Nini chimbuko la Vita vya Uhujumu Uchumi - 1983-84?

Nini chimbuko la Vita vya Uhujumu Uchumi - 1983-84?

Nashauri kwamba ni vizuri kuionesha sheria hiyo ili tuweze kuikosoa sawasawa, kwani hadi hivi sasa hakuna ushahidi ulioletwa wa mapungufu ya sheria hiyo.Itafute halafu uje uioneshe ina makosa gani katika suala la soko. Kinachonishangaza zaidi hakuna aliyejaribu kuiweka sheria hiyo hapa na watu wakaichambua na kuonesha mapungufu yake. Aidha sheria ilikuwa na makosa au utekelezaji ulikuwa na makosa. Ninavyoona wengi wanapinga jinsi Operesheni ilivyoendeshwa. Wale wanaoipinga sheria hawajafafanua hasa mapungufu ya sheria hiyo ni yapi kwa kuonesha ushahidi wa wazi.

La pili, ni hatari kuisoma historia kwa vipande bila kuiunganisha. Leo hii mtu akisimama na kusema matatizo ya uchumi wa dunia yalianza mwishoni mwaka 2008 na chanzo chake kilikuwa ni kati ya 2007/2008 na akajikita kuangalia historia kwa kipindi hicho hafanyi haki kwa dhamira yake na wala kwa utashi wake. Wana historia ya kiuchumi wataangalia kiini cha chanzo cha matatizo ya kiuchumi wengine wanaenda nyuma hadi miaka ya utawala wa Clinton! Nimekaa pembeni kuangalia mjadala huu na kwa kiasi kikubwa watu wamebakia kuangalia mwaka 1983/1984 kana kwamba matukio hayo yalitokea katika ombwe. Waheshimiwa wengi wanazungumza kwa umakini na umahiri mkubwa lakini wanakwepa kupenya kwenye kingo za historia. Kuna mtu anajua ugavi wa bidhaa nchini ulikuwaje mwaka 1983/1984 na mahitaji yalikuwaje na hicho kilisabaishwa na nini? Hapa wasomi wetu wangetusaidia.

La tatu, ni jaribu la kuonesha kuwa Nyerere (Rais) na Sokoine (Waziri Mkuu) waliiamka tu alfajiri moja na kuanza kamata kamata; kwamba hawakuna na taarifa zozote aidha za kijasusi au za kiuchumi zilizosababisha maamuzi yao; kwamba wao wawili walijiamulia tu "hey Mr. President lets go and kamata walanguzi"! Really? Kwamba sisi leo miaka karibu thelathini baadaye tuna taarifa za uhakika kuwa yaliyokuwa ni "mawazo ya Nyerere na Sokoine"! I know some of us have an insatiable proclivity to arrogance, but I didn't think it'd be by this much! Kweli Nyerere na akili zake timamu aliamua tu kuanzisha operesheni kwa sababu anajisikia na hana msingi wowote isipokuwa wivu, chuki, ignorance of realities on the ground! Oh yeah? Ila sisi leo ndio tunajua "what actually happened" bila kuonesha angalau empirical data kwamba "hii x,y, na z ndivyo ilivyokuwa wakati ule na Nyerere hakujua hili"!

Oh well!... wengine yawezekana ni vigumu kutazama masuala ya uhujumu uchumi ya miaka ile kwa sababu familia zetu ziliathirika n.k Bahati nzuri ninakumbukumbu nzuri tu ya wafanyabiashara wa Tanga waliokuwa wanachimbia bidhaa nje ya majumba yao na wengine kutengeneza false doors... sizungumzii nilichosikia.. Ukiingia kwenye duka lao hakuna kitu; ila ukitaka kitu fulani unalipa fedha zaidi wanaenda kuchukua wanakujua wao wenyewe. Na walipozukiwa na vyombo vya dola.... hawakuwa na jjinsi ya kuelezea ndiyo maana siyo wote walioshitakiwa kwenye makosa ya kuhujumu uchumi wote waliachiliwa!

Now, ukija kwenye suala la jinsi lilivyotekelezwa huo ni mjadala mwingine all together kwani sijaona hadi leo hii nchi ambayo imeweza kuendesha operesheni yoyote ile na wananchi wake WOTE wakashangilia!

BTW: Nimeambatanisha hapa sheria nzimaya Uhujumu Uchumi na Mabadiliko yake.

Mwanakijiji:

Nimeipitia kwa haraka. Na kuna uwezekano mkubwa kwa mafisadi kuhukumiwa kwa kutumia sheria hii bila ya kutafuta sheria zingine. Ukweli ukiwa fisadi umehujumu uchumi.

Na kuhusu wauzaji wa mafuta, soko la mafuta liko huru na ni complex. External factors zinachangia sana bei ya mafuta kuliko intents za wafanyabiasha.

Kuhusu Nyerere na Sokoine kuchemsha. Big time walichemsha. Wao walikuwa na moral obligations lakini principal za uchumi wazikiuka. Hii ni sawa na kuwafungia watu gerezani na kushindwa kuwapa chakula. Hapo itatokea cannibalism tu.
 
"Mikingamo... Sasa vita vimetangazwa jama, wananchi wote tuwe imara, vijijini na mijini tusisite kuwafichua wahujumu na walanguzi"

Nini kulikuwa chimbuko la kuanzishwa kwa vita dhidi ya wahujumu uchumi, walanguzi na wafanya magendo?

Sheria ya Uhujumu Taifa ya mwaka 1984 bado iko hai, kwa nini haitumiki?

Uchumi wa kijamaa, uhujumu uchumi na sheria ya uhujumu uchumi ya wakati huo yote ni motokeo ya njia potofu ambazo viongozi wa Juu wa Serikali ya CCM wamekuwa wakichukua ili kuleta maendeleo kwa watu ama kutatua matatizo. Mpaka hapa tulipo bado CCM hawajawa serious na issues za uchumi.
 
Kuhusu Nyerere na Sokoine kuchemsha. Big time walichemsha. Wao walikuwa na moral obligations lakini principal za uchumi wazikiuka. Hii ni sawa na kuwafungia watu gerezani na kushindwa kuwapa chakula. Hapo itatokea cannibalism tu.


kauli yako hii haina msingi katika historia, ushahidi usiopingika na haiwezi kusimama ikiangaliwa kwa karibu kama kwa darubini. Imejengwa kutokana na hisia na ambayo msingi wake ni matamanio ya kitu kisichokuwapo. Hakuna kanuni ya uchumi waliyokiuka isipokuwa kama ni ya kufikirika.

Unless unaweza kutuambia hali ya ugavi na mahitaji ilikuwaje mwanzoni mwa miaka ya themanini na ilisababishwa na nini.

a. Kwamba kulikuwa na ugavi wa kutosha kwa hiyo wazo la upungufu wa ugavi lilikuwa ni la kubuni?

b. Kwamba, kulikuwa hakuna mahitaji ya bidhaa hivyo ugavi ulizidi mahitaji na hivyo bei ilikuwa ya chini (si kweli kwamba kulikuwa na bei ya 'kuruka')

c. Kwamba mahitaji yalikuwa ya juu na ugavi ulikuwa wa juu na hivyo bei iliakisi hali halisi ya soko na hivyo madai kuwa kulikuwa na upungufu wa makusudi wa bidhaa ni ya uongo?

d. Kwamba, mahitaji ya ndani ya nchi yaliweza kutoshelezwa na bidhaa zinazozalishwa nchini na hivyo hakukuwa na haja ya kuingiza bidhaa kutoka nje?

e. Kwamba, mahitaji ya ndani yaliweza kabisa kutoshelezwa na ziada ndiyo iliyopelekwa nje ya nchi na hivyo hakukuwa na msingi wa kuzuia biashara ya "njia za panya"?



Ni kanuni gani ya uchumi ambayo Sokoine na Nyerere waliivunja!?
 
Mwanakijiji:

Nimeipitia kwa haraka. Na kuna uwezekano mkubwa kwa mafisadi kuhukumiwa kwa kutumia sheria hii bila ya kutafuta sheria zingine. Ukweli ukiwa fisadi umehujumu uchumi.

Kwamba umeipitia kwa haraka lakini una uthubutu wa kuihukumu inashangaza. Napata moyo kuwa katika haraka hiyo umekubali kuwa sheria hiyo inafaa kushughulikia wahujumu uchumi!
 
Mzee Mwanakijiji,
Believe me 20 yrs from now kuna watu watasema JK alikuwa mbumbumbu na mjinga kupitisha sheria hizi za Uhujumu uchumi, hata maswala ya EPA, Richmond na kadhalika ni blaaa blaa blaa, wataua kishenzi na kutungiwa hata hadithi yake...
Hawa wote mkuu wangu walikuwa watoto wa friji Open...wazee wao wakitumia zile Landrover na bendera za chama kufuata magunia ya mchele Kyela..Hawakumbuki ama hawakupata kuona jinsi mali ilivyokuwa ikitupwa baharini wengine wakizika mali na hela utafikiri anazikwa mtu...

Mkandara hicho unachosema ndicho kinaitwa "fabrication of history". Miaka ishirini ijayo watu wasema mwaka 2008 kulikuwa na ufisadi na kitendo cha aliyekuwa rais JK kuwapeleka mahakamani watuhumiwa wa ufisadi (ambao wataachiwa wengi wao) kilikuwa ni cha uonevu. Watathibitisha hayo pale watuhumiwa watakaporudishiwa mali zao.

Binafsi naamini yaliyotokea mwaka 84 yanathibitisha utawala wa sheria ulivyokomaa, kwani licha ya wananchi wengi kupelekwa "mikingamo" walikilimbilia mahakamani na ni mahakama zetu ziliona katika kesi kadhaa sheria haikufuatwa. Hilo siyo mara ya kwanza, liliwatokea kina Hemedi (wale wa Polisi); limetokea kwa kina Kiula; limetokea kwa waliotuhumiwa ujambazi wa bilioni mbiil n.k!

Sasa kama Mahakama isingefuatwa au ingelazimisha wananchi wasirudishiwe mali zao licha ya ushahidi wa uonevu ndio tungesema wameonewa. Lakini sheria ndivyo inavyofanya kazi wakati mwingine magurudumu yake yanaenza kama zig zag!

Ukiangalia hata kwenye mataifa makubwa, mtu anaweza kuonewa na vyombo vya chini na akakata rufaa hadi mahakama ya juu kabisa na akapata haki! Mfano mzuri yule jamaa wa Canada aliyefanyiwa rendition (nadhani alipelekwa Syria) kwa makosa.. lakini alilia haki yake hadi akaombwa msamaha! na sasa anadai fidia yake!

Sasa itashangaza sana kusema kuwa kwa vile jamaa wa Canada kakutwa hana hatia na alionewa ina maana hakuna watu wenye nia mbaya na Marekani au mataifa mengine. Kwa vile mtu mmoja kwa kutumia sheria ile ile amekutwa hana hatia haina maana watu wengine hawakufanya makosa na kuvunja sheria ile ile!

Kwa vile kuna waliotuhumiwa uhujumu uchumi walikutwa hawana hatia na wakalipwa fidia ya shilini milioni 800 hivi HAINA maana hakukuwa na wahujumu uchumi mwaka ule! Hii reasoning ambayo inaonekana humu inashangaza! Ati kwa vile watu walikutwa hawana hatia basi ina maana hakukuwa na uhujumu uchumi! what kind of reasoning is that!?
 
kauli yako hii haina msingi katika historia, ushahidi usiopingika na haiwezi kusimama ikiangaliwa kwa karibu kama kwa darubini. Imejengwa kutokana na hisia na ambayo msingi wake ni matamanio ya kitu kisichokuwapo. Hakuna kanuni ya uchumi waliyokiuka isipokuwa kama ni ya kufikirika.

Unless unaweza kutuambia hali ya ugavi na mahitaji ilikuwaje mwanzoni mwa miaka ya themanini na ilisababishwa na nini.

a. Kwamba kulikuwa na ugavi wa kutosha kwa hiyo wazo la upungufu wa ugavi lilikuwa ni la kubuni?

b. Kwamba, kulikuwa hakuna mahitaji ya bidhaa hivyo ugavi ulizidi mahitaji na hivyo bei ilikuwa ya chini (si kweli kwamba kulikuwa na bei ya 'kuruka')

c. Kwamba mahitaji yalikuwa ya juu na ugavi ulikuwa wa juu na hivyo bei iliakisi hali halisi ya soko na hivyo madai kuwa kulikuwa na upungufu wa makusudi wa bidhaa ni ya uongo?

d. Kwamba, mahitaji ya ndani ya nchi yaliweza kutoshelezwa na bidhaa zinazozalishwa nchini na hivyo hakukuwa na haja ya kuingiza bidhaa kutoka nje?

e. Kwamba, mahitaji ya ndani yaliweza kabisa kutoshelezwa na ziada ndiyo iliyopelekwa nje ya nchi na hivyo hakukuwa na msingi wa kuzuia biashara ya "njia za panya"?



Ni kanuni gani ya uchumi ambayo Sokoine na Nyerere waliivunja!?

Mwanakijiji:

Nashukuru kwa kuleta points ambazo kuichambua mada kidogo kwa undani. Kila siku tukiboronga tuna kisingizio kuwa Roma haikujengwa kwa siku moja. Pamoja na kwamba haikujengwa kwa siku ni lazima watawala wa Roma walipitia misukosuko fulani. Na kutokana na misukosuko hiyo waliweza kutafuta ufumbuzi ambao umefanywa Roma isijengwe kwa siku moja.

Kanuni za kiuchumi walizonazo Nyerere and Inc. zilikuwa ni za kufikirika japokuwa zilikuwa na nia nzuri. Bidhaa zilizokuwa pungufu ni bidhaa za kutengenezwa viwandani. Historia inaonyesha kuwa Tanzania haikuwa mzalishaji wa bidhaa za viwandani. Bidhaa nyingi za matumizi ya ndani zilitoka Kenya.

Hivyo katika miaka 1970 kulikuwa sera za kuongeza uzalishaji wa bidhaa ndani ya nchi. Na sera hii ilipata msukumo mkubwa baada ya kuvunjika kwa EAC. Na kutokana na ukweli kuwa tulikuwa ni taifa la kijamaa, viwanda vingi vilivyojengwa vilikuwa vya serikali.

Mpaka sasa nimesha-establish kuwa serikali ilikuwa na nia nzuri ya kuanzisha viwanda. Lakini nia nzuri na utekelezaji wa nia nzuri ni vitu viwili tofauti. Nitakupa mfano mmoja.Kulikuwa na viwanda vya nguo kama vile Mwatex, Mutex na viwanda vya nyuzi vilivyopangwa kujengwa Tabora. Viwanda hivi vilikuwa na nia nzuri lakini kiuchumi vilikuwa haviko katika nafasi ya kushamili. Umeme ni kitu muhimu. Viwanda vilikuwepo katika sehemu ambazo hazina nguvu za umeme wa kutosha. Matokeo ya production ilikuwa ndogo au pale production ilipokuwa kubwa basi cost za uzalishaji ziliongezeka.

Hivyo kwa sehemu kubwa siasa ilitawala uendeshaji wa vitu vilivyotakiwa kuwa vya kiuchumi.

Vilevile uendeshaji wa shughuli za kibiashara ni lazima utegemee expertise ya mambo hayo. Nia ilikuwa nzuri, lakini watanzania bado tulikuwa hatuna wataalamu wa kuongoza mashirika ya uzalishaji au usambazaji. Kwenye taaluma ya biashara wanasema thamani ni kitu kinachoongezwa katika bidhaa au huduma ambacho mteja anaweza kulipia. Kwa mfano sabuni ya OMO na FOMA zinatengenezwa kwa basic raw materials zilezile lakini ukiona mtu anaacha kununua FOMA iliyotengenezwa Tanzania na kukimbia OMO iliyotengenezwa Kenya ujue kuwa kuna thamani iliyoongezwa katika OMO. Thamani hiyo inaweza kuwa ya kipumbavu tu kama vile matangazo ya biashara au packaging materials lakini ni thamani.

Pamoja na hayo yote kulikuwepo na vita vya Uganda. Vita hivi vilitumia pesa za kigeni nyingi. Miundo mbinu yetu ilikuwa inategemea pesa za kigeni. Hivyo kukosekana kwa pesa za kigeni kuriathiri uzalishaji nchini.

Waanzilishi wa sera hawakuwa na nia mbaya kwa taifa. Lakini maendeleo ya jamii au uchumi sio mbio za kwenye mstari ulionyooka. Hivyo stay the course haikuwa sera nzuri ya ku-deal na matatizo yaliokuwa yanajitokeza. Hivyo mnaweza kuwatetea viongozi mnavyotaka lakini stay the course iliharibu uchumi wetu kwa sehemu kubwa.

Kuna uwezekano fulani kuwa kulikuwepo na njama za kuipindua serikali. Lakini hiyo ni package ya kuwa nchi ya kiAfrika. Hata Kenya serikali ilitaka kupinduliwa.

Vilevile Zambia walikuwa na sera ya viwanda vya serikali kama sisi. Na wao walipata matatizo yaleyale tuliokuwa nayo ya uhaba wa bidhaa. Hivyo badala ya kuangalia wafanyabiashara kama wakosefu ni muhimu kuziangalia sera zenyewe kwa sababu hii ni Phenomena iliyotokea katika nchi nyingi zilizotaka kuwa na viwanda lakini hazikuwa na sera nzuri.
 
Kwamba umeipitia kwa haraka lakini una uthubutu wa kuihukumu inashangaza. Napata moyo kuwa katika haraka hiyo umekubali kuwa sheria hiyo inafaa kushughulikia wahujumu uchumi!

Nikisoma Biblia leo ninaweza kusema inaweza kutumika kuwahukumu mafisadi. Nikisoma Koran ninaweza kusema kuwa inaweza kutumika kuwahukumu mafisadi. Na hata nikisoma sheria zilizokuwepo kabla ya hii bado naweza kusema kuwa inaweza kutumika.

Kuwa na milolongo ya sheria haifanyi taifa au jamii kupiga hatua kimaendeleo. Kuna tools nyingi zinazoweza kufanya nchi ipate maendeleo na kujenga tabia ya kuwajibika.

Mkapa alileta sera zake za uwazi. Sidhani kama kuna mtanzania atayekubaliana kuwa Mkapa alikuwa muwazi.

Je mikataba yote ingekuwa inafanyika katika misingi ya uwazi, si tusingekuwa mbali?

Uwazi ni moja ya tool nzuri.
 
Mwanakijiji:

Nashukuru kwa kuleta points ambazo kuichambua mada kidogo kwa undani. Kila siku tukiboronga tuna kisingizio kuwa Roma haikujengwa kwa siku moja. Pamoja na kwamba haikujengwa kwa siku ni lazima watawala wa Roma walipitia misukosuko fulani. Na kutokana na misukosuko hiyo waliweza kutafuta ufumbuzi ambao umefanywa Roma isijengwe kwa siku moja.

Kisingizio ni sababu ya udhuru isiyo na msingi katika ukweli lakini inayoonekana yaweza kuwa kweli. Kina lengo cha kutoa maelezo ya kufikirika ambayo yakiangaliwa hayatokani na ukweli. Kwamba Roma haikujengwa kwa siku moja ni ukweli! Kwanini haikujengwa kwa siku moja mtu anaweza kutoa kisingizio au sababu. Mtu akisema kuwa ilikuwa hivyo kwa sababu Waroma walikuwa wanapenda kunywa pombe atakuwa anatoa kisingizio na siyo sababu.

Kanuni za kiuchumi walizonazo Nyerere and Inc. zilikuwa ni za kufikirika japokuwa zilikuwa na nia nzuri.

Hiki ndicho kisingizio!

Bidhaa zilizokuwa pungufu ni bidhaa za kutengenezwa viwandani.

Ni rahisi kutoa kauli hii bila kuonesha angalau msingi wake. Unaposema "bidhaa zilizokuwa pungufu ni bidhaa za kutengenezwa viwandani" msingi wa kauli hiyo ni nini? Ulijuaje kuwa kulikuwa na upungufu wa bidhaa za viwandani na siyo za kilimo, ziyo za kuingizwa nchini n.k?

Historia inaonyesha kuwa Tanzania haikuwa mzalishaji wa bidhaa za viwandani. Bidhaa nyingi za matumizi ya ndani zilitoka Kenya.

Kauli yako hiyo tena ni too general na inapingana na maelezo yako mengine. Tulipofika mwaka 1984 Tanzania ilikuwa tayari na viwanda mbalimbali vya bidhaa za ndani. Unaposema kuwa "Tanzania haikuwa mzalishaji wa bidhaa za viwandani" unatutania.

- Tulikuwa na kiwanda cha Chuma Tanga
- Tulikuwa na kiwanda cha ngozi
- Tulikuwa na viwanda vya nguo (Mutex, Mwatex, Sunguratex, Urafiki, n.k)
- Tulikuwa na kiwanda cha Mbolea Tanga
- Tulikuwa na kiwanda cha zana za kilimo (UFI Ubungo) n.k
- Kulikuwa na kiwanda cha Chai Bora
- Kulikuwa na kiwanda cha FOMA
- Tulikuwa na TANBOND
- Tulikuwa na kiwanda cha sabuni cha Mbuni, Malaika, n.k
- Kulikuwa na kiwanda cha kusindika matunda pale Korogwe
- Tulikuwa na kiwanda cha "Viatu Bora"!

Naweza kuendelea kutaja viwanda vilivyokuwa mikoa mingine (Arusha, Morogoro n.k); viwanda hivyo vilikuwa vinadhalisha "bidhaa za viwandani"! Unless una maana nyingine ya "bidhaa za viwandani". Kwa hiyo SIYO KWELI kwamba "Tanzania haikuwa mzalishaji wa bidhaa za viwandani". Suala la kiasi na ubora hilo jingine.

Hivyo katika miaka 1970 kulikuwa sera za kuongeza uzalishaji wa bidhaa ndani ya nchi. Na sera hii ilipata msukumo mkubwa baada ya kuvunjika kwa EAC. Na kutokana na ukweli kuwa tulikuwa ni taifa la kijamaa, viwanda vingi vilivyojengwa vilikuwa vya serikali.

Hili silo la ajabu duniani, na kuwa taifa la kijamaa haina maana viwanda haviwezi kumilikiwa na serikali. Tunajifunza leo katika uchumi wa dunia jinsi gani serikali mbalimbali duniani zinaanza kurudi katika sekta za uzalishaji na kusimamia uchumi wao.

Ninavyoandika Serikali ya Marekani imetoa mkopo wa karibu bilioni 6 kwa GMAC na sharti mojawapo ni serikali kuwa na hisa/ubia wa aina fulani. Hilo liko hata kwenye bailout ya makampuni ya magari.

So, serikali kujihusisha na uzalishaji inaonekana siyo suala la ujamaa peke yake na kama wao wanafanya 2008 na sisi tulifanya in the 70s it seems we were way ahead of the times! Na ndio maana wengine bado tunaamini kuwa mojawapo ya mambo yaliyochochea ufisadi ndiyo haya ya kuacha watu wajifanyie mambo yao wakitegemea "soko" litasawazisha mambo yote. Wrong we were!

Mpaka sasa nimesha-establish kuwa serikali ilikuwa na nia nzuri ya kuanzisha viwanda. Lakini nia nzuri na utekelezaji wa nia nzuri ni vitu viwili tofauti.

Hii ni point nzuri lakini flawed. Nia nzuri haina uhusiano wa moja kwa moja na utekelezaji mzuri. Mtu anaweza kuwa na nia nzuri ya kujenga nyumba lakini kama hajui mambo yote ya ujenzi na kinachotakiwa kujenga nyumba hiyo anaweza akajenga kile anachodhania ni "nyumba nzuri" lakini kumbe anajenga kwenye eneo lenye tetemeko la ardhi! Mtu anaweza kutekeleza kwa uzuri kabisa kitu kibaya!

Nitakupa mfano mmoja.Kulikuwa na viwanda vya nguo kama vile Mwatex, Mutex na viwanda vya nyuzi vilivyopangwa kujengwa Tabora. Viwanda hivi vilikuwa na nia nzuri lakini kiuchumi vilikuwa haviko katika nafasi ya kushamili.

Hapa kuna ukweli wa aina fulani. Lakini kwanini havikuweza kushamili tatizo halikuwa katika uchumi tu lakini pia katika utendaji. Leo hii tunavyoshuhudia makampuni mbalimbali yanaendeshwa, nashangaa jinsi gani tuliweza hata kusurvive! Kama hawa leo pamoja na umeme, teknolojia n.k wanaboronga kwenye ATCL na Tanesco hivi miaka ile ya themanini ilikuwaje? Mbona leo tuko kwenye mazingira mazuri zaidi je tumeweza kufanya bora zaidi!?

Umeme ni kitu muhimu. Viwanda vilikuwepo katika sehemu ambazo hazina nguvu za umeme wa kutosha. Matokeo ya production ilikuwa ndogo au pale production ilipokuwa kubwa basi cost za uzalishaji ziliongezeka.

Hivi leo umeme upo wa kutosha? Sijui kama unajua kuwa wengine wetu hatukumbuki wakati wowote miaka ya themanini (kwenye mikoa iliyokuwa kwenye gridi) kukiwa na mgao wa umeme? Sikumbuki kata kata ya umeme. Wakati ule kama ulikuwa na umeme basi ndio unao kama hauna hauna! Haya ya kusema umeme "ulikuwa na nguvu kidogo" sijui yametoka wapi. Embu tupatie mfano wa kiwanda kilichojengwa mahali ambapo umeme ulikuwa na nguvu kidogo.

Kuhusu "pale production ilipokuwa kubwa basi cost za uzalishaji ziliongezeka". Kwa wana uchumi kuna kile wanakiita "law of diminishing returns". Kwanini katika ulimwengu wako kuzalisha vitu vingi kuongeze gharama badala ya kupunguza? Unless unataka kusema vile vilivyozalishwa havikununuliwa (kitu ambacho kitatufanya tujiulize kwanini?)

Hivyo kwa sehemu kubwa siasa ilitawala uendeshaji wa vitu vilivyotakiwa kuwa vya kiuchumi.

Dunia nzima ndivyo inavyofanywa; siasa na uchumi ni kama lila na fila!


Vilevile uendeshaji wa shughuli za kibiashara ni lazima utegemee expertise ya mambo hayo. Nia ilikuwa nzuri, lakini watanzania bado tulikuwa hatuna wataalamu wa kuongoza mashirika ya uzalishaji au usambazaji.

Hivi leo tunao? Tatizo la wakati ule halikuwa utalaamu hasa miaka ya mwisho wa sabini na themanini. Miaka ya mwanzo ya uhuru tunaweza kutoa kisingizio hicho kwani ni kweli hatukuwa na wataalamu. Lakini inapofika mwisho wa sitini, sabini na themanini karibu watalaamu wengi (wasomi wa vyuo vikuu) walikuwa kwenye nafasi mbalimbali.

Cha kushangaza ni kuwa hata leo tunaletewa kisingizio kile kile "hatuna wataalamu"! Kuna tatizo mahali fulani katika fikra zetu. Ila wakija wazungu wenye taaluma ile ile kama hawa wenzetu, hao tutawakumbatia na kuwaita "Wataalamu!" Tatizo la Tanzania halikuwa watalaamu!

Kwenye taaluma ya biashara wanasema thamani ni kitu kinachoongezwa katika bidhaa au huduma ambacho mteja anaweza kulipia. Kwa mfano sabuni ya OMO na FOMA zinatengenezwa kwa basic raw materials zilezile lakini ukiona mtu anaacha kununua FOMA iliyotengenezwa Tanzania na kukimbia OMO iliyotengenezwa Kenya ujue kuwa kuna thamani iliyoongezwa katika OMO. Thamani hiyo inaweza kuwa ya kipumbavu tu kama vile matangazo ya biashara au packaging materials lakini ni thamani.


Kuna ukweli wa aina fulani, lakini pia mtu kukimbilia bidhaa moja kwenda nyingine haina maana hiyo anayoikimbilia ina thamani zaidi. Pia kwa vile bidhaa zinatengenezwa kwa malighafi ile ile haina maana zinatengenezwa kwa gharama ile ile! Sitapenda kutoa somo la biashara ambalo sina ujuzi nalo lakini akili yangu inaniambia kuwa kitu chochote kitauzwa kulingana na gharama zilizoingia kukitengeneza kitu hicho. Malighafi ni gharama mojawapo tu! kuna vitendea kazi, nguvu kazi, n.k So, ukikuta kitu cha Tanzania kinauzwa kwa bei rahisi na kitu cha kenya kinauzwa kwa bei ghali mtu atafikiria (kama unavyofanya wewe) kuwa kile cha kenya kina thamani zaidi!

Pamoja na hayo yote kulikuwepo na vita vya Uganda. Vita hivi vilitumia pesa za kigeni nyingi. Miundo mbinu yetu ilikuwa inategemea pesa za kigeni. Hivyo kukosekana kwa pesa za kigeni kuriathiri uzalishaji nchini.

Kwa mara ya kwanza umetoa sababu! Hivi unajua ni gharama ya kiasi gani ilitumika kwenye vita vya Uganda? Ni nchi gani katika historia ya wanadamu imetoka vitani na mara moja ikawa katika mafanikio? Je wakati nchi iko vitani hali ya uzalishaji na ugavi wa bidhaa mbalimbali unakuwaje? Je yawezekana "kukosekana pesa za kigeni kuriathiri uzalishaji nchini" na matokeo yake yalikuwa ni upungufu wa bidhaa, na kile kidogo kikaanza kulanguliwa and hence trigger vita ya uhujumu uchumi?
Waanzilishi wa sera hawakuwa na nia mbaya kwa taifa. Lakini maendeleo ya jamii au uchumi sio mbio za kwenye mstari ulionyooka. Hivyo stay the course haikuwa sera nzuri ya ku-deal na matatizo yaliokuwa yanajitokeza.

Hakuna aliyesema "stay the course". Ndio maana mambo yalibadilishwa! Watu walienda mahakamani, mipango ilipangwa upya. Kama hukumbuki huko nyuma tulikuwa na msimamo wa "kupanga ni kuchagua, na kuchagua ni kupangua".

Hivyo mnaweza kuwatetea viongozi mnavyotaka lakini stay the course iliharibu uchumi wetu kwa sehemu kubwa.

Bahati nzuri unayewatetea viongozi ni wewe kwani unaonesha kuwa walichofanya kuwa sahihi. Bado sijaanza kuwatetea viongozi wa wakati ule!

Kuna uwezekano fulani kuwa kulikuwepo na njama za kuipindua serikali. Lakini hiyo ni package ya kuwa nchi ya kiAfrika. Hata Kenya serikali ilitaka kupinduliwa.

and????


Vilevile Zambia walikuwa na sera ya viwanda vya serikali kama sisi. Na wao walipata matatizo yaleyale tuliokuwa nayo ya uhaba wa bidhaa. Hivyo badala ya kuangalia wafanyabiashara kama wakosefu ni muhimu kuziangalia sera zenyewe kwa sababu hii ni Phenomena iliyotokea katika nchi nyingi zilizotaka kuwa na viwanda lakini hazikuwa na sera nzuri.

wasichofanya wengine sisi tusifanye na wanachofanya wengine tufanye; hazifanani!
 
Kauli yako hiyo tena ni too general na inapingana na maelezo yako mengine. Tulipofika mwaka 1984 Tanzania ilikuwa tayari na viwanda mbalimbali vya bidhaa za ndani. Unaposema kuwa "Tanzania haikuwa mzalishaji wa bidhaa za viwandani" unatutania.

- Tulikuwa na kiwanda cha Chuma Tanga
- Tulikuwa na kiwanda cha ngozi
- Tulikuwa na viwanda vya nguo (Mutex, Mwatex, Sunguratex, Urafiki, n.k)
- Tulikuwa na kiwanda cha Mbolea Tanga
- Tulikuwa na kiwanda cha zana za kilimo (UFI Ubungo) n.k
- Kulikuwa na kiwanda cha Chai Bora
- Kulikuwa na kiwanda cha FOMA
- Tulikuwa na TANBOND
- Tulikuwa na kiwanda cha sabuni cha Mbuni, Malaika, n.k
- Kulikuwa na kiwanda cha kusindika matunda pale Korogwe
- Tulikuwa na kiwanda cha "Viatu Bora"!

Naweza kuendelea kutaja viwanda vilivyokuwa mikoa mingine (Arusha, Morogoro n.k); viwanda hivyo vilikuwa vinadhalisha "bidhaa za viwandani"! Unless una maana nyingine ya "bidhaa za viwandani". Kwa hiyo SIYO KWELI kwamba "Tanzania haikuwa mzalishaji wa bidhaa za viwandani". Suala la kiasi na ubora hilo jingine.

Viwanda vyote ulivyotaja vilizalisha chini ya viwango vyao. Vingine ambavyo vilitaifishwa kutoka kwa watu binafsi kama vile Bora vilikuwa na mitambo ya zamani.

Gridi ya umeme imefika Mwanza na Musoma mwanzoni mwishoni mwa 80 na mwanzoni mwa 90. Viwanda hivi vilikuwepo mwaka 1984 lakini vilikuwa vinakabiliwa na matatizo ya umeme.

Kama kichuguu alikuwa anapeleka ngozi kuuza Kenya, hicho kiwanda cha ngozi kilipata wapi ngozi?

Na hizi suala la kusema kuwa tulikuwa wazalishaji Give me a break. Tanzania ilikuwa haijafikia kiwango cha uzalishaji. Ndio kilimo kilikuwa ni uti wa mgongo.



Hili silo la ajabu duniani, na kuwa taifa la kijamaa haina maana viwanda haviwezi kumilikiwa na serikali. Tunajifunza leo katika uchumi wa dunia jinsi gani serikali mbalimbali duniani zinaanza kurudi katika sekta za uzalishaji na kusimamia uchumi wao.

Ninavyoandika Serikali ya Marekani imetoa mkopo wa karibu bilioni 6 kwa GMAC na sharti mojawapo ni serikali kuwa na hisa/ubia wa aina fulani. Hilo liko hata kwenye bailout ya makampuni ya magari.

So, serikali kujihusisha na uzalishaji inaonekana siyo suala la ujamaa peke yake na kama wao wanafanya 2008 na sisi tulifanya in the 70s it seems we were way ahead of the times! Na ndio maana wengine bado tunaamini kuwa mojawapo ya mambo yaliyochochea ufisadi ndiyo haya ya kuacha watu wajifanyie mambo yao wakitegemea "soko" litasawazisha mambo yote. Wrong we were!

Hapa kuna masuala mengi ambayo umekologa. Hata pa kuanzia sina. Serikali kutoa grant au kukopesa hili kitu fulani kifanyike sio Ujamaa. Watawala wa Roma walitumia pesa za umma kujenga viwanja vya michezo au mifereji ya maji au mabafu kabla Ujamaa haujawa invented.


Hii ni point nzuri lakini flawed. Nia nzuri haina uhusiano wa moja kwa moja na utekelezaji mzuri. Mtu anaweza kuwa na nia nzuri ya kujenga nyumba lakini kama hajui mambo yote ya ujenzi na kinachotakiwa kujenga nyumba hiyo anaweza akajenga kile anachodhania ni "nyumba nzuri" lakini kumbe anajenga kwenye eneo lenye tetemeko la ardhi! Mtu anaweza kutekeleza kwa uzuri kabisa kitu kibaya!

Unazungumza kama mcheza bahati nasibu. Mwenye-Mungu hakucheza kamari alipounda ulimwengu. Mafanikio ya utekelezaji wa vitu vingi unategemea mitigation of risk factors. Hivyo hakuna bahati nasibu kwenye utekelezaji.

Hapa kuna ukweli wa aina fulani. Lakini kwanini havikuweza kushamili tatizo halikuwa katika uchumi tu lakini pia katika utendaji. Leo hii tunavyoshuhudia makampuni mbalimbali yanaendeshwa, nashangaa jinsi gani tuliweza hata kusurvive! Kama hawa leo pamoja na umeme, teknolojia n.k wanaboronga kwenye ATCL na Tanesco hivi miaka ile ya themanini ilikuwaje? Mbona leo tuko kwenye mazingira mazuri zaidi je tumeweza kufanya bora zaidi!?

Hivi leo umeme upo wa kutosha? Sijui kama unajua kuwa wengine wetu hatukumbuki wakati wowote miaka ya themanini (kwenye mikoa iliyokuwa kwenye gridi) kukiwa na mgao wa umeme? Sikumbuki kata kata ya umeme. Wakati ule kama ulikuwa na umeme basi ndio unao kama hauna hauna! Haya ya kusema umeme "ulikuwa na nguvu kidogo" sijui yametoka wapi. Embu tupatie mfano wa kiwanda kilichojengwa mahali ambapo umeme ulikuwa na nguvu kidogo.

Kuhusu mifano ni viwanda vya nguo vya Mwatex na Mutex. Gridi ya taifa imefika mwanzoni mwa 90. Mwanza na Musoma walikuwa wanategemea generators. Kama sikosehi ya Musoma ilikuwa kwenye 3MW.


Kuhusu "pale production ilipokuwa kubwa basi cost za uzalishaji ziliongezeka". Kwa wana uchumi kuna kile wanakiita "law of diminishing returns". Kwanini katika ulimwengu wako kuzalisha vitu vingi kuongeze gharama badala ya kupunguza? Unless unataka kusema vile vilivyozalishwa havikununuliwa (kitu ambacho kitatufanya tujiulize kwanini?)

Hapa unakologa tena. Nilitoa mfano wa viwanda ambavyo vilikuwa katika sehemu ambazo hazina nguvu za umeme wa kutosha. umeme uliozalishwa kwa maji ulikuwa ni cheaper kulinganisha na uliozalisha kwa diesel injini. Hivyo katika sehemu kama vile Mwanza na Musoma viwanda vilikuwa vinatumia gharama kubwa kwa unit hilehile ya umeme.


Hivi leo tunao? Tatizo la wakati ule halikuwa utalaamu hasa miaka ya mwisho wa sabini na themanini. Miaka ya mwanzo ya uhuru tunaweza kutoa kisingizio hicho kwani ni kweli hatukuwa na wataalamu. Lakini inapofika mwisho wa sitini, sabini na themanini karibu watalaamu wengi (wasomi wa vyuo vikuu) walikuwa kwenye nafasi mbalimbali.

Cha kushangaza ni kuwa hata leo tunaletewa kisingizio kile kile "hatuna wataalamu"! Kuna tatizo mahali fulani katika fikra zetu. Ila wakija wazungu wenye taaluma ile ile kama hawa wenzetu, hao tutawakumbatia na kuwaita "Wataalamu!" Tatizo la Tanzania halikuwa watalaamu!

Hapa tena unakologa. Kwenda shule na kupata digrii kuna tofauti na kuwa na expertise. Unachosema wewe ni kuwa tulikuwa wahitimu. Lakini walikuwa hawana track records za kuonyesha ni jinsi gani walitumia elimu zao. Na hayo tunaweza kusema kwa wengi waliopo sasa.


Kuna ukweli wa aina fulani, lakini pia mtu kukimbilia bidhaa moja kwenda nyingine haina maana hiyo anayoikimbilia ina thamani zaidi. Pia kwa vile bidhaa zinatengenezwa kwa malighafi ile ile haina maana zinatengenezwa kwa gharama ile ile! Sitapenda kutoa somo la biashara ambalo sina ujuzi nalo lakini akili yangu inaniambia kuwa kitu chochote kitauzwa kulingana na gharama zilizoingia kukitengeneza kitu hicho. Malighafi ni gharama mojawapo tu! kuna vitendea kazi, nguvu kazi, n.k So, ukikuta kitu cha Tanzania kinauzwa kwa bei rahisi na kitu cha kenya kinauzwa kwa bei ghali mtu atafikiria (kama unavyofanya wewe) kuwa kile cha kenya kina thamani zaidi!

Hapa itabidi ukae kimya tu maana utakologa tena. Nikienda dukani kununua soda, siku zote naagiza Coca hata kama kuna Vimto ya bei ya kutupa hipo pale. Kwa sababu kuna Coca ni bland, napenda packaging yao, napenda staili, naonyesha status. Hivyo kuna mlolongo mzima unao-trigger mimi kununua kitu fulani. Kumbuka kuwa dunia imeshaendelea kutoka katika mwangalio wa bidhaa kutokana na basic functionalities na bidhaa hizo.
 
Viwanda vyote ulivyotaja vilizalisha chini ya viwango vyao. Vingine ambavyo vilitaifishwa kutoka kwa watu binafsi kama vile Bora vilikuwa na mitambo ya zamani.

Hii kauli bado iko hewani! Nilinganishie kuwa "kilichozalishwa Tanzania mwaka 1984 hakikulingana na kilichozaliwa nchi x,y kwa kuangalia vipimo hivi, na hivi na vile". Unataka nikubali maneno yako kuwa "vilizalisha chini ya kiwango chako" kwa ujumla wake wote? Kwamba viwanda vya Bora vilikuwa na mitambo ya zamani? Zamani kulinganisha na nini? Kwamba vilikuwa vimedepreciate kupita ilivyotarajiwa? Kwamba mitambo ilikuwa ni ya kufanya kazi kwa muda gani na miaka ya themanini ilikuwa imepita muda gani?

Gridi ya umeme imefika Mwanza na Musoma mwanzoni mwishoni mwa 80 na mwanzoni mwa 90. Viwanda hivi vilikuwepo mwaka 1984 lakini vilikuwa vinakabiliwa na matatizo ya umeme.

Kama kichuguu alikuwa anapeleka ngozi kuuza Kenya, hicho kiwanda cha ngozi kilipata wapi ngozi?

Hapa ni wewe unachanganya; gridi ya taifa au kutokuwa na gridi ya Taifa haina maana hakuna umeme! Lakini pia kutumia majenereta haina maana kuwa umeme ni dhaifu!

Na hizi suala la kusema kuwa tulikuwa wazalishaji Give me a break. Tanzania ilikuwa haijafikia kiwango cha uzalishaji. Ndio kilimo kilikuwa ni uti wa mgongo.

sasa unataka watu waamini kuwa Tanzania ilikuwa haidhalishi bidhaa yoyote?



Hapa kuna masuala mengi ambayo umekologa. Hata pa kuanzia sina. Serikali kutoa grant au kukopesa hili kitu fulani kifanyike sio Ujamaa. Watawala wa Roma walitumia pesa za umma kujenga viwanja vya michezo au mifereji ya maji au mabafu kabla Ujamaa haujawa invented.

Angalia kinachofanywa basi ili angalau uwe na msingi wa kusimamia! Kinachotolewa na serikali kwenye hizi siyo tu grants au loans, nyingine zina masharti ya umiliki au hisa. Serikali inapoingia na kuwa hisa kwenye kampuni binafsi ili kuisimamia kampuni hiyo inafanya kile kinachofanywa katika ujamaa! Ni mfumo wa ujamaa unaoruhusu serikali kuingilia kwenye productions au kusimamia means of production! Ubepari production inafanywa (at least theoretically) kwenye sekta binafsi na serikali inakaa pembeni kama mratibu, msimamizi na mwamuzi siyo mmiliki! Sasa kama hii tofauti kubwa kati ya Ujamaa na Ubepari huijui au hutaki kuikubali itakuwa kazi kidogo.




Unazungumza kama mcheza bahati nasibu. Mwenye-Mungu hakucheza kamari alipounda ulimwengu. Mafanikio ya utekelezaji wa vitu vingi unategemea mitigation of risk factors. Hivyo hakuna bahati nasibu kwenye utekelezaji.

Bahati mbaya sana kuna watu wanaamini kuwa Mungu alicheza Kamari! Katika biashara na katika utekelezaji wa vitu vingi watu wanachukua risk na risk wakati mwingine ni bahati nasibu. Hakuna mwanasiasa au mwanasheria ambaye anaweza kuguarantee end results ya mpango wowote ule uwe wa kiuchumi au kisiasa. they always gamble that it'll turn out in their favor!

Ingekuwa kila kitu kikipangwa hakuna hiyo element ya bahati nasibu, basi mambo yote yangekuwa yanafanyika yalivyotakiwa. Nipe mfano wowote duniani wa mpango ambao ulichukuliwa ikijuliikana kuwa matokeo yake yatakuwa yale tu yaliyotarajiwa!

Kuhusu mifano ni viwanda vya nguo vya Mwatex na Mutex. Gridi ya taifa imefika mwanzoni mwa 90. Mwanza na Musoma walikuwa wanategemea generators. Kama sikosehi ya Musoma ilikuwa kwenye 3MW.

Mahitaji ya viwanda hivyo yalikuwa kiasi gani, na majenereta yalikuwa yana uwezo wa kiasi gani. KUtumia majenereta haina maana umeme ni dhaifu kama unavyotaka watu waamini. 3MW inayozalishwa na umeme wa maji, 3MW inayozalishwa na umeme wa mafuta zina tofauti gani katika potency yake?



Hapa unakologa tena. Nilitoa mfano wa viwanda ambavyo vilikuwa katika sehemu ambazo hazina nguvu za umeme wa kutosha. umeme uliozalishwa kwa maji ulikuwa ni cheaper kulinganisha na uliozalisha kwa diesel injini. Hivyo katika sehemu kama vile Mwanza na Musoma viwanda vilikuwa vinatumia gharama kubwa kwa unit hilehile ya umeme.

Unazungumzia nguvu au gharama? Ukisema kuwa gharama ya umeme wa mafuta ilikuwa ni kubwa zaidi kuliko ile ya umeme wa maji na hivyo viwanda vilivyotumia umeme wa mafuta vilikuwa na gharama kubwa ya uendeshaji hapo utakuwa umetoa sababu! Lakini ukisema kwa vile umeme wa mafuta ni ghali basi ni dhaifu hapa unatoa kisingizio!



Hapa tena unakologa. Kwenda shule na kupata digrii kuna tofauti na kuwa na expertise. Unachosema wewe ni kuwa tulikuwa wahitimu. Lakini walikuwa hawana track records za kuonyesha ni jinsi gani walitumia elimu zao. Na hayo tunaweza kusema kwa wengi waliopo sasa.

Hapa unaleta semantics tu! HIvi wote waliohitimu hawawezi kufanya kitu kifanyika vizuri kutokana mafunzo wanayoyapata wakati wa masomo? MBona leo tuna watu waliohitimu miaaka ya sabini wengine sitini tena kwenye mavyuo makubwa tu wanashindwa kusimamia ATCL? Kusema kuwa tatizo ni watalaamu si kweli; Kuna fani chache sana ambazo Tanzania haina watalamu wake, lakini nyingi tayari tuna wataalamu kibao tu!

Ukisema uzoefu, uzoefu utapatikana vipi bila watu kuanza kufanya wanachotakiwa kufanya au uzoefu ni hadi ufanye kwenye kampuni ya kizungu au majuu ndio uzoefu wako unacount?



Hapa itabidi ukae kimya tu maana utakologa tena. Nikienda dukani kununua soda, siku zote naagiza Coca hata kama kuna Vimto ya bei ya kutupa hipo pale. Kwa sababu kuna Coca ni bland, napenda packaging yao, napenda staili, naonyesha status. Hivyo kuna mlolongo mzima unao-trigger mimi kununua kitu fulani. Kumbuka kuwa dunia imeshaendelea kutoka katika mwangalio wa bidhaa kutokana na basic functionalities na bidhaa hizo.

Sasa unaposema kuwa Watanzania kununua bidhaa za Kenya ni sababu ya valued added mimi nakuuliza ya Tanzania unajuaje kuwa haikuwa na value added? Na umesema kitu kingine kizuri, kuna watu wananunua vitu kutokana na rangi, uzuri wake, na hata jina lake! Sasa hayo ni mambo ya masoko! Kama kitu cha Tanzania ni bora na imara lakini kikauzwa vibaya huwezi kulaumu uzalishaji wake au kukiona duni ati kwa vile hakikuwekwa kwenye chupa nzuri au jina lake siyo la kuvutia! Mambo ya masoko ni hoja nzuri zaidi kuliko ya uzalishaji.

Mapungufu makubwa ya biashara yetu ya zamani miaka ile ilikuwa ni mbinu duni za masoko (marketing strategies). Hatukujua mambo ya branding, market analysis n.k Pole pole watu wanaanza kujifunza hasa kutokana na makampuni kama ya simu n.k ambayo yanaonesha kwa kiasi kikubwa masoko yanavyofanywa!

Ninakuambia ukinipa TANBOND leo hii naweza kuiuza kwa Mtanzania vizuri zaidi kuliko Kimbo au wenzake!

Sasa kutokuwa na ufundi au mikakati bora ya masoko haina kilichozalishwa ni duni!

Unataka watu waamini kuwa bidhaa za Kenya zilikuwa bora zaidi kuliko za Tanzania kisa "zilikuwa na brand nzuri, rangi nzuri, n.k" hicho ni kisingizio!
 
Mapungufu makubwa ya biashara yetu ya zamani miaka ile ilikuwa ni mbinu duni za masoko (marketing strategies). Hatukujua mambo ya branding, market analysis n.k Pole pole watu wanaanza kujifunza hasa kutokana na makampuni kama ya simu n.k ambayo yanaonesha kwa kiasi kikubwa masoko yanavyofanywa!

Ninakuambia ukinipa TANBOND leo hii naweza kuiuza kwa Mtanzania vizuri zaidi kuliko Kimbo au wenzake!

Sasa kutokuwa na ufundi au mikakati bora ya masoko haina kilichozalishwa ni duni!

Mwanakijiji:

I am impressed kama TANBOND leo hii unaweza kuiuza kwa Mtanzania vizuri zaidi kuliko Kimbo au wenzake!.

Hata mimi leo ukinipa ATCL, nitalifanya liwe kampuni moja ambalo wazawa watajivunia kuwa ni la kwao.
icon10.gif


Kulikuwa na mapungufu makubwa ya biashara na mambo mengi. Lakini je tunayafanya mapungufu hayo kuwa shule ?

Kama Ben Bernanke, Chairman of the Federal Reserve, ni mwanachuoni aliyebobea mambo ya Great depression. Kwanini tusitumie mapungufu yetu ya uhaba wa bidhaa kama shule?

Hivyo usiwe na kinyongo na mimi nachukua kushindwa kwetu kama mambo ya kidarasa tu.

Bonane
 
Huu mjadala ni wa kina sana. Unagusa masuala mazito ya kitaifa. Naomba muuweke kwenye kijarida maalumu ili Watanzania tuujue ukweli kuhusu uhujumu uchumi. Mtakuwa mnatutendea sisi wananchi dhambi isiyosameheka kama hamtasambaza nchi nzima haya mnayoyajadili hapa ili mtufumbue macho. Mustakabali wa taifa uko mikononi mwenu.

Tafakari. Chukua Hatua.
 
Mwanakijiji:

I am impressed kama TANBOND leo hii unaweza kuiuza kwa Mtanzania vizuri zaidi kuliko Kimbo au wenzake!.

hahahaha.. unajua salesman mzuri ni yule anayeweza kukuuzia kitu ambacho hukihitaji! Nimewashi kushuhudia jamaa alienda kuuliza kwenye dealer fulani maelekezo ya jinsi kufanyia matengenezo gari lake; alirudi akiwa na gari jipya!

Hata mimi leo ukinipa ATCL, nitalifanya liwe kampuni moja ambalo wazawa watajivunia kuwa ni la kwao.
icon10.gif

exactly!! nina uhakika utafanya hivyo kwa sababu unaamini ndani yako una uwezo wa kufikiri na kukabiliana na matatizo. Unaamini ya kwamba ATCL haijatushinda Watanzania. Mwamko huo wa fikra ndicho ninachopigania mimi; kwamba tuna uwezo wa kufanya 99.99 ya vitu vinavyofanywa vizuri sehemu nyingine duniani! Hatuhitaji Wachina wala WaSouth Africa kutufanyia kilichomo ndani ya uwezo wetu!

Kulikuwa na mapungufu makubwa ya biashara na mambo mengi. Lakini je tunayafanya mapungufu hayo kuwa shule ?

Hilo ndilo swali la Shilingi milioni moja!

Kama Ben Bernanke, Chairman of the Federal Reserve, ni mwanachuoni aliyebobea mambo ya Great depression. Kwanini tusitumie mapungufu yetu ya uhaba wa bidhaa kama shule?

make that a billion Tshs question!

Hivyo usiwe na kinyongo na mimi nachukua kushindwa kwetu kama mambo ya kidarasa tu.

Bonane

usiwe na shaka sijadiliani na mtu yeyote kwa kinyongo; never. NI katika kubadilishana mawazo tu na wakati mwingine kunoana kifikra kwani tunapofanya hivyo tunaibua hoja nzuri, bora, na zile dhaifu tunaziona kwa mwanga mkubwa zaidi.

Na hapa tuko pamoja, swali ni kuwa kwanini Watanzania hatujifunzi? tumeboronga kwenye mkataba wa IPTL, tukaendelea na Richmond, Dowans, Buzwagi, ATCL, n.k why?


Tukaboronga kwenye ubinafsishaji na ubia wa uendeshaji kwenye TANESCO, hatukutosheka tukaenda na kwingine?

Mtu atusaidie kupata jibu la kwanini tuna facts zote na darasa liko wazi mbele zetu kwanini hatujifunzi?

Leo Rais anauliza kwanini matokeo ya darasa la saba ni mabaya sana!! siku hiyo hiyo bodi ya NBAA inasema kati ya wanafunzi 3125 waliofanya mtihani wa bodi ni 513 (sawa na asilimia 16.7) ndiyo waliofaulu! any correlation? Kwani hii ni mara ya kwanza?

Labda kutojifunza kunataka ujasiri zaidi kuliko kujifunza!
 
hahahaha.. unajua salesman mzuri ni yule anayeweza kukuuzia kitu ambacho hukihitaji! Nimewashi kushuhudia jamaa alienda kuuliza kwenye dealer fulani maelekezo ya jinsi kufanyia matengenezo gari lake; alirudi akiwa na gari jipya!

exactly!! nina uhakika utafanya hivyo kwa sababu unaamini ndani yako una uwezo wa kufikiri na kukabiliana na matatizo. Unaamini ya kwamba ATCL haijatushinda Watanzania. Mwamko huo wa fikra ndicho ninachopigania mimi; kwamba tuna uwezo wa kufanya 99.99 ya vitu vinavyofanywa vizuri sehemu nyingine duniani! Hatuhitaji Wachina wala WaSouth Africa kutufanyia kilichomo ndani ya uwezo wetu!

Hilo ndilo swali la Shilingi milioni moja!

make that a billion Tshs question!

usiwe na shaka sijadiliani na mtu yeyote kwa kinyongo; never. NI katika kubadilishana mawazo tu na wakati mwingine kunoana kifikra kwani tunapofanya hivyo tunaibua hoja nzuri, bora, na zile dhaifu tunaziona kwa mwanga mkubwa zaidi.

Na hapa tuko pamoja, swali ni kuwa kwanini Watanzania hatujifunzi? tumeboronga kwenye mkataba wa IPTL, tukaendelea na Richmond, Dowans, Buzwagi, ATCL, n.k why?

Tukaboronga kwenye ubinafsishaji na ubia wa uendeshaji kwenye TANESCO, hatukutosheka tukaenda na kwingine?
Mtu atusaidie kupata jibu la kwanini tuna facts zote na darasa liko wazi mbele zetu kwanini hatujifunzi?

Leo Rais anauliza kwanini matokeo ya darasa la saba ni mabaya sana!! siku hiyo hiyo bodi ya NBAA inasema kati ya wanafunzi 3125 waliofanya mtihani wa bodi ni 513 (sawa na asilimia 16.7) ndiyo waliofaulu! any correlation? Kwani hii ni mara ya kwanza?

Labda kutojifunza kunataka ujasiri zaidi kuliko kujifunza!


Mwanakijiji:

Wewe, Mkandara, Companero na wengine washabiki wa Nyerere nimeshapigana nanyi battle mara nyingi toka tukiwa darhotwire. Kuna kipindi nilikuwa far right lakini baada ya kupitia vitabu vya watu mbalimbali ninaanza kurudi kati.

Kwa maoni yangu ya sasa. Maendeleo ya sasa ya Tanzania ni lazima yawe guided. Serikali ni lazima i-guide maendeleo ya nchi.

Hata katika sekta binafsi. Lazima serikali itoe-guidance. Nina mifano ya kutosha iliyonifanya nibadili mawazo.

Kwanza: Intel ndio inayoongoza kwa kuuza chips za computers duniani. Lakini katika miaka ya 80, serikali ya Japan waliongoza viwanda vyao na kuweza kuzidi Intel. Lakini Marekani ilibidi wa-force wajapan kubadili na kuingia mikataba ambayo iliwapa advantage Intel.

Pili: Actual cost ya uzalishaji wa mazao ya shamba katika nchi zilizoendelea ni kubwa sana kiasi cha kwamba hakuna mkulima katika nchi zilizoendelea anayeweza kupata faida kwa kutegemea kilimo. Kwa mfano ya mkulima wa pamba wa Ugiriki au Spain hili aweze kupata faida ni lazima apewe ruzuku ambazo zitamfanya amshinde mkulima wa pamba wa Mwanza. Hivyo mkulima wa Mwanza hataweza kuuza pamba yake na kupata mtaji wa kutosha kuendelea.

Na hile Jiografia ya wanafunzi wa darasa la sita ya wakulima Marekani haina mpango tena. Mkulima wa Marekani bila guidance na ruzuku za serikali hana chake. Hivyo hakuna sababu ya kufungua vyuo vya kilimo na kuwafundisha watu ukulima wa kisasa hili washindane na wakulima wa Marekani. Cha muhimu ni ku-guide watu wa productive. Kilimo hakiwaongezii wanafunzi wa Tanzania their intellectual curiosity, hivyo cha muhimu ni kuongeza productivity. Na mambo ya intellectual curiosity tuwaachie wale wachache watakaofanya R&D za kilimo na ufugaji.

Tatu: Niliangalia mashirika ya ndege ya Ethiopia na nchi za Kiarabu. Mashirika haya hayakuangalia sana technologia ya ndege. Lakini wamejaribu kuweka models ya operation ambazo zinawapa wao faida. Hivyo unaweza kuwa na watu wasiojua masuala ya kiufundi lakini ukawa na watu wanaojua kuweka business models ambazo zinatoa faida.

Kama mitambo ya kiwando cha nguo inaweza kufanya kazi no-stop kwa miaka mitano bila kufanyiwa matengenezo makubwa kwanini kiwanda kama Urafiki kishindwe kuendelea kwa faida. Ni model za operation tu zinakwamisha lakini sio mitambo au wateja.

Nne: Nimesoma kidogo kuhusu great depression. Na hata hapa watu wanamjadili Roosevelt kama alifanya kazi kubwa kuondoa depression. Lakini kuna siri moja watu hawataki kuiona. Vita vya pili vya dunia vilichangia kuondoa depression. Katika kipindi hiki shughuli nyingi za armament zilifanyika. Shughuli hizi ziliwapa watu kazi. Na kazi ziliwapa watu neema.

Tano: Baada ya vita vya kwanza vya dunia. Ujerumani nayo iliweza kuondokana na matatizo yake ya kiuchumi baada ya Hitler kuingia madarakani na kuanza shughuli za armament na ujenzi wa miundo mbinu.

Kwa point ya nne na ya tano. Kulikuwa na viwanda hapa Marekani vinakufa, Lakini Bush alipoingia madarakani alianza na sera za military modernization. Hii imefanya serikali kutumia na ku-create kazi.

Na kwa point hizo hizo Obama naye atakuja na kuanza kujenga mabarabara na miundombinu.

Sehemu kubwa ya vita vya 1978-1979 ilipiganwa Uganda. Na haikuathiri miundo mbinu ya Tanzania. Hivyo basi zile dollar 500 Million zilizotumika katika vita, zingetumika kununua silaha zinazotengenezwa Tanzania, tungekuwa well off. Matatizo yanayokuja pesa hizo zilikwenda Urusi, China na Bulgaria.

Na vilevile pesa zinazotumiwa kujenga mabarabara zingekuwa zinatumia makandarasi wa ndani, ukweli tungekuwa na faida kubwa kuliko kuwa na makandarasi kutoka nje.

Hivyo ni lazima turudi kwenye drawing board. Serikali ni lazima i-guide sekta binafsi.
 
Mwanakijiji:Wewe, Mkandara, Companero na wengine washabiki wa Nyerere nimeshapigana nanyi battle mara nyingi toka tukiwa darhotwire. Kuna kipindi nilikuwa far right lakini baada ya kupitia vitabu vya watu mbalimbali ninaanza kurudi kati.Kwa maoni yangu ya sasa. Maendeleo ya sasa ya Tanzania ni lazima yawe guided. Serikali ni lazima i-guide maendeleo ya nchi.Hata katika sekta binafsi. Lazima serikali itoe-guidance. Nina mifano ya kutosha iliyonifanya nibadili mawazo.

Karibu kundini ewe kondoo uliyekuwa umepotea. Hakika Tanzania inahitaji 'Njia ya Tatu'. Hapo katikati ndio panafaa. Uchumi mchanganyiko ndio utatusaidia. Serikali itoe mwongozo. Iingilie kati ikibidi. Ila isiingilie kati sana na kutusonga.

Kuwe na udhibiti wa hali ya juu wa uhujumu/ufisadi. Mkaguzi Mkuu wa Serikali apewe meno ya kushikisha adabu taasisi na watu wote wanaokiuka sheria na taratibu za kifedha kila mwaka - ripoti yake iwe inatoka haraka mara tu baada ya mwaka wa fedha kuisha. Kuwe na mwendesha mashtaka huru anayeweza hata kumshitaki waziri aliyepo kwenye baraza la mawaziri lililopo madarakani.

Kamwe tusiruhusu siasa ichanganywe na biashara. Kila mtumishi wa umma akaguliwe mali zake na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kila mwisho wa mwaka wa fedha. Na atoe maelezo ameipataje mali hiyo.Benki nazo zikaguliwa ili zisitunze fedha chafu. Na Mkaguzi naye akaguliwe pia. Jino kwa jino. Jicho kwa jicho.
 
Zakumi na Mwanakijiji,

Naomba niendelee kutoa heko kwa kuleta uchangamfu katika thread hii. Kama nilivyosema hapo awali, thread hii yawezekana ikawa ndiyo thread yenye uchambuzi wa kina kuhusiana na uchumi wetu na miundo yake tukiwa tunajaribu kuchangua chimbuko la vita vya uhujumu.

Nitakaa kitako wikiendi hii niendeleze hoja.
 
Wanabodi,
Inabidi niendeleze mjadala huu kwa sababu kutokana na mawazo ya Zakumi nashindwa kabisa kuelewa kwa nini viongozi na wasomi wetu wanashindwa kuelewa hali halisi ya nchi yetu..anajaribu sana kupandikiza mbegu za kulaumu watu na uwezo wa nchi badala ya mfumo..
Nimemsoma sana Zakumi lakini kila mara naona kwamba anatumia sana kitabu badala ya kuangalia watu na mazingira ktk hali halisi kufuatia miaka hiyo..
Imefikia hata kusema kulikuwepo na Tatizo la Umeme mikoa ya Mwanza miaka hiyo jambo ambalo nashindwa hata kumwelewa..Mwanza wala Musoma haikuwa na matatizo ya Umeme wakati wa Nyerere, kwa sababu tulikuwa tukizalisha umeme zaidi ya matumizi yetu na ndio umeme huo huo umetumika hadi miaka ya hivi karibuni pamoja na kupanda kwa population, uwejekeshaji na kadhalika X2..

Amekazania sana kusema vitu vilivyokuwa vikisafirishwa nje vilikuwa havitoshi hata kama vingebakia nchini akiwa hana takwimu za kuonyesha hivyo isipokuwa kutumia nadharia inayoonyesha demand na supply inavyocheza..
Leo hii watu wanaingiza magari toka nchi za nje haina maana huko nje kuna Upungufu wa magari kwa sababu tu kuna Operation ya kukamata watu wanaosfirisha magari nje hasa nchi za kiafrika..Anashindwa kufikiria kiini au sababu hasa ya vita kama hii kuwa inatokana na mfumko wa wizi wa magari haya kuyapeleka nchi za Afrika na haihusiani kabisa na hali ya uzalishaji wa magari nchi hizo.
.
Pia nitarudia kwamba fikra za criminal hata siku moja haziwezi kupimwa na Uchumi kwa sababu huwa wako one step ahead ya somo la kiuchumi..nayo ni kuwepo ktk hali halisi ya watu na mazingira yanayoohusika na uchumi tunaounzungumzia.
Kwa mfano, kabla na wakati wa Uhujumu Uchumi tulikuwa tukichukua Prawns toka Chakula barafu kwa Tsh 600/Ib wakati thamani ya shilingi ilikuwa Tsh.21 kwa Us dola. Sasa Ukitumia hesabu za Kisomi utakuta bei hiyo ilikuwa kubwa ajabu (almost Usd 30/Ib) na unaweza bisha hadi kesho ukaanza kutumia mfumko wa bei kutokana na demand... lakini hata hivyo huko nje prawns hao hao waliuzwa dollar 10 kwa Pound! sasa hawa watu wanauza vipi...mahesabu hayapandi kabisa.
Lakini kwa wabaingazaji walijua bei ya dola Mtaani ni Tsh 175 hivyo inaponunua Apound of Prawns kwa 600 ni sawa na Usd 4 tu.. Soko Harare lilikuwa Zd 10 na chenji ilikuwa 1Zd =1Usd..
Hapa nyumbani bei ya prawns under price control chini ya Tsh. 50/Ib hivyo, mfanya magendo akiingia Chakula barafu tu wajomba wanashangilia wanajua wataingia 600/ib wakati zinazokwenda mfuko wa Chakula barafu ni Tsh 50 /ib..pato la ziada Tsh.550/Ib wanagawana wahusika ndani ya ofisi ya Chakula barafu..Kama kutakuwepo na Upungufu wa prawns mahoteli yetu ya Kitalii, mfanya magendo na Mpokea rushwa hawatazai hilo isipokuwa kiwango cha fedha anazoweza yeye kutengeneza kutokana na sheria ambazo hazikuzingatia hali halisi.

Magendo hayatazami uzalishaji na ugawaji wa prawns Tanzania isipokuwa soko lake nje lipo vipi, Na hatukupeleka Kenya kwa sababu ilikuwa hailipi kama Zimbabwe na South Africa..Hatukutazama kama sisi tunazalisha in excess au less ya demand ya ndani ila tulichofahamu ni biashara haramu..Uharamu wake unakuja kwamba hairuhusiwi kusafirisha prawns nje bila kuwa na kibali pamoja na mlolongo wa regulations kupitia benki kuu..Hivyo hivyo kila siku walanguzi walikuwa wakitafuta masoko nje kutokana na ukweli kwamba mali hizo zilizalishwa nchini..

Chimbuko la Magendo nchini lilitokana na siasa ya Ujamaa ktk Biashara..Vitu kama price control, Export regulations na kadhalika ndivyo vilichangia sana watu kuanza kupitia mlango wa nyuma kinyume cha sheria kwa sababu soko lilikuwepo nje lakini sheria hazikuruhusu watu kufanya biashara hizo free kwani viwanda vilivyokuwa mali ya serikali na mali iliyozalishwa ilikuwa kwa malengo ya huduma za ndani nchini na kama Export basi serikali ndiyo ilihusika pia kwa sababu nyinge ya kisiasa kuwa unafanya biashara na nchi yenye kukubaliana na mrengo ama utawala uliopo. Politics ndizo zilikuwa zikiendesha Uchumi wa nchi badala ya Uchumi kuendesha Politics..

Haya mambo menngine mtasema weeee... lakini ukweli upo on the ground..
1 Magendo - ni ku supply vitu kinyume cha sheria.
2. Rushwa - ni kutoa/kupokea malipo ya ziada ktk huduma..
3. Uhujumu Uchumi - ni pamoja na crimes zote zinazohusiana na Uchumi wa nchi iwe moja kwa moja au kwa kupitia (indirectly)..
 
Mkandara,

..sasa kama uzalishaji haukuwa na kasoro zozote zile , ilikuwaje uchumi wetu ukatitia kiasi kwamba wakati Mwalimu anaondoka madarakani hazina ilikuwa imekauka, na tulishindwa hata kugomboa meli moja ya mafuta pale bandarini?

..kwasababu kwa theories zako, viwanda vilikuwa vinazalisha kiwango cha kutosha ila tatizo bidhaa zote zilikuwa zinakwapuliwa na walanguzi kabla hazijamfikia mlaji.

..kama hilo hapo juu lingekuwa kweli basi tungeweza kuona expansion ya namna fulani ya viwanda na makampuni ya umma. badala yake viwanda hivyo ndiyo kwanza vilikufa.

NB:
..swali lingine kwa wachangiaji: kwanini viwanda vyetu vilikufa wakati vilikuwa na soko la uhakika kutokana na monopoly? fikiria kiwanda kama UFI ambacho kilipewa jukumu la kuzalisha majembe nchini.
 
Back
Top Bottom