Nini Faida ya kuoa au kuolewa na kabila lako?

Last KING Ontuzu

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
585
778
Wengi wenu nadhani mshawahi kukutana na pingamizi za ndugu na wazazi linapokuja suala la kuolewa au kuoa mtu fulani ambaye ni mtu wa jamii tofauti na yako namaanisha kabila tofauti.

Mambo haya yapo tangu enzi za mababu zetu ukiangalia ndani ya biblia utakutana na habari za akina Samsoni alipotaka kumuoa Delila mwanamke wa kabila tofauti na lake.
Japo kwa miaka ya hivi karibuni jambo hilo linaonekana kupitwa wakati.

Suala la kujiuliza je kitu gani hasa ambacho wazee wetu walitaka tukipate kwa kuoa wanawake wa kabila moja ?

Na je kipi cha kupoteza unapoamua kuoa jamii tofauti na yako?

Maoni yenu wadau

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni Mjadala Mzuri

Kipindi hicho Interaction za jamiii hazikua kubwa Sana Kama ilivyo Sasa.
Hiyo ndio Sababu kubwa

Nadhani ni urahisi tuu wa kuelewana baina ya pande Mbili, Labda kudumisha ukabila
.
Binafsi navutiwa Sana Sana na Mtu mwenye asili ya Ninapotokea wala sio ushamba
 
Kwa sababu mnafanana tamaduni na unakuwa comfortable zaidi, ndugu wa mume utawaona ndugu zako tu tofauti na hapo utakuwa kama stranger. Ni mtazamo wangu tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo unakuta mama mkwe au baba mkwe kaja unaanza kubabaika bila kujiamini ufanyacho ni sahihi au sio sahihi kwa tamaduni za ukweni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ma
Wengi wenu nadhani mshawahi kukutana na pingamizi za ndugu na wazazi linapokuja suala la kuolewa au kuoa mtu fulani ambaye ni mtu wa jamii tofauti na yako namaanisha kabila tofauti ,
Mambo haya yapo tangu enzi za mababu zetu ukiangalia ndani ya biblia utakutana na habari za akina Samsoni alipotaka kumuoa Delila mwanamke wa kabila tofauti na lake.
Japo kwa miaka ya hivi karibuni jambo hilo linaonekana kupitwa wakati.

Suala la kujiuliza je kitu gani hasa ambacho wazee wetu walitaka tukipate kwa kuoa wanawake wa kabila moja ?

Na je kipi cha kupoteza unapoamua kuoa jamii tofauti na yako?

Maoni yenu wadau

Sent using Jamii Forums mobile app
mada yako ni nzuri LAST KING Ontuzu
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom