7
  Dec 5, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kuna watu wanapigana vita hadi leo kutetea utaifa wao, utamaduni wao, mipaka ya nchi zao, haki ya kujiamulia maisha yao. Kama haina maana kutunza utaifa wetu na utamaduni wetu kwa nini tusiwaite wajerumani waje waiendeshe nchi hii nafikiri itakuwa better off kiuchumi!
   
 8. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #8
  Dec 7, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,667
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  LordJustice1 kwani muungano huu ni muungano wa nchi au nini? hivi kama tukiungana si tunakuwa kitu kimoja?
  Lakini angalia wetu, ni muungano wa nchi mbili lakini moja ina serikali yake na nyingine je?
  Kisha ukinijibu kwa nini zanzibar hawataki tuwe serikali moja tu! yaani kusiwe na taifa linaloitwa zanzibar, basi nitakuwa na majibu mengi kwa nini tunahitaji Tanganyika yetu. Usidhani hatuna sababu ndugu yangu tunazo kabisa. Na mimi ni mmoja kati ya watu wanaoombea Tanganyika izaliwe au zanzibar ife. Na litatokea tu kama si leo, kesho.

  Tumechoshwa na usanii..
   
 9. Aaronium

  Aaronium Senior Member

  #9
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 10. k

  king'oko Member

  #10
  Jan 29, 2012
  Joined: Nov 26, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanganyika ni dira,dhamira,utaifa,mtazamo,kiu,thamani ya maisha yaliyopotea kwa watanganyika mara tu baada ya muungano kuasisiwa.kuna faida nyingi sana kwa kuwepo nchi na serikali ya tanganyika.Ni kweli wengi wanaoidai Tanganyika leo hawaijui bali kwao TANGANYIKA ni historia, ni kama kitu cha kufikirika tu.Na ni kweli endapo tutafanikiwa kuihuisha tanganyika yetu ni lazima tupite kwenye tanuri la hasara nyingi vile kwa miaka zaidi 48 Tanganyika ilikuwa kwenye hali ya ufu, hali ambayo fursa zozote hupoteza ujuzi,maarifa,uzoefu,utambuzi,thamani, n.k.Mtafakari mwanamke anapopoteza uthamani wake aolewapo,japo anabaki ni binadamu lakini hata nduguze humsahau na pengine kumsukumia kwa mumewe isipokuwa kwenye GHARAMA tu iwe furaha au tatizo. Imetugharimu na itaendelea kutugharimu so long tupo na tumeshilia mwamvuli ASINYESHEWE.
   
 11. k

  king'oko Member

  #11
  Jan 29, 2012
  Joined: Nov 26, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanganyika ni dira,dhamira,utaifa,mtazamo,kiu,thamani ya maisha yaliyopotea kwa watanganyika mara tu baada ya muungano kuasisiwa.kuna faida nyingi sana kwa kuwepo nchi na serikali ya tanganyika.Ni kweli wengi wanaoidai Tanganyika leo hawaijui bali kwao TANGANYIKA ni historia, ni kama kitu cha kufikirika tu.Na ni kweli endapo tutafanikiwa kuihuisha tanganyika yetu ni lazima tupite kwenye tanuri la hasara nyingi vile kwa miaka zaidi 48 Tanganyika ilikuwa kwenye hali ya ufu, hali ambayo fursa zozote hupoteza ujuzi,maarifa,uzoefu,utambuzi,thamani, n.k.Mtafakari mwanamke anapopoteza uthamani wake aolewapo,japo anabaki ni binadamu lakini hata nduguze humsahau na pengine kumsukumia kwa mumewe isipokuwa kwenye GHARAMA tu iwe furaha au tatizo. Imetugharimu na itaendelea kutugharimu so long tupo na tumeshilia mwamvuli ASINYESHEWE.
   
 12. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #12
  Feb 4, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tuache mawazo mgando tufikiri kwanza kwa akili zetu.
  Je muungano wetu umekaa sawa? ukijiuliza swali hili na ukiona haupo sawa basi kuna vitu vya kuweka sawa.
  Hofu za kuwa usalama sijui nini ni bahati mbaya tu kwamba tunashindwa kufikiria sawasawa zaidi ya kusukumwa na hofu/uoga.
  Ukiangalia duniani kote hakuna muungano kama huukwahiyo ili tuwe na maendeleo endelevu tunahitaji mifumo imara na sio watu imara kwani mtu imara akitutoka kama ilivyo Mwalimu tunayumba sana.
  Watanzania tufikiria kwanza huku tukiweka utaifa mbele.
   
 13. K

  KAMBAKO Member

  #13
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Hapo mwanzo palikuwepo na Serikali na Tanganyika. Pakawepo Serikali ya Zanzibar. Kisha wakaja wajanja wakatuambia tutafaidika sana tukiwa na Serikali ya Muungano wa nchi mbili tanganyika na Zanzibar. Lakini wakatuambia sisi watanganyika si kitu. Kitu ni Wazanzibari. Tukakubali tukaingizwa kwenye ndoa ya mkeka. Sasa watu wanataka Serikali yao ya awali. Mbona maswali yanazidi? Kipi rahisi, kuwaamulia? au kuwauliza wao wanachotaka ni nini????
   
 14. morenja

  morenja JF-Expert Member

  #14
  Feb 15, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 3,536
  Likes Received: 1,054
  Trophy Points: 280
  faida ya kurudisha tanganyika ni kuondoa udhalilishaji na makemeo ya dharau tunayo fanyiwa na idadi ya watu sawa na wa kata moja jiji dar es salaam..dhidi ya nchi ya tanganyika .kuwa tanzania kwa wazanzibar wanatuchukulia tanganyika sawa na mtu kubwa jinga ,
   
 15. n

  ng'wanigulu New Member

  #15
  Apr 11, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na @chakunyuma, ili tupate maendeleo endelevu, tunahitaji kujenga taasisi imara. Si watu imara. Maana tukichagua hilo la pili, basi hatuwezi kuwa na hakika na kesho.
   
 16. N

  NYAMKANG'ILI JF-Expert Member

  #16
  Apr 25, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 223
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Matatizo ya siku zote za muungano kwa maoni yangu yanaweza kupunguzwa kwa njia mbili tu, inayotekelezeka na isiyotekelezeka. Njia hizo ni (1) kuunda serikali moja tu (SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - SJMT), yaani SMZ ielee (be in suspense) kama inavyoelea TANGANYIKA; na (2) kuwa na serikali tatu: SMZ, SJMT na ST(SERIKALI YA TANGANYIKA). Njia ya kwanza ya kuwa na serikali MOJA, SJMT pekee, haitekelezeki bila ya kuingia gharama ambazo hazilipiki. NTAELEZA japo kidogo.


  ZANZIBAR kwa sasa kiuhalisia ni nchi (dola/state) kamili kabisa. Na hapa naomba nieleweke kuwa nimesema 'kiuhalisia' ZANZIBAR is a state, japo kisheria ZNZ is not a state (tazama hukumu ya MAHAKAMA YA RUFANI TANZANIA kati ya MACHANO KHAMIS ALLY & OTHERS V SMZ, kesi ya uhaini ya akina MAALIMU SEIF). Swali ni je, kwa nini ZNZ is a dola? KWA SABABU (1) wananchi wa ZNZ wanaamini kuwa ZNZ ni dola na taifa huru. Kwa kuwa ZNZ NI TAIFA HURU UKITAKA KUIFUTA zitaibuka vurugu ambazo gharama zake hazilipiki ; na (2) ZNZ ni dola kwa kuwa SJMT imeiruhusu itende kama dola kamili, matendo ya ZNZ ni ya kidola. Japokuwa kwa Katiba ya JMT RAIS wa ZNZ hadhi yake ni waziri katika SJMT, AMERUHUSIWA atende kama mkuu wa dola kwa (a) kupigiwa mizinga, (b) kutoa amri kwa mawaziri wenzake wa SJMT, (C) KUPEWA ULINZI wa RAIS wa dola kamili nk.


  Kwa nini TANGANYIKA inadaiwa irudi? KWA sababu, kwa maoni yangu, (1) ZNZ imekuwa dola ndani ya dola JMT kinyume na inavyotakiwa iwe; (2) kukosekana kwa mipaka inayoonekana wazi kati ya mamlaka ya SMZ na SJMT, ambapo sasa inaonekana kama vile JMT inaongozwa marais wawili na makamu wa rais watatu na mawaziri wakuu 2 nk. Kuthibitisha hayo, fuatilia matamko au maagizo yanayotolewa na viongozi kutoka ZNZ, tena kwa mambo ambayo si ya muungano, kwa watu wa TANGANYIKA na viongozi wao. HAPA HASIRA ZINAPANDA, na sauti ya madai ya TANGANYIKA inapazwa: na (3) kwa kuwa TANGANYIKA haijawahi kufa, ipo inaelea majukumu yake yakiwa yanatekelezwa na SJMT (TAZAMA KATIBA ya JMT IBARA ZA 4, 64 nk). KWA HIYO NI SUALA LA KUSEMA SASA, TANGANYIKA RUDI KAZINI.

  FAIDA ZA KURUDISHWA kwa TANGANYIKA ni (1) kuondoa mikanganyiko ya kimamlaka kati ya SMZ na SJMT, kwa TANG kutekeleza mambo yanayoihusu yasiyo ya muungano kama inavyofanya sasa hivi SMZ kwa upande wa ZNZ, na hivyo kupunguza kama siyo kuondoa kero za muungano; (2) HAKI ya TANG kuishi kwa mujibu wa mkataba wa MUUNGANO kati ZNZ na TANG wa 1964; (3) kupunguza muzigo wa TANG inayoelea kuendesha shughuli za JMT, kwani TANG ikirudi basi kwa nia ya kuleta usawa ZNZ na TANG zitachangia kwa usawa kuendesha SJMT, kama ambavyo MCHANGO wa BURUNDI katika Jumuia ya AFRIKA MASH (JAM) unavyolingana na ule wa Kenya na Tanzania, na ndiyo maana BURUNDI inapewa haki sawa na nchi hizo katika JAM. Kwa sasa ZNZ inadai usawa kutoka JMT wakati haichaingii kitu chochote katika kuiendesha, wanafanya JMT inayogharimiwa na TANG kama sehemu ya kuja kuchuma vyeo, mishahara minene pasipo wao kuchangia katika MFUKO WA PAMOJA WA FEDHA WA KUENDESHA JMT; na (4) muhimu zaidi, TANG nayo kupanga mikakati yake ya kuendesha shughuli za maendeleo ya watu wake.


  HOJA za kuwa MWL JKN alisema (1) kurudishwa kwa TANG ni sawa na (2) kuvunja muungano hazina mashiko. KWANZA JKN mwenyewe hakueleza ni kwa namna gani TANG ikija MUUNGANO utavunjwa. PILI hata kama alichosema MWL kina chembe za ukweli, ambazo kwa bahati mbaya mimi sizioni, MWL hakuwa MOHAMED wala YESU kwamba alichosema hakibadiliki daima. I humbly submit, part of my considered opinion ...
   
 17. N

  NYAMKANG'ILI JF-Expert Member

  #17
  Apr 26, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 223
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  WABONGO, BILA BONGO: mbona kweli hachangii faida za kurejeshwa Tanganyika?

   
 18. b

  balibamo Member

  #18
  May 3, 2012
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wana jf mi naunga mkono hoja ya kwa serikali ya tanganyika kwani kwa muda mrefu wazanzibar wamekuwa wkilalamikia mfumo wa muungano tulinao sasa,hivyo ni bora tuwe na serikali tatu,ya muungano,zanzibar na ya tanganyika,ya muungano ita deal na mambo yote ya muungano kama yatakavyokubaliwa,ya znz ita deal na yake ya ki-znz na ya tanganyika ita deal na welfare za watanganyika wake.
   
 19. L

  LOVI MEMBE JF-Expert Member

  #19
  May 3, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,121
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  tanganyika ni identity ya wabara kama ilivyo kwa wazanzibari na zanzibar yao. hakuna hoja hapa ya kusema kwakuwa ufisadi umejitokeza sana baada ya serkali ya muungano then tuvunje muungano ili kuepukana na ufisadi no.this is a narrow sense of the circumstances towards reclaim of the tanganyika sovereignty. kuna manung'uniko yanayoumbua utu wa mtanganyika. watu wanajisikia kuitwa watanzania hasa wabara. lakini mzanzibari piga ua huo utanzania hautaki . zanziba kwanza then hiyo tanzania. ndio maana wana spirit kubwa ya kuwafurusha watanganyika huko zanzibar. ingawa wao sisi huku bara tunawaona wtz wenzetu. hii noma sana tumechoka kuona kama tunajipendekeza na zanzibar. kwanza raia sisi wa kawaida faida yetu ya utanzania ni nini zaidi ya anasa ya kufikirika kuwa sisi ni wamoja. nia ya mwalimu kuikamata zenji inatokana na hofu iliyokuwa nayo dhidi ya sultan hata kabla ya uhuru. nafikiri tuachane na fikira potofu kama hizi gharama ya mawazo ya mtu mmoja yanatugharimu utu wetu hata leo. tuanze na neutral ground tuanze na mkataba mpya kwa kuweka mambo upya .tufanye ule ulifanywa haraka ili kumuondoa sultan na sasa tutengeneze kitu kipya kwa mkataba mpya utakaoridhiwa umma wa tanganyika na waznazibar bila kumuogopa yeyote. ukiona unawaogopa watu na kuwakamata wale wanokupinga basi ujue hicho unachokilinda kina walakini. iko tsunami itakayokuja kama maporomoko ya ardhi katika vilele vya milima na hakuna atakyezuia maana kila mmoja ataamua kulinda uhai wake dhidi ya mapande ya ardhi yatakayoshuka kwa kasi ya ajabu. MUUNGANO NINI BWANA MBARA HANA FAIDA LABDA WAFANYA SIASA NA WAFANYABIASHARA WA KIPEMBA WALIOJAZANA DAR HUKU NDUGU ZAO WANACHOMA MALI ZA WABARA HUKO ZANZIBAR KWA KISINGIZIO CHA UKAFIRI WA WABARA.
   
 20. L

  LOVI MEMBE JF-Expert Member

  #20
  May 3, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,121
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  ni akili gani tunayotumia huku bara wazanzibar wanatuteta hata kutunga sheria za kuwabagua watanganyika kwenye ajira kwenye baraza la wawakilishi. je sisi tuna nafasi gani ya kujibu mapigo kama haya. leo hii muswada unapopelekwa bungeni kutetea ajira za WABARA LAZIMA WAZENJI WASHIRIKI KWA AJILI YA KUWATETEA wazanzibar. kuna wazenji wangapi wako huku bara katika wizara zisizo za muungano wanapata ujira bila bughudha yoyote. lakini wabara wanafanya kazi za ujira WA kupanga nyanya NA NGUO kwa mitaji ya kubangaiza lakini ndo hivyo wazenji wenye roho ZA shetani wanawachomea VIBANDA biashara KIROHO MBAYA. hapa unahitaji roho YA PAKA kuendela kuvumilia kadhia kama hizi. hebu fikiria mtu akijitokeza kupinga muungano anahongwa cheo mfano hai ni DR. gHARIB bILAL. HUYU ANSEMEKAMANA KUMWAGA SUMU YA KUPINGA MUUNGANO LAKINI KIKWETE KAMCHOMOA LEO KANAWIRI UKIMWAMBIA HABARI YA KUVUNJA MUUNGANO HAWEZI KUKUBALI MAANA YEYE KAONJA RAHA YA UVC PRESIDENT. SASA TUTAENDELA KUWABEMBELEZA HAWA NYANGAU KWA STAHILI YA KUWAHONGA VYEO HADI LINI?
   
Loading...