Nini chanzo cha vita ya kagera?

Sakata zima lilianza tu baada ya IDD AMIN kumpindua kijeshi Rais MILTON OBOTE january 1971,IDD AMIN ambaye alipata mafunzo huko Israel kama askari wa miavuli(paratrooper)alikuwa karibu sana na Wa-ISRAEL na ndio waliomsaidia sana kuingia Madarakani wakisaidiwa na Mashirika ya Kijasusi ya UINGEREZA na ISRAEL.
Wakati huo ARAB WORLD ilikuwa inauguza vidonga vya kushindwa na ISRAEL katika vita vya siku 6 ambavyo ISRAEL ilionyesha UBABE wake katika MEDANI ya vita vya ardhini,angani na Majini.Gaddafi na Maofisa wengine vijana walikuwa madarakani wakati huo waliweza kwa kiasi fulani kuondoa unyonge huo katika nchi za Kiarabu.
Mwaka 1972 March Gaddafi alianza kufanya Mazungumzo ya siri na IDD AMIN na alimwomba avunje Mahusiano ya Kibalozi na ISRAEL na yeye GADDAFI angeweza kumpa misaada yoyote ya kijeshi na misaada mingine ya ki-uchumi na IDD AMIN alikubaliana naye na hapo hapo Balozi wa ISRAEL nchini Uganda alifukuzwa na kurudi kwao yeye pamoja na washauri wa mambo ya kijeshi wote hapo hapo GADDAFI alitoa 5,000,000USD.Hapo GADDAFI alipata sifa sana katika nchi za Kiarabu maana aliweza kukatilia Mbali Uhusiano wa Uganda na Israel na hapo hapo Libya ilianza kuweka Vitega uchumi vyake nchini Uganda.
IDD AMIN alilengwa sana na GADDAFI sababu yeye alikuwa Mwislamu na istoshe yeye alikuwa kama mtu mbabe sana na aliyefundishwa vizuri na ISRAEL hivyo ingekuwa tishio sana kwa nchi za Kiarabu ndiyo maana Gaddafi alimushawishi AMIN aunge mkono harakati za nchi za Kiarabu hasa kuhusu PALESTINA na alipokubali alizawadiwa zawadi nzuri pamoja na pesa ili kuinua uchumi wa UGANDA. Misaada hiyo aliahidiwa haiwezi kukoma mpaka mwisho wa utawala wake ndiyo maana hata Utawala wake ulipowekewa vikwazo na OAU wakati ule 1975 pamoja na nchi za magharibi kumwekea vikwazo lakini LIBYA na SAUD ARABIA waliendelea kumwaga misaada UGANDA na walilipa michango yote ya UGANDA huko OAU mwaka 1975.
Uhusiano kati ya Tanzania na Uganda uliendelea kuzorota baada tu ya IDD AMIN kumpindua MILTON OBOTE Mwaka 1971,Baada ya Mapinduzi hayo Rais Nyerere alimpa hifadhi ya kisiasa MILTON OBOTE pamoja na wakimbizi wengine 20,000 waliokimbia Utawala wa mabavu wa IDD AMIN,Baadaye mwaka 1972 wakimbizi wa Uganda walifanya jaribio lililoshindwa la kutaka kumpindua AMIN tokea Tanzania,Kitendo hicho kilimfanya AMIN alimshutumu sana Nyerere kuwa nyuma ya tukio hilo la kuwapatia silaha wafuasi wa MILTON OBOTE tokea hapo uhusiano wa Tanzania na Uganda ulizidi kuwa tete sana
Hatimaye Mwaka 1978 wapinzani wa IDD AMIN walivamia Ikulu ya Kampala lakini IDD AMIN aliweza kutoroka na Helicopter hii ilikuwa kipindi kigumu sana kwa IDD AMIN hasa alikosa maelewano na Makamu wake wa Rais wakati ule aliyekuwa anaitwa General MUSTAFA ADRISA aliyepata ajali kwa ajali ambayo ilihisiwa kuwa ilikuwa ya kupangwa na wale askari waliokuwa wanamuunga mkono walimuasi AMIN hivyo kupelekea askari hao kuvamia Ikulu ya Kampala,Kitendo hicho kilimfanya AMIN Kutuma askari wake watiifu kwenye kambi iliyokuwa inajulikana kama SIMBA BATTALION na kusababisha waasi kukimbilia Tanzania ambako kulikuwa na askari wenzao kutoka Uganda waliokuwa wakimpinga AMIN Kitendo ambacho AMIN kilimfanya awafuatilie huko waliko kwa matamushi yake mwenyewe alitumia dakika 25 tu kuteka eneo lote la kagera na kulitangaza eneo hilo kuwa sehemu ya UGANDA.
Katika uvamizi huo ambao ulihusisha zaidi ya askari 3,000 wenye silaha za kisasa wakti huo,Majeshi ya Uganda yaliyokuwa hayana Nidhamu walianza kwa Kuwabaka wanawake na walipora vitu mbali mbali vijiji viliteketezwa Makanisa yaliharibiwa vilevile waliweza kupora mashine nzito,Mabati,Magari,Mabomba pia yaliharibiwa shule pamoja na Hospitali hazikuweza kubaki salama mbele ya askari wa Amin,Miji jirani na Bukoba ilifulika wakimbizi waliokuwa wakikimbia toka uwanja wa mapambano ambao AMIN alisema aliweza kukalia eneo hilo kwa mwendo wa SUPERSONIC yaani dakika 25 tu na kilifanya eneo la UGANDA. ndipo Majeshi ya Tanzania yalipoingia vitani na ukawa ndio mwanzo wa VITA VYA KAGERA.
A good analysis! Congratulation for knowing the history!
 
"Nakuomba sana usiingize DINI harakaharaka angalia pande zote vaa na wewe uhusika uone kama wewe ndo ungekuwa Nyerere ungemtendeaje Rafiki yako Dhidi ya ADUI yake????."

Jamana watu mmeomba historia, mtu anaelezea jinsi anavyoelewa anakosolewa, ungeleelezea wewe basi kama vip.
 
Tukiacha ushabiki Ukweli nyerere alikosea sana na ndie alieanza uchokozi.
 
Hakuna uchokozi wowote uliofanyika hapo
katika sheria za kimataifa zinaruhusu utumiaji wa nguvu pindi ukivamiwa. Kwa kuwa idd amin alikuwa amevuka mpaka na kukalia eneo la tanzania tanzania ilikuwa na uhalali wa kuzuia hali hiyo kutumia nguvu kumwondosha adui huyo
Kosa pekee tanzania ililolifanya ni kutoomba kibali umoja wa mataifa kabla ya kutumia nguvu kwa kuwa sheria za kimataifa zinahitaji nchi inayotaka kutekeleza haki ya self defence kupata baraka za UN
 
Hii sheria imekaa kimangungo kabisa. Yaani nivamiwe na jambazi kwangu halafu nikimbie kwa balozi kuomba idhini ya kupambana naye! Si narudi nakuta jambazi kabeba si mali zangu tu bali hata mke na watoto! Imekaa kushoto aisee.
 
lengo la sheria hii ni kuzuia nchi zenye nguvu kuvamia kiuchokozi nchi dhaifu kwa kosa dogo ambalo linaweza kutatuliwa mezani ambalo madhara yake ni madogo kiasi cha kuanzisha vita au kitendo kilichotokea mara moja ambacho hakina mpango kuendelea.

Hii sheria imekaa kimangungo kabisa. Yaani nivamiwe na jambazi kwangu halafu nikimbie kwa balozi kuomba idhini ya kupambana naye! Si narudi nakuta jambazi kabeba si mali zangu tu bali hata mke na watoto! Imekaa kushoto aisee.
 
Hakuna uchokozi wowote uliofanyika hapo
katika sheria za kimataifa zinaruhusu utumiaji wa nguvu pindi ukivamiwa. Kwa kuwa idd amin alikuwa amevuka mpaka na kukalia eneo la tanzania tanzania ilikuwa na uhalali wa kuzuia hali hiyo kutumia nguvu kumwondosha adui huyo
Kosa pekee tanzania ililolifanya ni kutoomba kibali umoja wa mataifa kabla ya kutumia nguvu kwa kuwa sheria za kimataifa zinahitaji nchi inayotaka kutekeleza haki ya self defence kupata baraka za UN
Kumbuka baada ya kuyaondoa majeshi ya Amin nchimi Tanzania waasi waliokuwa wanampinga Amin na walikuwa tayari wanataka kumtoa Amin madarakani JWTZ ilifanya tu kuwasaidia kumtoa Amin hivyo Tanzania hatukuwa na haja ya kuomba kibali UN.
 
Sasa mbona kuna upinzan zidi ya historia!!yaan nataka kujua Nyerere alianzisha uchokoz kivipi??

Mtake msitake Late Nyerere ndie mchokozi. Huwezi kufuga wapinzani kwako wakapindue nchi ingine. Halafu late IdiAmini atulie tu.
Baada ya Rais Obote na ndg yake yule General wa jeshi kukimbizwa Uganda walikuja ishi TZ na mwalimu alihakikisha wanapata kila kitu kijeshi ili wakamtoe Amin.
Haikuwa Kazi rahisi kwani Amin alikuwa na uwezo mkubwa kijeshi.
Urafiki wa Nyerere na Obote ndo umetuponza economically hadi leo, kwa kuingiza nchi vitani bila tija yoyote. Angalia Mwalimu alivyoitengeneza hii vita.
Mwaka 1977, kulifanyika mazoezi ya Brigade zote kitu ambacho hakikuwahi tokea tangu kupatikana kwa uhuru.
1978, yakafanyika tena, pale Arusha, this time hali ilikuwa tofauti. Mh. Rais JK alifika hapo na akatangaza vita.
Baada ya vita JK akawa anajipanga jinsi ya kumrudisha Obote madarakani, kama mtakumbuka, baraza la kijeshi, Binaisa, Yusuf Lule n.k. Waganda hawakumtaka kabisa Obote pamoja na udikteta wa Mwalimu wa kuwachagulia Rais.
 
Iddi Amini hakutakiwa na Waingereza na Waisrail. Nyerere alisaidiwa sana kwenye vita.
 
Back
Top Bottom