Nini Faida ya kuoa au kuolewa na kabila lako?

Mkuu fanya sampling ya ndoa za same tribe na zenye different tribes. Utakuta ndoa za kabila moja wanaishi vizuri zaidi.
Upo sahihi kabisaa

xi xhua tumzgunch
Marehemu sita na mkewe magreti sita hawa wote wanyamwezi,zs makabila tofauti Ay kutoka Mbeya( Nyakyusa) na mkewe Mtusi wa Rwanda,Alikiba Muha na mkewe wa mombasa ,
Stamina na n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si kweli, ndoa ni maelewano ndani ya nyumba na kila mtu kumkubali na kijishusha kwa mwenza wake hiyo itadumu

Sent using Jamii Forums mobile app
Chunguza mkuu utakuja kuona ukweli huo
Marehemu sita na mkewe magreti sita hawa wote wanyamwezi,za makabila tofauti Ay kutoka Mbeya( Nyakyusa) na mkewe Mtusi wa Rwanda,Alikiba Muha na mkewe wa mombasa ,
Stamina na n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata ndani ya kabila lako siyo mwanamke yoyote atakufaa hapana ila angalau mtaendana baadhi ya vitu,Hujajiuliza kwanini ndoa za mababu zetu zilikuwa hazivunjiki hovyo kama za kwetu !

Sent using Jamii Forums mobile app
Wengi waliishi Kwa mazoea na si kwa mapenzi, pia ule uoga kwamba akiiondoka atadhalilisha na kutia aibu ukoo wao. Tambua bint akirudi nyumbani tayari kuna dosari familia inanyooshewa kidole kwamba pale si pa kuoa hawakai na waume. Nje wanamsifia kumbe hawajui kabeba mangapi moyoni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samson alipaswa kuoa wa kabila lake sio kwa msingi wa U kabila Bali kwa msingi wa Kiimani ( Waisrael kwa kuepusha kutoharibiwa Maadili yao yakidini iliwalizimu kuona wao kwa wao bila kuchangamana, nahiii iliendelea.



Kwa wazee , nisababu kwanza.. hakukua na maendeleo nahivo walikua hawana Means yoyote ya kuwatoa Mtwara hadi kuwafikisha Mwanza walipo watoto wakisukuma ........hii ikawafanya kama uko Mtwara utaoa hukohuko....


Pili, Tabia za kiasili zinazotokana na kabila, ilikua ukitaka kabila Fulani, wanajulikana kwa jambo hili...sasa zimwi linalokujua halikuli likakwisha.

Na ukazie, zamani Mfumo Dume ulitiwa mkazo.

Kwa sasa kila kitu Kimebadilika, usiangalie habari za ukabila wala nn..

Kama unataka kuoa, Omba Mungu, toka kutafuta, na lazima uyo mwanamke awe mcha Mungu, anayependa watu , anayejua Wazazi wako nikm wake , ndugu zako nikm zake zaidi ya yote, Asikae hata siku moja kmchezea Mama yako mzazi.


Hiki kizazi chetu, usipokua makini, utaoa jikeshupa kucha kukutenganisha na wazazi nandugu Nambaya zaidi kujaribu kuchukua nafasi ya Mama yako.
 
Hapana, ushauri wao ulihusu zaidi maendeleo. Ni rahisi kupata maendeleo ukioa kabila lingine tofauti na ukiwa umeoa kabila lako.
Ukioa kabila lako maendeleo hutapata au mbona marehemu mengi alioa kwao na alipata maendeleo mpaka mkewe kuja kutangulia mbele ya haki ndo kaoa muha
Labda hiyo pointi ya maendeleo uniambie kuwa uondoke home area ukasake life mbali so unaweza kuoa binti kule kwenu na kuja Dar kusaka life na mkeo na mkafanikiwa mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo wewe unajivunia uhayawani wa kutojua lugha yenu ya asili, khaaaa

xi xhua tumzgunch
Ipi hapo? Kabila lipi? Mkuu hayawani utakuwa wewe ambaye unanipa maneno ya kuniumiza moyo kwa kitu ambacho sikukipanga Mimi na hata wazazi wangu wamekikuta, wakati mwingine kabla hujaandika fikiria huyu mlengwa atapokeaje unachoandika, mtu asiuewaza hilo.mara.nyingi anakuwa hayawani. Mjadala na wewe umeisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ipi hapo? Kabila lipi? Mkuu hayawani utakuwa wewe ambaye unanipa maneno ya kuniumiza moyo kwa kitu ambacho sikukipanga Mimi na hata wazazi wangu wamekikuta, wakati mwingine kabla hujaandika fikiria huyu mlengwa atapokeaje unachoandika, mtu asiuewaza hilo.mara.nyingi anakuwa hayawani. Mjadala na wewe umeisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndo JF yenyewe hiyo kila mmoja na mawazo yake tuvumiliane tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu fanya sampling ya ndoa za same tribe na zenye different tribes. Utakuta ndoa za kabila moja wanaishi vizuri zaidi.
Upo sahihi kabisaa

xi xhua tumzgunch
Kwa uziefu wangu waliooana kabila tofauti wakifika miaka 50 hadi 60 na watoto wao walishakuwa na kipato Mama ujitenga na Baba na kukimbilia kwa watoto wake, baba naye ukimbilia kijijini nakuanza maisha mapya.Hiyo ni kwa familia zenye kipato cha kusuasua.
 
faida haipo kusema eti ukioa au kuolewa na mtu wa kabila lako kama kuna unafuu au llaa maana matatizo yenu wawili ya kiuchumi hayatatuliwi kuwa katika kabila moja mababu zetu walisisitiza kwasababu hawakuwa na uwezo wa kuona mbali inavyotakiwa.
Ni kweli kabisa mkuu.
Hao watu wa zamani hawakuwa na mawazo na challenges kama tulizonazo sasa hivi.
akili yao iliishia tu kwenye kumiliki mashamba na kugawana majukumu ya kulima hakuna cha zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukioa kabila lako maendeleo hutapata au mbona marehemu mengi alioa kwao na alipata maendeleo mpaka mkewe kuja kutangulia mbele ya haki ndo kaoa muha
Labda hiyo pointi ya maendeleo uniambie kuwa uondoke home area ukasake life mbali so unaweza kuoa binti kule kwenu na kuja Dar kusaka life na mkeo na mkafanikiwa mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimeiongelea kwa muktadha wa kuondoka mbali na home kusaka maisha, ikitokea ukakutana wa kabila lako ni vizuri zaidi.
 
Inategemea kama familia yenu ina ukabila bado au la....

wakabila wanaweza pata tabu kukubali mtu mpya..kila ukifanya kitu lazma kionekane tofauti

wasiojali sana wataona huyu ni mpya basi tumchukulie kama alivyo hajui ya kabila yetu na sie hatujui ya kwao...hapo kikubwa upendo na ubinadamu.,
 
Sioni mbaya kuchanganya makabila kuna Uzi nilieleza humu, wazazi wangu hawajatoka kwenye kabila moja, Baba wazazi wake wametofautiana kabila na mama yangu naye wazazi wake vile vile. Sasa hao wajukuu ambao ni watoto wetu na watoto wa watoto wetu, hatuna lugha tuzoongea za asili nyumbani zaidi ya hizi tunazozikuta shule yaani lugha ya Taifa na ya Biashara, hii ya kabila moja imepitwa na wakati tena naona wengine ni kama wamefuata mkumbo kuoa kabila lake baadae anajutia sasa ukute awe yule dini moja mke mmoja ni shida bora wale ambao wanaruhusiwa kuongeza mke angalau atapata faraja akiongeza

Sent using Jamii Forums mobile app

Aisee,look at this!

Kwahiyo nyie hamna kabila tena!

Kabila lenu ni Waswahili!

The Swahilis!

Mmepoteza traditions za ancestors wenu wa more than 10,000years na halafu you are proud kabisa!

Aiseee
 
Back
Top Bottom