Nini chanzo cha vita ya kagera?

TOURMALINE

Senior Member
Jan 4, 2013
125
24
Wana jf habari zenu
Naomba msaada wenu ili niweze kujua chanzo halisi cha vita ya kagera
Nawasilisha
 
Kwa hiyo chanzo kilikuwa ubabe wa Idd Amini au mzee wetu kufananishwa na binti.Mbona hapo celewi vizuri
 
Sakata zima lilianza tu baada ya IDD AMIN kumpindua kijeshi Rais MILTON OBOTE january 1971,IDD AMIN ambaye alipata mafunzo huko Israel kama askari wa miavuli(paratrooper)alikuwa karibu sana na Wa-ISRAEL na ndio waliomsaidia sana kuingia Madarakani wakisaidiwa na Mashirika ya Kijasusi ya UINGEREZA na ISRAEL.
Wakati huo ARAB WORLD ilikuwa inauguza vidonga vya kushindwa na ISRAEL katika vita vya siku 6 ambavyo ISRAEL ilionyesha UBABE wake katika MEDANI ya vita vya ardhini,angani na Majini.Gaddafi na Maofisa wengine vijana walikuwa madarakani wakati huo waliweza kwa kiasi fulani kuondoa unyonge huo katika nchi za Kiarabu.
Mwaka 1972 March Gaddafi alianza kufanya Mazungumzo ya siri na IDD AMIN na alimwomba avunje Mahusiano ya Kibalozi na ISRAEL na yeye GADDAFI angeweza kumpa misaada yoyote ya kijeshi na misaada mingine ya ki-uchumi na IDD AMIN alikubaliana naye na hapo hapo Balozi wa ISRAEL nchini Uganda alifukuzwa na kurudi kwao yeye pamoja na washauri wa mambo ya kijeshi wote hapo hapo GADDAFI alitoa 5,000,000USD.Hapo GADDAFI alipata sifa sana katika nchi za Kiarabu maana aliweza kukatilia Mbali Uhusiano wa Uganda na Israel na hapo hapo Libya ilianza kuweka Vitega uchumi vyake nchini Uganda.
IDD AMIN alilengwa sana na GADDAFI sababu yeye alikuwa Mwislamu na istoshe yeye alikuwa kama mtu mbabe sana na aliyefundishwa vizuri na ISRAEL hivyo ingekuwa tishio sana kwa nchi za Kiarabu ndiyo maana Gaddafi alimushawishi AMIN aunge mkono harakati za nchi za Kiarabu hasa kuhusu PALESTINA na alipokubali alizawadiwa zawadi nzuri pamoja na pesa ili kuinua uchumi wa UGANDA. Misaada hiyo aliahidiwa haiwezi kukoma mpaka mwisho wa utawala wake ndiyo maana hata Utawala wake ulipowekewa vikwazo na OAU wakati ule 1975 pamoja na nchi za magharibi kumwekea vikwazo lakini LIBYA na SAUD ARABIA waliendelea kumwaga misaada UGANDA na walilipa michango yote ya UGANDA huko OAU mwaka 1975.
Uhusiano kati ya Tanzania na Uganda uliendelea kuzorota baada tu ya IDD AMIN kumpindua MILTON OBOTE Mwaka 1971,Baada ya Mapinduzi hayo Rais Nyerere alimpa hifadhi ya kisiasa MILTON OBOTE pamoja na wakimbizi wengine 20,000 waliokimbia Utawala wa mabavu wa IDD AMIN,Baadaye mwaka 1972 wakimbizi wa Uganda walifanya jaribio lililoshindwa la kutaka kumpindua AMIN tokea Tanzania,Kitendo hicho kilimfanya AMIN alimshutumu sana Nyerere kuwa nyuma ya tukio hilo la kuwapatia silaha wafuasi wa MILTON OBOTE tokea hapo uhusiano wa Tanzania na Uganda ulizidi kuwa tete sana
Hatimaye Mwaka 1978 wapinzani wa IDD AMIN walivamia Ikulu ya Kampala lakini IDD AMIN aliweza kutoroka na Helicopter hii ilikuwa kipindi kigumu sana kwa IDD AMIN hasa alikosa maelewano na Makamu wake wa Rais wakati ule aliyekuwa anaitwa General MUSTAFA ADRISA aliyepata ajali kwa ajali ambayo ilihisiwa kuwa ilikuwa ya kupangwa na wale askari waliokuwa wanamuunga mkono walimuasi AMIN hivyo kupelekea askari hao kuvamia Ikulu ya Kampala,Kitendo hicho kilimfanya AMIN Kutuma askari wake watiifu kwenye kambi iliyokuwa inajulikana kama SIMBA BATTALION na kusababisha waasi kukimbilia Tanzania ambako kulikuwa na askari wenzao kutoka Uganda waliokuwa wakimpinga AMIN Kitendo ambacho AMIN kilimfanya awafuatilie huko waliko kwa matamushi yake mwenyewe alitumia dakika 25 tu kuteka eneo lote la kagera na kulitangaza eneo hilo kuwa sehemu ya UGANDA.
Katika uvamizi huo ambao ulihusisha zaidi ya askari 3,000 wenye silaha za kisasa wakti huo,Majeshi ya Uganda yaliyokuwa hayana Nidhamu walianza kwa Kuwabaka wanawake na walipora vitu mbali mbali vijiji viliteketezwa Makanisa yaliharibiwa vilevile waliweza kupora mashine nzito,Mabati,Magari,Mabomba pia yaliharibiwa shule pamoja na Hospitali hazikuweza kubaki salama mbele ya askari wa Amin,Miji jirani na Bukoba ilifulika wakimbizi waliokuwa wakikimbia toka uwanja wa mapambano ambao AMIN alisema aliweza kukalia eneo hilo kwa mwendo wa SUPERSONIC yaani dakika 25 tu na kilifanya eneo la UGANDA. ndipo Majeshi ya Tanzania yalipoingia vitani na ukawa ndio mwanzo wa VITA VYA KAGERA.
 
Kwa history hiyo ya mdau 1 hapo juu inaonyesha kabisa kua Nyerere ndiye aliye mchokoza Iddi Amin, nachanzo cha yote nikutaka kumrudisha mkiristo mwenzie madarakani. Hii tunaweza iita ilikua ni vita ya msalaba aliyo pigana Nyerere kuimarisha kanisa ktk ukanda huu wa Africa mashariki.
 
Nakuomba sana usiingize DINI harakaharaka angalia pande zote vaa na wewe uhusika uone kama wewe ndo ungekuwa Nyerere ungemtendeaje Rafiki yako Dhidi ya ADUI yake????.
Kwa history hiyo ya mdau 1 hapo juu inaonyesha kabisa kua Nyerere ndiye aliye mchokoza Iddi Amin, nachanzo cha yote nikutaka kumrudisha mkiristo mwenzie madarakani. Hii tunaweza iita ilikua ni vita ya msalaba aliyo pigana Nyerere kuimarisha kanisa ktk ukanda huu wa Africa mashariki.
 
hiyo vita haikuhusisha udini, ila maoni ya msomaji tu, idi amini alitaka kuonyesha ubabe wake lakini majeshi yetu yalikaa imara
Mungu ibariki tanzania
 
echolima kashasema ukweli hapo juu!!!! ukweli ni kwamba nyerere ndio alikua mchokozi na ndio maana baada ya vita hakuna nchi nyingine kwenye OAU iliyokubali kulipia cost za peacekeeping uganda wakat serikali mpya ikijenga instituitions na kutokna na cost hizo uchumi wa TZ haukuweza ku-recover pamoja na kwamba chini ya nyerere viwanda na uzalishaji ulikua juu!!!! cost za hii vita na peacekeeping ndio zimetufilisi we love nyerere lakini kwa apa alikosea... alitakiwa baada ya kuigomboa kagera basi angetuliza mpira!!!
 
...hivi jirani yako akiingia nyumbani kwako akawaingilia watoto, pia akambaka mkeo, na ukamkuta bado amelala chumbani kitandani kwako;
Unataka kutwambia kwamba ukisha mtoa ndani ya nyumba yako basi?
 
ni afadhali nchi yenye uchumi mdogo kuliko nch isiyojali wananchi wake, mafisadi ni wengi kuliko waaminifu, that is why uchumi hauja'recover'
 
Iddi Amini ( Allah amrehemu) alimwambia JK Nyerere " unaongea sana mwanamama" kie kie kie kie
 
echolima kashasema ukweli hapo juu!!!! ukweli ni kwamba nyerere ndio alikua mchokozi na ndio maana baada ya vita hakuna nchi nyingine kwenye OAU iliyokubali kulipia cost za peacekeeping uganda wakat serikali mpya ikijenga instituitions na kutokna na cost hizo uchumi wa TZ haukuweza ku-recover pamoja na kwamba chini ya nyerere viwanda na uzalishaji ulikua juu!!!! cost za hii vita na peacekeeping ndio zimetufilisi we love nyerere lakini kwa apa alikosea... alitakiwa baada ya kuigomboa kagera basi angetuliza mpira!!!

umetanguliza zaidi udini badala ya kuutafakari ukweli, amini na gadafi ndiyo waliokuwa wadini, hamnataifa lililomsaidia nyerere kwa ukristo wake lakini gadafi alimsaidia amini kwa vile tu ni mwislamu na akasahau ukweli na haukuchukua muda yakamrudi! vile vile kumbuka wakati na baada ya vita ya kagera maraisi wengi walikuwa wakristo hivyo isinekuwa nongwa kwao kumsupport nyerere kama issue ilikuwa kuupinga uislamu, TAFAKARI MAOVU YA IDD AMINI KAMA YALIVO YA KAGAME. Nyerere angekuwa mdini asingewaunga mkono wapalestina na awaache waisraeli, asingetaifisha shule za kanisa kwa ajili ya wakristo na kuzifanya za kitaifa kutoa elimu kwa wote, tafakari acha utoto najua ndiyo mnayofundishwa misikitini.
 
''ndiyo mnayofundishwa misikitini'' Tafadhali chunga mdomo wako kijana.
 
Back
Top Bottom