Pole sana. Ukweli ni kwamba inauma sana kwa mzazi kuwa na mtoto shoga. Mzazi kama mzazi hufurahia pale anapojaliwa kupata mtoto wa kiume na kumlea hadi afikie kuwa baba na wa kike na kuwa mama. Tofauti na matarajio hayo huleta uchungu mzito moyoni.
Kuna baadhi ya mambo ambayo mzazi ni lazima ayajue/ayaangalie wakati wa kulea watoto wake.
1. Chunguza na kujua tabia za watoto wako tangu wakiwa wadogo/wachanga
2. Chunguza uwezo wao kiakili, afya zao, utendaji kazi wa milango yao ya faham, homon zao n.k.
3. Andaa mazingira mazuri ikiwa ni pamoja na kujua wanapenda michezo gani, wanacheza na nani, wapi, wakati gani, watu wanaoshinda nao nyumbani na shuleni wana tabia gani, wanalala katika mazingira gani. Chunguza haya kadri siku zinavyoenda nao wanavyozidi kukuwa na kubadilika kimaumbile.
Kuna wakati mwingine kwa kufanya hivi kunaweza kusaidia kuzuia uwezo wa watoto wa kupokea tabia mbaya kutoka kwa wengine. Ni vizuri kukaa na kuongea na watoto kuhusu tabia mbalimbali zinazoweza kuwasaidia au kuwapotosha.
Kwa bahati mbaya, ikitokea umegundua tabia kama hizi za ushoga, bado usisite kuongea na mtoto, kipindi hiki huna sababu ya kuwa mkali hadi utakapopata taarifa kamili za sababu zilizopelekea yeye kuwa shoga. Kama ni vishawishi na vitisho, au ni kwa kuona na kutaka kujaribu mchezo huo, au ni kujisikia na kupenda kufanya hivvyo. Jambo hili si rahisi, unaweza kuwashirikisha watoa ushauri nasaha maana kama mtoto amefikia kuwa shoga, hatua za haraka zenye uhakika zinapaswa kuchukuliwa ili kumtoa kwenye tabia hizi, la sivyo utampoteza kabisa.
Naandika hapa kama mzazi, jambo hili limenigusa, sina utaalamu sana katika hili. Ila usiache kutafuta msaada kwa wataalamu.